Kumekucha UKAWA: Lipumba kutoa msimamo wa CUF leo saa tano Asubuhi

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wadau amani iwe kwenu.

Hali ndani ya UKAWA inazidi kuwa tete. Mtakumbuka kuwa UKAWA walipanga kutangaza jina la Mgombea atakayepeperusha bendera ya Umoja wao Julai 11. Hata hivyo, kutokana na sababu ambazo hazikuelezwa bayana, mgombea wao hakutangazwa siku hiyo na badala yake wakasema kuwa watamtangaza Julai 14.

Hata hivyo, kwa mara nyingine tena, UKAWA wameshindwa kuafikiana hali iliyosababisha wasogeze mbele siku ya kumtangaza mgombea wao hadi siku tano zijazo. Bahati mbaya sana kauli hii haikutolewa na UKAWA bali ilitolewa na CHADEMA pekee hasa baada ya viongozi wa CUF kususia vikao vya jana.

HOJA ZA CUF NDANI YA UKAWA
Kwa ujumla CUF ni kama wameshajitoa ndani ya UKAWA. Hoja wanazotoa ni hizi zifuatazo.

  1. Wanapinga kitendo cha CHADEMA kung'ang'ania kupata mgawo wa asilimia 70 ya nafasi za ubunge na asilimia 80 ya nafasi za udiwani. Kwamba, Viongozi wa CHADEMA wanasisitiza kuwa wapewe mgawo wa viti asilimia 70 na vyama vingine vigawane asilimia 30 zinazobaki. CUF wanasema kuwa wakati wanaingia kwenye umoja huo, walikuwa vyama vyenye hadhi sawa bila kujali idadi ya wabunge. Wanasema kuwa hata maamuzi ya awali hayakufanywa kwa muktadha wa idadi ya wabunge. Sasa wanawashangaa CHADEMA wamebadilika ghafla na hivyo CUF wana kila sababu ya kuhoji kuna nini nyuma ya pazia
  2. CUF wanapinga kitendo cha CHADEMA kulazimisha wasimamishe mgombea Urais kwa madai kuwa wao ni chama kikubwa na kina wafuasi wengi. Viongozi wa CUF wanasisitiza kuwa kama CHADEMA wangekuwa na wafuasi wengi, kwa nini hawakushinda kwenye chaguzi za nyuma waliposimamisha mgombea wao? Kutokana na hali hiyo, CUF wanasema kuwa CHADEMA wana uroho wa madaraka na kwamba huenda wakawageuka baada ya uchaguzi kama wakishinda uchaguzi huo. Kwamba, CHADEMA wanataka kuvitumia tu vyama vingine kushinda na huenda watawageuka baada ya uchaguzi. Hii ni kutokana na ukweli kwamba umoja wao haupo kisheria na kwamba mgombea atakayeshinda atahesabika kuwa ni mgombea wa chama na si UKAWA.
  3. CHADEMA hawaaminiki. CUF wanaona kuwa CHADEMA ni walaghai. Kwamba waliposhinda idadi kubwa ya viti vya wabunge mwaka 2010, hawakutaka kushirikiana na vyama vingine kuunda serikali kivuli bungeni. Kwa hali hiyo wamenusa harufu ya kusalitiwa baadaye hali itakayoleta mtafaruku ndani ya umoja wao.
  4. CUF wanapinga uamuzi wa CHADEMA kutaka kumuweka Dr Slaa juu ya Prof Lipumba. Kwamba, wao wanaona kuwa kati ya wanasiasa hao wawili, ni Prof Lipumba ndiye mwenye hadhi ya kuwa mkuu wa nchi na si Dr Slaa kutokana na taswira yake kwenye jamii kuwa mbaya.
  5. Mgawanyo wa ruzuku haujawekwa sawa. Kwamba, kwa mujibu wa sheria za sasa, chama chenye wabunge wengi ndicho kitakachopata kiwango kikubwa cha fedha za ruzuku. CUF wanasisitiza kuwe na makubaliano rasmi ya kugawanya ruzuku hiyo miongoni mwa vyama washirika kwa uwiano sawa. Hata hivyo, hoja hiyo inakataliwa na CHADEMA.
  6. Mgawanyo wa viti maalum vya wabunge. CUF inataka viti maalum vya wabunge vigawanywe sawa miongoni mwa vyama washirika vinavyounda UKAWA. Hoja yao inatokana na ukweli kwamba, viti maalum vitapatikana kutokana na idadi ya kura atakazopata mgombea urais. kwa vile mgombea huyo atasimamishwa na UKAWA, basi idadi ya viti maalum itakayopatikana igawanywe sawa. hata hivyo, CHADEMA wanataka kuwa kusiwe na uwiano sawa kutokana na hadhi ya vyama hivyo kutofautiana.
Kutokana na hoja hizi na nyingine ambazo hazijawa revealed, CUF wanaona kuwa CHADEMA wana ajenda ya siri ndani ya umoja huo. Hivyo hofu waliyonayo juu ya CHADEMA ni sahihi na wanapaswa kupata muda zaidi wa kujitafakari. Kwamba, wamepata maoni kutoka kwa wanachama na wafuasi wao na kutokana na maoni hayo, CUF watatoa msimamo wa chama leo ambapo Prof Lipumba ataitisha kikao na Waandish wa Habari Kwenye Ofisi za CUF Buguruni kuanzia saa tano asubuhi.

Mytake: UKAWA wamevurugana. Kilichowavuruga zaidi ni baada ya CCM kubadili upepo kwa kumsimamisha Magufuli. Hali hii imewachanganya sana UKAWA kwani walitegemea kuwa CCM ingemteua ama Lowasa ama Membe hali ambayo ingewafanya watambe kwenye majukwaa. Na bado.
 
Walishindwa kupata majibu ya mgombea wa ukawa kabla ya ccm kumtangaza magufuli,sasa katangazwa magufuli ndiyo wamevurugwa kabisa maana hazina ya ukawa ni slaa na lipumba,na hawatoshi kwa magufuli
 
Walishindwa kupata majibu ya mgombea wa ukawa kabla ya ccm kumtangaza magufuli,sasa katangazwa magufuli ndiyo wamevurugwa kabisa maana hazina ya ukawa ni slaa na lipumba,na hawatoshi kwa magufuli
Kweli kabisa Mkuu
 
Lipumba amekubali kuthariti Mabadiliko kwani Wao CUF wametoa taarifa kwanini Vyama vinavyounda Ukawa vimemuunga Mkono maalim Seif kule Zanzibar? Lipumba amegombea Urais Kwa vipindi vinne lkn kila mwaka Nguvu yake Ilipungua kwasababu hakuwa na Mbinu mpya nakwa Ubinafsi huu Anatafuta Aibu..!
 
Naona umeandika kwa mbwembwe nyingi ukifikiri kuwa kama CUF watajiondoa UKAWA ndiyo mtasalimika na kipigo,kipigo bado kipo palepale CHADEMA peke yake wanawamudu CCM.
 
Lipumba amekubali kuthariti Mabadiliko kwani Wao CUF wametoa taarifa kwanini Vyama vinavyounda Ukawa vimemuunga Mkono maalim Seif kule Zanzibar? Lipumba amegombea Urais Kwa vipindi vinne lkn kila mwaka Nguvu yake Ilipungua kwasababu hakuwa na Mbinu mpya nakwa Ubinafsi huu Anatafuta Aibu..!
Hoja hizo si za Lipumba bali ni za CUF. Kuhusu vyama vingine kutosimamisha mgombea kule Zanzibar, naomba unijulishe ni lini CHADEMA waliwahimkusimamisha mgombea ubunge na Urais Zanzibar
 
Mambo yameiva kama mlivyoona ccm wamishaanzakampeni kimya kimya, hivyo basi tunawaomba vyama vitavyokubali ukawa tangazeni mgombea bila kuchelewa, baada ya kutangaza mgombea andaeni utaratibu wa kuzindua harambee, wazalendo tupo tayari kuwachangia, ili mwingie ikulu kwa nguvu na rasilimali za umma,
 
Taswira ya dr slaa n mbaya mbele ya jamii, ebu thibitisha hilo.

Na hii taarifa unayotoa ebu thibitisha kama ndo maazimio ya chama cha CUF au unaota kutoa taarifa ambayo ni mfu
 
Back
Top Bottom