I am Groot
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,727
- 10,023
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo amesema Wizara hiyo inatarajia kufanya utafiti mkubwa na usanifu wa mradi mkubwa wa maji wa kuchukua maji kutoka Ziwa Victoria kupeleka Mkoani Dodoma kwa kupitia Mkoani Singida katika mwaka wa fedha wa 2020/2021>>”hii itaondoa kabisa shida ya maji Dodoma na Singida”
•
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof.Kitila Mkumbo alitoa kauli hiyo kwenye hafla ya kupokea mabomba ya maji ambayo ni sehemu ya Programu kubwa inayotekelezwa kwa nchi nzima katika mikoa 17, Singida ikiwa ni moja ya Mikoa hiyo.
•
Mkumbo amesema fedha za mradi wa kutoa maji Ziwa Victoria kupeleka Dodoma kupitia Singida tayari zimetengwa katika bajeti ya mwaka huu wa fedha, hivyo anaamini kipindi cha miaka 5 ijayo Singida na Dodoma wanaweza kupata maji kutoka Ziwa Victoria.
Source; millard ayo