Hakuna mbingu ya wachochezi.....endelea kuota
View attachment 2097849
Ushindi...
Hiki kibonzo ulichoweka ni propaganda tupu hakiakisi ukweli na hali halisi ya Tanganyika ambako dini kuu mbili ni Uislam na Ukristo.
Haya hayakupata kutokea katika historia ya Tanganyika kuwa wafuasi wa dini hizi mbili wamepambana ukiweka matukio machachae miaka hii ya karibuni ambayo laiti yangeshughulikiwa kwa haki pasingekuwa na matatizo yaliyotokea.
Ukitoa matukio machache wakati wa Vita Vya Maji Maji ambapo wamishionari waliuawa na vutuo vyao kushambuliwa kabla ya vita na Wajerumani hapakuwa na matatizo ya iana hiyo.
Unaweza kujiuliza kwa nini askari wa Maji Maji washambulie vituo vya wamishionari na kuwaua wamishionari.m
Haya yalitendeka kwa kuwa wapiganaji wengi wa Maji Maji walikuwa Waislam na zile dhulma za wakoloni wa Kijerumani waliona wamishionari ni sehemu ya utawala dhalim kwa hiyo na wao ni maadui.
Tatizo kubwa ni kuwa waliokuwa na elimu na kushika madaraka nchini petu si Waislam na hii imeathiri hata usomeshaji na utafiti wa historia ya kweli ya Tanganyika.
Ndiyo unakuta majina ya Kiislam katika historia yanakwepwa kwa makusudi.
Mara kadhaa hapa nimeeleza kuwa Songea Mbano jemadai wa Maji Maji jina lake ni Abdulraufu na Nkomanile mwanamke pekee jemadari jina lake ni Khadija.
Hawa wote ni mashujaa wa Maji Maji na walinyongwa na Wajerumani.
Uislam hapa Tanganyika umesaidia sana katika kujenga udugu kati ya wafuasi wa dini hizi mbili.
Nani walimtia Julius Nyerere katika uongozi wa TAA na baadae TANU?
Wazalendo hawa ni Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Ali Mwinyi Tambwe.
Historia hii ipo isomeni.
Huyu Ali Mwinyi Tambwe alikuwa Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika iliyoundwa na baba yake Abdul Sykes, Kleist Sykes 1933 kutokana na uongozi ule ule uliounda African Association.
Nani aliyemuunga mkono na kumtia nguvu Mwalimu wakati anachukua uongozi wa TAA kisha TANU?
Mufti Sheikh Hassan bin Ameir ambae yeye mwenyewe alikuwa ndani ya TAA Political Subcommittee toka 1950 na Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.
Nyerere alikuwa kazungukwa na watu gani wakati wa kupigania uhuru?
Waislam.
Nyerere kasomewa dua na Waislam mjini Dar es Salaam nyumbani kwa Jumbe Tambaza Upanga, Lindi nyumbani kwa Masudi Mnonji dua ikiongozwa na Sheikh Yusuf Badi.
Katika dua hii alikuwa Bi. Sharifa bint Mzee mwanamke shujaa katika akina mama waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Nyerere alifanyiwa dua kijiji cha Mnyanjani Tanga na waliohudhuria walikuwa Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Dhikr bin Said, Mzee Zonga, Hemed Anzwan, Salehe Kibwana, Akida Boramimi bin Dai, Mmaka Omari na Sheikh Ali Kombora.
Lakini kwa kuwa hii historia ilifunikwa haijulikani matokeo yake ndiyo huu uadui ambao hata hapa barzani unajitokeza waziwazi.
Laiti watu wangejua tulikotoka historia hii ingezidisha mapenzi na mchango wa Waislam na Uislam kwake Julius Nyerere mwenyewe na kwa nchi hii ungeheshimiwa.
Leo inasikitisha kuwa walio madarakani hawataki kusikia lolote kuhusu Waislam na Uislam.
Matokeo yake ndiyo haya mnaweka vibonzo vya propaganda kuwatisha watu pasi na sababu.
Sisi dua yetu siku zote ni kuwa Allah adumishe amani na viongozi wetu watoe haki sawa kwa waumini wa dini hizi kuepusha vurugu kwa sababu dhulma ikiachiwa kuenea huangamiza.
Mifano iko mingi duniani.