Kumdai mfiwa niianze lini?

Kumdai mfiwa niianze lini?

Una ushahidi wowote kwamba ulimpatia pesa na akurudishie baada ya msiba?
Tulipeana kwa kuaminiana Sana ndugu yangu, na hajawahi kukataa kuwa simdai, anachonishangaza ni kuwa BADO HAJAMALIZA MSIBA
 
Honestly una ukuu ndani yako, Naweza kukuelewa kupitia thread na comments zako hapa. Hebu jaribu kumweleza jambo hilo ili atambue kama unakelekwa nalo na uwe muwazi kwake kama unahitaji pesa yako. Acha kunung'unika pembeni while uwezo wa kumweleza unao.

Na kama hatojali basi samehe kabsa na uendekee ma maisha mengine.
Hakika ushauri huu naubeba kwa mikono miwili.. Nahisi harufu ya kuvunjika kwa undugu kisa Pesa, Jambo ambalo ntajitahidi Sana kulizuia kwa kukubali kusamehe
 
Yaani hii awamu ukitaka kugombana na mtu mkopeshe.
Watu hawaaminiki kabisa.
Ataomba kwa huruma ila kwenye kulipa sasa wewe mlipwaji ndii utatia huruma.
Kweli kabisa hata wale usiotarajia ukiwakopesha tu subiria kuangukia pua.
 
Ni vile tu pua hazinusi yajayo... Labda ningempatia tu ile ambayo niliitoa kama Rambirambi
Wakati anaomba umkopeshe yeye mwenyewe aliahidi kulipa hiyo pesa baada ya muda gani? Maana kama hakuweka time frame ya ulipaji basi hapo unaweza kuendelea kuhesabu maumivu kwa muda mrefu kidogo. Wengine hayo yalishawahi kututokea na tunaendelea kusikilizia maumivu hadi hii leo. Pole sana.
 
Wakati anaomba umkopeshe yeye mwenyewe aliahidi kulipa hiyo pesa baada ya muda gani? Maana kama hakuweka time frame ya ulipaji basi hapo unaweza kuendelea kuhesabu maumivu kwa muda mrefu kidogo. Wengine hayo yalishawahi kututokea na tunaendelea kusikilizia maumivu hadi hii leo. Pole sana.
Doh!!! Hili Ni Kubwa na la muhimu mno!! Kweli hatukuwekeana muda!! Ila kwa akili yangu nilitegemea yaliponikuta nami ya kufiwa ungekuwa ni wakati muafaka was kurudisha...
 
Nakushauri hivi;
Kwanza sijui dini yako ila kwa dini ya kikristo, biblia ipo wazi kabisa kuwa; Akopeshaye asitegemee kurudishiwa. Amua tu kuwa, Nilimkopesha Mungu na Mungu atakulipa.
Jambo la pili; Nadhani ulisema nyiye ni marafiki. Basi elewa kuwa Urafiki gharama. Hii nayo ndio gharama yako. Usimsumbue tena ili ajisahau. Siku isojulikana atajisahau akupe fedha hata kama ni ya kupeleka mahali. Nawe jifanye umejisahau ukazitumia. Akikuuliza, mpe sababu ilokufanya ukazitumia. Akipamba moto, mkumbushe tu kuwa, Zipunguze paleeee.
 
2M ni nyingi kwa kweli. Kwanini usimuambie akukopeshe labda 3M hivi?

Akikukopa ndipo hela yako iwe imerudi?

Ila nahisi kama na yeye yupo humu anaangalia tu sound utakazompelekea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom