Chibike
JF-Expert Member
- Aug 16, 2024
- 4,897
- 7,525
Irene,
... jina lako bado linatoa furaha moyoni mwangu, kama upepo wa bahari, kwenye majira ya joto, upepo ulionitunza kwa huruma. Sikiliza, leo hii napenda kukumbuka wewe kwa maneno haya, kwa kuwa wakati haukuruhusu kuwa wangu, moyo wangu kamwe haukusahau.
Nilikupenda kwa uaminifu mkubwa, kwa ule mtindo wa mapenzi yasiyotamani kitu bali urithi wa furaha. Uliniambia "hapana," lakini sikukataa nilikubali kwa heshima, nikajifunza kuwa pendo langu halikuwa mzigo wala halikua na hatia. Leo, pengine naamini kuwa ulifanya chaguo sahihi kwa wakati huo, na najali hata kama tumepoteana kwenye njia za maisha.
Bado nakumbuka kumbukumbu kadhaa za sisi, mpaka leo. Ulikuwa mwanzo wa wimbo mzuri ambao haujakwisha, hata kama sikuona mwisho wake.
Siku Moja, ghafla nakuona kipenzi changu, najisemea yule pale, moyo wangu ukapasuka paaah! Ila hukuniona, nikakosa hata nguvu ya kuja ulipo, nikajibanza mahali , nakuangalia mwanamke niliekupenda tangu enzi , ulipaswa uwe mke wangu, nilikua nakuoa Irene, embu nione, dume la mbegu mwanaume mzima nashindwa kwenda kukusabahi baada ya miaka zaidi ya 15 kutoonana , naangalia uzuri wako, najisemea umekua Mrembo zaidi, 😭 naamua kuondoka, pengine Bado sijawa tayari kuku face...ipo siku najua Mungu ataniambia Sasa fulani uko tayari sasa, nakuja kuchunguza nakuta Bado hujaolewa, nabaki kushangaa, au ndio Kauli zangu za no man will ever love you the way I did ..? Sijui, sio kwa ubaya
Irene, ikiwa siku moja utasikia ama kusoma haya, nakusalimu kwa sauti ya upole ya roho yako. Nashukuru kwa kila kicheko, kila sauti yako iliyoniponya, na hata kwa machozi yale yaliyonifundisha kuwa mapenzi si mara zote ni ya kujibu, bali ya kukua. Umeniweka kwenye ukurasa mahsusi wa maisha yangu, na huo utabaki daima.
Mungu akubariki, mpenzi wa zamani, mwenye busara na uzuri wa moyo.
Wako, .......c