Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Wadau amani iwe kwenu.
Hali ndani ya UKAWA inazidi kuwa tete. Mtakumbuka kuwa UKAWA walipanga kutangaza jina la Mgombea atakayepeperusha bendera ya Umoja wao Julai 11. Hata hivyo, kutokana na sababu ambazo hazikuelezwa bayana, mgombea wao hakutangazwa siku hiyo na badala yake wakasema kuwa watamtangaza Julai 14.
Hata hivyo, kwa mara nyingine tena, UKAWA wameshindwa kuafikiana hali iliyosababisha wasogeze mbele siku ya kumtangaza mgombea wao hadi siku tano zijazo. Bahati mbaya sana kauli hii haikutolewa na UKAWA bali ilitolewa na CHADEMA pekee hasa baada ya viongozi wa CUF kususia vikao vya jana.
HOJA ZA CUF NDANI YA UKAWA
Kwa ujumla CUF ni kama wameshajitoa ndani ya UKAWA. Hoja wanazotoa ni hizi zifuatazo.
Mytake: UKAWA wamevurugana. Kilichowavuruga zaidi ni baada ya CCM kubadili upepo kwa kumsimamisha Magufuli. Hali hii imewachanganya sana UKAWA kwani walitegemea kuwa CCM ingemteua ama Lowasa ama Membe hali ambayo ingewafanya watambe kwenye majukwaa. Na bado.

- Wanapinga kitendo cha CHADEMA kung'ang'ania kupata mgawo wa asilimia 70 ya nafasi za ubunge na asilimia 80 ya nafasi za udiwani. Kwamba, Viongozi wa CHADEMA wanasisitiza kuwa wapewe mgawo wa viti asilimia 70 na vyama vingine vigawane asilimia 30 zinazobaki. CUF wanasema kuwa wakati wanaingia kwenye umoja huo, walikuwa vyama vyenye hadhi sawa bila kujali idadi ya wabunge. Wanasema kuwa hata maamuzi ya awali hayakufanywa kwa muktadha wa idadi ya wabunge. Sasa wanawashangaa CHADEMA wamebadilika ghafla na hivyo CUF wana kila sababu ya kuhoji kuna nini nyuma ya pazia
- CUF wanapinga kitendo cha CHADEMA kulazimisha wasimamishe mgombea Urais kwa madai kuwa wao ni chama kikubwa na kina wafuasi wengi. Viongozi wa CUF wanasisitiza kuwa kama CHADEMA wangekuwa na wafuasi wengi, kwa nini hawakushinda kwenye chaguzi za nyuma waliposimamisha mgombea wao? Kutokana na hali hiyo, CUF wanasema kuwa CHADEMA wana uroho wa madaraka na kwamba huenda wakawageuka baada ya uchaguzi kama wakishinda uchaguzi huo. Kwamba, CHADEMA wanataka kuvitumia tu vyama vingine kushinda na huenda watawageuka baada ya uchaguzi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba umoja wao haupo kisheria na kwamba mgombea atakayeshinda atahesabika kuwa ni mgombea wa chama na si UKAWA.
- CHADEMA hawaaminiki. CUF wanaona kuwa CHADEMA ni walaghai. Kwamba waliposhinda idadi kubwa ya viti vya wabunge mwaka 2010, hawakutaka kushirikiana na vyama vingine kuunda serikali kivuli bungeni. Kwa hali hiyo wamenusa harufu ya kusalitiwa baadaye hali itakayoleta mtafaruku ndani ya umoja wao.
- CUF wanapinga uamuzi wa CHADEMA kutaka kumuweka Dr Slaa juu ya Prof Lipumba. Kwamba, wao wanaona kuwa kati ya wanasiasa hao wawili, ni Prof Lipumba ndiye mwenye hadhi ya kuwa mkuu wa nchi na si Dr Slaa kutokana na taswira yake kwenye jamii kuwa mbaya.
- Mgawanyo wa ruzuku haujawekwa sawa. Kwamba, kwa mujibu wa sheria za sasa, chama chenye wabunge wengi ndicho kitakachopata kiwango kikubwa cha fedha za ruzuku. CUF wanasisitiza kuwe na makubaliano rasmi ya kugawanya ruzuku hiyo miongoni mwa vyama washirika kwa uwiano sawa. Hata hivyo, hoja hiyo inakataliwa na CHADEMA.
- Mgawanyo wa viti maalum vya wabunge. CUF inataka viti maalum vya wabunge vigawanywe sawa miongoni mwa vyama washirika vinavyounda UKAWA. Hoja yao inatokana na ukweli kwamba, viti maalum vitapatikana kutokana na idadi ya kura atakazopata mgombea urais. kwa vile mgombea huyo atasimamishwa na UKAWA, basi idadi ya viti maalum itakayopatikana igawanywe sawa. hata hivyo, CHADEMA wanataka kuwa kusiwe na uwiano sawa kutokana na hadhi ya vyama hivyo kutofautiana.