Kumbukumbu ya kesi ya Sheikh Ponda 2015

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,787
30,080
KUMBUKUMBU YA KESI YA SHEIKH PONDA MOROGORO 2015

''Allah ni Mjuzi Allah na ni Mbora wa kulipa.

Sheikh Ponda utayakuta malipo yako kwa Allah yakiwa makubwa kwa subra na ustahamilivu kwa ajili ya dini yake.

Hukuwa tayari kuuza uhuru wako kwa matakwa ya wenye kudhulumu.

Muda wote ulitutia moyo mawakili wako kila tulipokutana na vitimbi.

Mara nyingi sisi mawakili tulikuwa kama wateja na wewe ndiye wakili.

Hakika wewe ni kiongozi.

Umma huu wa Waislam wa Tanzania utaishi kwa mfano wako.

Alhamdulilah leo uko huru baada ya miaka miwili na miezi mitatu jela ukiwa na jeraha kubwa la risasi.

Allah anayo siri kubwa katika maisha yako Sheikh Ponda.

Allah akuhifadhi kiongozi wetu.

Amin.''

Wakili Juma Nassoro

Screenshot_20220120-235820_Facebook.jpg
 
hivi ndio alipelekewa kitu chenye ncha kali kikamkosa kikaingia kwa mtu aliyekuwa pembeni...!

huyu mzee hana itikadi za ki ccm vp wewe mzee said?
 
aache ukorofi, anamkosea Allah.
Laki...
Naamini umetoa kauli hiyo kuhusu Sheikh Ponda kwa kukosa kwanza kuwa na ujuzi wa kuchagua maneno ya staha yanayostahili kutamkwa hadharani kwa kiongozi wa dini

Pili ni kwa kukosa kutambua hadhi na heshima aliyonayo Sheikh Ponda katika umma wa Waislam wa Tanzania.

Hukustahili kumwita Sheikh Ponda 'mkorofi," kwani si katika sifa zake.

Hupenda unadhani kwa kuwa ni kiongozi wa Waislam unaweza ukamvunjia heshima.

Sheikh Ponda ni kiongozi mkubwa sana wa Waislam kwa kuchaguliwa na wenyewe Waislam na ndiyo maana ana heshima hii aliyonayo.

Fanya staha unapowazungumza viongozi wa dini.

Sijaelewa hapo ulipomtaja Allah na kusema Mwenyezi Mungu kakosewa na Sheikh Ponda.

Kushoto ni Sheikh Ponda, Ado Shaibmmoja wa viongozi wa ACT Wazalendo na Hamza Kassongo katika Kongamano la Maalim Seif Zanzibar.View attachment 2090384
 
namuheshimu sana shehe Ponda, anachokosea ni kuchanganya dini na siasa......halafu kiongozi mkubwa wa waislamu tunaemtambua ni mufti, huyu Ponda hatambuliki popote
 
namuheshimu sana shehe Ponda, anachokosea ni kuchanganya dini na siasa......halafu kiongozi mkubwa wa waislamu tunaemtambua ni mufti, huyu Ponda hatambuliki popote
Laki...
Kuchanganya dini na siasa wewe unaona anakosea lakini yeye si wa kwanza kufanya hilo.

Uislam kama dini umetumika sana wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika na nimeandika kitabu kuhusu historia hii.

Halikadhalika dini imetumika sana kupambana na Uislam baada ya uhuru kupatikana na historia hii imeandikwa na Bergen (1981), Sivalon (1992).

Sasa kipi cha ajabu?

Sawa Mufti ni kiongozi kutoka BAKWATA na serikali ndiyo iliyounda BAKWATA mwaka wa 1968 na ndiyo kiongozi wanaemtambua.

Hakuna ugomvi.

Waislam kwa upande wao wameunda taasisi zao wenyewe na wanawatambua viongozi wao Sheikh Ponda akiwa mmoja wa viongozi hao.

Hakuna ugomvi.

Sheikh Ponda anatambulika kama kiongozi wa Shura ya Maimamu chini ya Taasisi na Jumuiya za Kiislam (Baraza Kuu) na imesajiliwa serikalini.

Hakuna ugomvi.

Hatuhitaji yeyote atambue viongozi wetu ndiyo Waislam wamkubali kwani viongozi wa Waislam wako masuul kwa Allah si kwa nguvu yeyote ya kidunia.
 
KUMBUKUMBU YA KESI YA SHEIKH PONDA MOROGORO 2015

''Allah ni Mjuzi Allah na ni Mbora wa kulipa.

Sheikh Ponda utayakuta malipo yako kwa Allah yakiwa makubwa kwa subra na ustahamilivu kwa ajili ya dini yake.

Hukuwa tayari kuuza uhuru wako kwa matakwa ya wenye kudhulumu.

Muda wote ulitutia moyo mawakili wako kila tulipokutana na vitimbi.

Mara nyingi sisi mawakili tulikuwa kama wateja na wewe ndiye wakili.

Hakika wewe ni kiongozi.

Umma huu wa Waislam wa Tanzania utaishi kwa mfano wako.

Alhamdulilah leo uko huru baada ya miaka miwili na miezi mitatu jela ukiwa na jeraha kubwa la risasi.

Allah anayo siri kubwa katika maisha yako Sheikh Ponda.

Allah akuhifadhi kiongozi wetu.

Amin.''

Wakili Juma Nassoro

View attachment 2089970

Mambo yanaenda kasi sana. Shekhe kimya sana siku hizi 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Mkuu,. Ponda alishiriki sana kampeni za mwaka 2010 upande wa Ccm ila kuanzia mwaka 2012 alijikuta kwenye misukosuko na polisi na hata kwenye malumbano na Bakwata ,tatizo lilikuwa nini hasa ?
 
