Habari wanajamvi,
Katika safari ya maisha, kuna watu ambao huwa wa karibu sana kiasi kwamba wanapohitaji msaada wa kifedha unawasaidia bila kusita, kutokana na heshima na uaminifu mliojenga kwa miaka mingi. Hilo ndilo lililonikuta mimi.
Kuna rafiki yangu wa muda mrefu ambaye tumekuwa tukiheshimiana sana. Ni mtumishi wa umma mwenye kipato cha uhakika katika moja ya taasisi zinazoheshimika hapa nchini. Takribani mwaka mmoja uliopita aliniomba nimkopeshe kiasi cha shilingi milioni 10 ili aongezee mtaji kwenye biashara aliyokuwa akiifanya pamoja na marafiki zake aliokutana nao ukubwani.
Mimi sikuwa nawafahamu hao washirika wake, lakini kutokana na historia yetu nzuri ya urafiki na kuaminiana, nilimkopesha bila hiyana, kwa makubaliano kwamba angenirejeshea pesa hiyo ndani ya miezi mitatu pamoja na bakshishi ndogo ya shukrani.
Fast forward, leo ni zaidi ya miezi 15 imepita na bado hajarejesha fedha hiyo. Sababu anazotoa ni kwamba baadhi ya biashara walizoanzisha zilifeli, nyingine zinaendelea kwa faida ndogo sana, na katika moja ya biashara hizo mmoja wa washirika alitoroka na kiasi kikubwa cha fedha.
Kutokana na hali hiyo, amenieleza kuwa kwa sasa hawezi kumudu kunilipa fedha yangu kwa mkupuo. Badala yake, amenipa pendekezo kwamba fedha kidogo iliyobaki baada ya kupata hasara hiyo aliiongezea kwa mkopo wa benki na kununua hekari 100 za shamba la mikorosho huko Mtwara.
Sasa anashauri badala ya kunirudishia fedha taslimu, anipatie hekari 30 za shamba hilo, ambazo ataendelea kuzihudumia kwa gharama zake mpaka mavuno yatakapopatikana, kisha nijilipe kupitia mauzo ya korosho hizo na hatimaye nimiliki sehemu hiyo ya shamba moja kwa moja.
Hakika, urafiki na mikopo ni mtihani mzito sana.