Kumdai mfiwa niianze lini?

Kumdai mfiwa niianze lini?

Samahani

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
237
Reaction score
355
Ndugu zangu, walau naombeni msaada walau wa mawazo. Nina rafiki yangu ambaye kwakweli tunaishi kwa misingi yote ya kidugu.

Kwa bahati mbaya, alipata Msiba wa MAMA YAKE miezi tisa iliyopita, na katika kuwezesha suala la msiba, aliomba nimkopeshe kiasi fulani Cha Pesa.

Kwa kuijali misingi ya undugu, Kuna pesa nilimpa Kama mchango wangu kwa ajili ya msiba, na kiasi kingine NILIMKOPESHA KAMA ALIVYOOMBA.

Sasa ni miezi TISA, na kwa bahati mbaya, hapa Katikati nami nilipata msiba wa Mlezi wangu lakini sikupata msaada wowote kutoka kwake. Mara mbili nimeshamkumbusha juu ya Pesa hiyo lakini Mara zote anajibu kuwa, BADO HAJAKAA SAWA KUTOKANA NA MSIBA.

Tafadhali kibinadamu kabisa, walau naweza kufanya Nini juu ya Hili.

Mbarikiwe Sana.
 
Aisee ule muda umefiwa na wewe ingekuwa muda sahihi kumkumbusha fadhila zako na wewe maana ni wakati mgumu sana! Pole sana inahitaji hekima katika hili...
 
Aisee ule muda umefiwa na wewe ingekuwa muda sahihi kumkumbusha fadhila zako na wewe maana ni wakati mgumu sana! Pole sana inahitaji hekima katika hili...
Hakika nilijaribi kwa kiasi chake, lakini kwa kuwa sikitaka nimwoneshe kuwa "NADAI CHANGU", alipoonesha ushirikiano hafifu ilinilazimu kumpa muda.. Sasa tunakwenda mwaka na sioni hata dalili za kukumbukwa, na walau mtu huyu ni mwajiriwa!!!
 
Aisee kama ana source ya income mwambie tu hali halisi coz ulimpa hela ya pole na hiyo nyingne aliomba Umkopeee so usimuones haya mwambie uone atakujibu nini!
 
Aisee kama ana source ya income mwambie tu hali halisi coz ulimpa hela ya pole na hiyo nyingne aliomba Umkopeee so usimuones haya mwambie uone atakujibu nini!
Sawasawa ndugu yangu.. Nitatafuta muda nimkalishe. Mara ya mwisho nilipomkumbusha alijibu "BADO SIJAKAA SAWA BAADA YA MSIBA", lakini hapo ilikuwa Miezi SABA toka apate msiba, na Mimi ndio nilikuwa na msiba mbichi kabisa
 
Ila jibu lake kuwa "BADO HAJAMALIZA MSIBA" linaniwazisha Sana... MIEZI TISA?????
 
Una ushahidi wowote kwamba ulimpatia pesa na akurudishie baada ya msiba?
 
Honestly una ukuu ndani yako, Naweza kukuelewa kupitia thread na comments zako hapa. Hebu jaribu kumweleza jambo hilo ili atambue kama unakelekwa nalo na uwe muwazi kwake kama unahitaji pesa yako. Acha kunung'unika pembeni while uwezo wa kumweleza unao.

Na kama hatojali basi samehe kabsa na uendekee ma maisha mengine.
 
Hakika nilijaribi kwa kiasi chake, lakini kwa kuwa sikitaka nimwoneshe kuwa "NADAI CHANGU", alipoonesha ushirikiano hafifu ilinilazimu kumpa muda.. Sasa tunakwenda mwaka na sioni hata dalili za kukumbukwa, na walau mtu huyu ni mwajiriwa!!!
HALIPI HUYO KAMA UNAWEZA MSAMEHE MKUU
 
Doh!!! Hili pia nalibeba mkuu maana mwisho wa siku akiweka ngumu kuridisha Wala sitakuwa na msaada popote zaidi ya KUSAMEHE TU!!!!
japo huwa inauma kusamehe lakini ni njia sahihi nakumbuka kuna mama mchungaji kutokana na imani kwake kuna mradi tulifanya pamoja alikula peke yake nikamdai sana lakini alijitetea kafanya yote baada ya kufiwa nikaachana nae na kusamehe million moja
 
Ungetoa tu rambirambi bila kutoa mkopo mkuu.Siku nyingine jifunze!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom