Mtukutu wa Nyaigela
JF-Expert Member
- Sep 4, 2018
- 6,545
- 11,095
kama una mpango wa kwenda mbinguni ,Usichukie sabato maana hata mbinguni itakuwepo
kwa wale wanaopenda agano jipya: na kama wewe ni mtu wa Mungu
Hatutunzi sabato ili kuokolewa. tunatunza sabato kwa sababu tumeokolewa.
niwatakie sabato njema watu wa Mungu
Isa 66:23 SUV
Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA.kwa wale wanaopenda agano jipya: na kama wewe ni mtu wa Mungu
Waebrania 4:9-10
Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake.Kut 20:8-11 SUV
Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.Hatutunzi sabato ili kuokolewa. tunatunza sabato kwa sababu tumeokolewa.
Efe 2:8-10 SUV
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.niwatakie sabato njema watu wa Mungu