Ili account ya kampuni ifunguliwe katika benki yoyote ni lazima kuwe na site visit ( Relationship/Account manager) lazima afike kwenye office inayotarajia kufungua akaunti na pia kuna kitu kinaitwa company search,black list check for all directore and signatories (mabenki mengine huita Norkom) ili kujiridhisha kuwa directors hawajawa black listed! KYC na AML lazima zifanyiwe kazi vizuri.
Wasiwasi wangu ni kama hayo yalifanyika,ikumbukwe kwa wakati huo benki hiyo ilikuwa chini ya managing director aitwaye Bashir Awale,ni mtoto wa mjini ukute hii akaunti ilianzia juu kisha ikashushwa chini,sasa mara nyingi akaunti za kuanzia juu huskip KYC vibaya mno! RM ukute kasainishwa tu bila kujua anasaini nini,na mabenki yetu haya RM's hupewa target za kufa mtu, hapa RM atakuwa aliambiwa kuwa akaunti itawekewa USD 122million lazima alipagawa coz aliona bonus anayoenda kupata ni ya kufa mtu...sidhani kama hata alikumbuka kucheck black list, ingawa kiuhalisia akaunti kama hizo huwa zinaangukia kwenye EDD yaani Enhanced Due Deligence,ambazo huhitaji kuangaliwa sana kiundani na kufunguliwa ni mpaka head wa compliance aweke mkono wake!
Kufunguliwa tu kwa akaunti kuatchukua mlolongo wa watu...achilia mbali pesa kuchotwa...
Kuna inernal auditors ambao kazi yao ni kupitia mafaili, kuna mtu wa risk pia withdrawal kubwa inapopita kwenye account lazima inatoka kwenye report ya exceptional report....sijui waliandika vitu gani hao waliocheck report....
Stanbic ni vigumu sana kukwepa saga hili kama regulator ataamua kumfuatilia,hawa jamaa walichofanya hakina tofauti na walichofanya FBME kule Syprus!