Kumekucha UKAWA: Lipumba kutoa msimamo wa CUF leo saa tano Asubuhi

Prof hasomi mwelekeo wa upepo???

Atausoma kwa kukosa nini? Kazi aliyotumwa ameimaliza. Mimi nawalaumu sana chadema kwani toka wanaunganisha hizo nguvu kuzaa ukawa nilielewa ni kwa masuala ya kutetea katiba mpya na nzuri basi na sio zaidi ya hapo. Kuungana kumteua raisi mmoja na kuachiana majimbo mlipenda kujiua na kujicheleweshea maendeleo wenyewe.Sasa siku za mbele msijepitisha maamuzi mazito kama yale bila kuwashirikisha wanachama wenu ni hatari sana. Viongozi wangechukua maoni ya wanachama wao ambao wangewapa faida na hasara zake haswa kwa siasa na misimamo ya baadhi ya viongozi wa baadhi ya vyama isiyotabirika msingeleta matatizo makubwa. Hivi kweli wakati mnaungana na cuf mlikuwa mmeshasahau uchaguzi wa 2010 Lipumba alikiri kumpigia kampeni Kikwete eti kwa kuwa alimwona kuzidiwa? Usaliti huu kwa wananchi aliowawakilisha na kwa upinzani aliuombea lini msamaha? Ni kwa nini hamkuyajadili kwanza kwa kuweka misingi(criteria) ya haya anayoyaona sasa kama mapungufu yanayohitaji makubaliano kwanza? Ni kwa nini hata huo ukawa haukuandikishwa kabisa na kuwa na katiba yake ambayo ingetoa suluhu kwa haya yanayooneoana ni matatizo?Sasa muda mliobakia nao mnaamini mnaweza kuyarekebisha yote hayo kabla ya kampeni kuruhusiwa rasmi? Kwa hali hii ilivyo ni bora muungane mnaokubaliana na mtangaze mgombea wenu.
 
acha Hasira Mkuu km sio Lizabonitungejuaje kuwa UKAWA imekufa?
mlivyokuwa mkibwabwaja na kumtusi JK ilikuwa ni Jukwaa gani
au kumpendekeza Lowassa awe mgombea kupitia CCM ili mje mumuweke Slaa mpige bao mlidhani wote ni wajinga
attachment.php

Aahha watu wamemaliza kazi IKAWA quishney

Saa tano bado tuuu
 
Yetu macho mwaka huu lazima utabiri wa Askofu Kakobe utimie.

CCM inakuwa chama cha Upinzani ndani ya Bunge. wenye akili wameshaanza kukimbia na kujiunga na umoja wa Wazalendo (UKAWA)

Mh. James Lembeli na bado wengi wenye akili watakuja UKAWA tu.

CCM itabaki na MAFISADI.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Hata SHIBUDA alipokelewa kama Lembeli baadae kageuka kuwa mwiba..Selasini nae alitokea NCCR akapokwe cdm sasa hivi kawa msaliti..Siasa za tz tema mate chini usimalize maneno mkuu weka na akiba.Hushangai majuzi tu Lowassa alitangazwa fisadi Muembe Yanga na Slaa leo hii kawa lulu anatakiwa kugombea urais kwa mgongo wa ukawa.politiki za tz usipime
 
Hata SHIBUDA alipokelewa kama Lembeli baadae kageuka kuwa mwiba..Selasini nae alitokea NCCR akapokwe cdm sasa hivi kawa msaliti..Siasa za tz tema mate chini usimalize maneno mkuu weka na akiba.Hushangai majuzi tu Lowassa alitangazwa fisadi Muembe Yanga na Slaa leo hii kawa lulu anatakiwa kugombea urais kwa mgongo wa ukawa.politiki za tz usipime


Mkuu haitakuwa tatizo hata wakienda CHADEMA mwaka huu na mwakani wakahama hakuna shinda kwani wameshaiunga mkono UKAWA uchaguzi wa mwaka huu ili tupunguze Wabunge na Madiwani CCM katika vyombo vya kutunga sheria ambapo tutakuwa na uhakika ile Katiba ya Wananchi itarudishwa tena mjengoni.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Back
Top Bottom