GE2025 Kumekucha, CCM Njombe waanza Kampeni kwa mabango kabla ya muda

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,446
Reaction score
2,093
Haya sasa mambo yapo nje ya muda, yaani CCM mwaka huu hata hawaogopi ni mambo hadharani kuvunja kanuni na sheria za nchi na hawachukuliwi hatua.

Hapo ingekuwa ni CHADEMA tayari huyo mgombea angefutwa na kuondolewa kuwania tena Tume ya uchaguzi wangeshatangaza ila kwa sababu ni CCM ni kama hawaoni

---------------------
Sigrada Mligo ambaye ni Mgombea Ubunge kwa Jimbo la Njombe Mjini kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) amelalamikia uvunjwaji wa kanuni za kiuchaguzi kutokana na Mgombea Ubunge wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) kwa Jimbo hilo Deo Mwanyika kuanza kufanya kampeni akiwa bado hajateuliwa bado na Tume Huru ya Uchaguzi (INEC).

Akizungumza na Jambo TV leo Agosti 27, 2025 Sigrada amesema ameshangazwa na kitendo kilichofanywa na Mwanyika cha kuanza kubandika mabango ya kampeni usiku wa kuamkia leo pamoja na asubuhi ikiwa Tume bado haijafanya uteuzi

"Maelekezo tuliyokuwa tumepewa na msimamizi wa Uchaguzi ni kwamba huruhusiwi kufanya kampeni kabla ya uteuzi lakini cha ajabu zaidi mtia nia mwenzangu toka jana usiku naona yametandazwa mabango mji mzima" amesema Sigrada

Jambo TV imezungumza na Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo, Samson Medda ambaye amekiri kupokea malalamiko hayo leo asubuhi akisema kuwa ameanza kuyafuatilia na pindi ikithibitika hatua zitachukuliwa

“tumepokea taarifa muda sio mrefu tunafanya ufuatiliaji kujua uhalisia” amesema Medda

Ameongeza kuwa ikiwa imethibitika mgombea anaweza kuwekewa pingamizi na endapo waliotoa malalamiko watafanya hivyo hatua zitachukuliwa

“kanuni zinaelekeza wapo watu ambao wana mamlaka ya kuweka pingamizi endapo watafanya hivyo sisi tutashughulikia kwa mujibu wa kanuni” ameeleza Medda

sigrada alikuwa very smart wakati Msigwa kwenda CCM, kumbe nalo hovyo...
 
Sigrada rudi Chadema mjenge demokrasia
 
  • Kicheko
Reactions: Lax
Sigrada Mligo ambaye ni Mgombea Ubunge kwa Jimbo la Njombe Mjini kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) amelalamikia uvunjwaji wa kanuni za kiuchaguzi kutokana na Mgombea Ubunge wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) kwa Jimbo hilo Deo Mwanyika kuanza kufanya kampeni akiwa bado hajateuliwa bado na Tume Huru ya Uchaguzi (INEC).

Akizungumza na Jambo TV leo Agosti 27, 2025 Sigrada amesema ameshangazwa na kitendo kilichofanywa na Mwanyika cha kuanza kubandika mabango ya kampeni usiku wa kuamkia leo pamoja na asubuhi ikiwa Tume bado haijafanya uteuzi.

Soma pia: Deo Mwanyika achukua Fomu ya Kugombea Ubunge kwa awamu ya Pili Jimbo la Njombe Mjini

"Maelekezo tuliyokuwa tumepewa na msimamizi wa Uchaguzi ni kwamba huruhusiwi kufanya kampeni kabla ya uteuzi lakini cha ajabu zaidi mtia nia mwenzangu toka jana usiku naona yametandazwa mabango mji mzima" amesema Sigrada

Jambo TV imezungumza na Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo, Samson Medda ambaye amekiri kupokea malalamiko hayo leo asubuhi akisema kuwa ameanza kuyafuatilia na pindi ikithibitika hatua zitachukuliwa.

“tumepokea taarifa muda sio mrefu tunafanya ufuatiliaji kujua uhalisia” amesema Medda

Ameongeza kuwa ikiwa imethibitika mgombea anaweza kuwekewa pingamizi na endapo waliotoa malalamiko watafanya hivyo hatua zitachukuliwa.

Back
Top Bottom