Wajameni... Leo naomba tusaidiane kujadili jinsi tunavyowadhalilisha wapenzi wetu in the name of love and protection
Kuna rafiki yangu ana kaugonjwa kabaya sana ka kumnyang'anya mkewe simu na kukaa nazo hata siku mbili kusubiria nani atampigia mkewe... i tried to ask him kuacha tabia hiyo kwani inamweka mwanamke kwenye hisia za kudhalilishwa na kutoaminiwa na pia mke anaweza sasa akaanza kufanya siyodhani simply because jamaa ndicho alichonacho kichwani!!
Sipendi hii tabia na nina imani wengi hamuipendi
please pals, lets not do this aisee
swahiba, and that is my spirit...
this dude anatudhalilisha and i hope anaingia JF.... ukimuona huwezi amini
Huo ni unyanyasaji wa kijinsia!Mwambie ache ujinga au kama anataka hata kazini/chooni/bar awe anaenda nae ili hata salamu asipewe au akipewa ajue!!
Babu hizo ni lawama nyingine all together!!Ndo yale yale ya kungangania...kunyenyekea...kutulia na kuwa mdogo hata sehemu zisizohusu!!Ila wakati mwingine wanawake nao wanatakiwa kubeba sehemu ya lawama..Yaana unakubali mtu akunyanyase kiasi hicho kwa sababu ndiye anakumegea hewa ya kupua au?
Babu hizo ni lawama nyingine all together!!Ndo yale yale ya kung‘ang‘ania...kunyenyekea...kutulia na kuwa mdogo hata sehemu zisizohusu!!
Hahahaha!!Babu hiyo ya kutoa taarifa (SIO KUOMBA RUHUSA) wakati mmoja anapoenda kuonana na rafiki wa mwenzake naisupport 105%...sema iwe kwa pande zote.Ni ustaarabu na common sense pia.Ila bado nakubaliana na wewe kwamba wenyewe ndio tunaoruhusu hali ya kuonewa.Wale waojiweka kwenye mazingira yanayoepusha hayo ndo wale tunaitwa wanaharakati na wakorofi...mwisho wa siku mtu anaogopa kua branded majina haya anaruhusu kukanyagwa kichwa mpaka macho.Inasikitisha kweli mmoja anapoona ana haki ya kumfanya mwenzake kama KITU badala ya MTU...yani anakua hapewi haki yoyote ile!Ila Lizzy utakubaliana na mimi kwamba wanawake ndio tatizo kubwa katika mchakato mzima wa ukombozi wa mabinti na wajukuu zetu wa kike? Nadhani umeona jinsi ambavyo wanawake wenyewe wana-confess kwamba hawawezi kwenda kukutana na mtu yeyote (kama vile shemeji) bila sijui kutoa taaria, mara kuomba ruhusa au consent ya mume!! Nimechoka mie....Hivi wanaume ni miungu wa wanawake???
Hahahaha!!Babu hiyo ya kutoa taarifa (SIO KUOMBA RUHUSA) wakati mmoja anapoenda kuonana na rafiki wa mwenzake naisupport 105%...sema iwe kwa pande zote.Ni ustaarabu na common sense pia.Ila bado nakubaliana na wewe kwamba wenyewe ndio tunaoruhusu hali ya kuonewa.Wale waojiweka kwenye mazingira yanayoepusha hayo ndo wale tunaitwa wanaharakati na wakorofi...mwisho wa siku mtu anaogopa kua branded majina haya anaruhusu kukanyagwa kichwa mpaka macho.Inasikitisha kweli mmoja anapoona ana haki ya kumfanya mwenzake kama KITU badala ya MTU...yani anakua hapewi haki yoyote ile!
Kweli kabisa!!Nikibarikiwa kuwa na kabinti ntakafundisha kua kakorofi kama mimi!!Basi wafundishe watoto wenu kutafakari na kuchukua hatua....Kuna jamaa alihubiri kuwa ukifanya mkeo kama chombo unamfanya valueless! Ila mbaya zaidi ni pale mwanamke anapojifanya au kuruhusu kufanywa chombo......Then value yake inakuwa closer to zero!!