Mkuu,. Ponda alishiriki sana kampeni za mwaka 2010 upande wa Ccm ila kuanzia mwaka 2012 alijikuta kwenye misukosuko na polisi na hata kwenye malumbano na Bakwata ,tatizo lilikuwa nini hasa ?
Proved,
Nitageuza kidogo na sijui kama utanielewa.
Ikiwa imetokea hukunielewa sema.

Sheikh Ponda hakuwa upande wa CCM.
Sheikh Ponda alikuwa anamsaidia Kikwete.
 
Proved,
Nitageuza kidogo na sijui kama utanielewa.
Ikiwa imetokea hukunielewa sema.

Sheikh Ponda hakuwa upande wa CCM.
Sheikh Ponda alikuwa anamsaidia Kikwete.
Huko kumsaidia mgombea wa Ccm kumshinda mgombea wa upinzani wa wakati huo si sawa na kuisaidia tu Ccm?.....mbona walikuja kuingia kwenye mvutano nae ?
 
Huko kumsaidia mgombea wa Ccm kumshinda mgombea wa upinzani wa wakati huo si sawa na kuisaidia tu Ccm?.....mbona walikuja kuingia kwenye mvutano nae ?
Muhitimu,
Hukijui kisa hiki.

Ponda anafanya haya hata CCM hawajuwi kuwa sheikh anapita kijiji kwa kijiji kwa pikipiki na baiskeli akilala misikitini pale alipokosa mwenyeji wa kumkaribisha kwake.

Katikati ya kampeni nimekuja likizo Dar-es-Salaam mwezi wa Ramadhani.

Ikatokea tukakutana msikitini.

Namuona Ponda kakonda na mikono yake ina upele ametafuwa na mbu.

Siku hii tukakaa pembeni akanipa kisa chote.

Waliokuwa wanasaidiwa hawakuwa na taarifa yoyote.

Kama wewe una taarifa ya mvutano basi ni ule wetu wa kudumu si kwa kuwa wezi wa fadhila hawana shukurani.

Ponda mtu mwingine sana si mtu wa kawaida unaekutananae kila siku mitaani.

Nikimtembelea Segerea yuko rumande.
Akiniona akifurahi sana.

Mimi naumia roho yeye ananiletea maskhara ya kila aina kunichangamsha.

Jiulize Ponda alikuwa anamsaidia nani?

Mgombea alikuwa anachimbwa na yeye Ponda akitambua sababu yake.

Hapo ndipo lilipo jibu lako.
 
Hakuna mbingu ya wachochezi.....endelea kuotaView attachment 2097849
Ushindi...
Hiki kibonzo ulichoweka ni propaganda tupu hakiakisi ukweli na hali halisi ya Tanganyika ambako dini kuu mbili ni Uislam na Ukristo.

Haya hayakupata kutokea katika historia ya Tanganyika kuwa wafuasi wa dini hizi mbili wamepambana ukiweka matukio machachae miaka hii ya karibuni ambayo laiti yangeshughulikiwa kwa haki pasingekuwa na matatizo yaliyotokea.

Ukitoa matukio machache wakati wa Vita Vya Maji Maji ambapo wamishionari waliuawa na vutuo vyao kushambuliwa kabla ya vita na Wajerumani hapakuwa na matatizo ya iana hiyo.

Unaweza kujiuliza kwa nini askari wa Maji Maji washambulie vituo vya wamishionari na kuwaua wamishionari.m

Haya yalitendeka kwa kuwa wapiganaji wengi wa Maji Maji walikuwa Waislam na zile dhulma za wakoloni wa Kijerumani waliona wamishionari ni sehemu ya utawala dhalim kwa hiyo na wao ni maadui.

Tatizo kubwa ni kuwa waliokuwa na elimu na kushika madaraka nchini petu si Waislam na hii imeathiri hata usomeshaji na utafiti wa historia ya kweli ya Tanganyika.

Ndiyo unakuta majina ya Kiislam katika historia yanakwepwa kwa makusudi.

Mara kadhaa hapa nimeeleza kuwa Songea Mbano jemadai wa Maji Maji jina lake ni Abdulraufu na Nkomanile mwanamke pekee jemadari jina lake ni Khadija.

Hawa wote ni mashujaa wa Maji Maji na walinyongwa na Wajerumani.

Uislam hapa Tanganyika umesaidia sana katika kujenga udugu kati ya wafuasi wa dini hizi mbili.

Nani walimtia Julius Nyerere katika uongozi wa TAA na baadae TANU?
Wazalendo hawa ni Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Ali Mwinyi Tambwe.

Historia hii ipo isomeni.

Huyu Ali Mwinyi Tambwe alikuwa Secretary wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika iliyoundwa na baba yake Abdul Sykes, Kleist Sykes 1933 kutokana na uongozi ule ule uliounda African Association.

Nani aliyemuunga mkono na kumtia nguvu Mwalimu wakati anachukua uongozi wa TAA kisha TANU?

Mufti Sheikh Hassan bin Ameir ambae yeye mwenyewe alikuwa ndani ya TAA Political Subcommittee toka 1950 na Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.

Nyerere alikuwa kazungukwa na watu gani wakati wa kupigania uhuru?
Waislam.

Nyerere kasomewa dua na Waislam mjini Dar es Salaam nyumbani kwa Jumbe Tambaza Upanga, Lindi nyumbani kwa Masudi Mnonji dua ikiongozwa na Sheikh Yusuf Badi.

Katika dua hii alikuwa Bi. Sharifa bint Mzee mwanamke shujaa katika akina mama waliopigania uhuru wa Tanganyika.

Nyerere alifanyiwa dua kijiji cha Mnyanjani Tanga na waliohudhuria walikuwa Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Dhikr bin Said, Mzee Zonga, Hemed Anzwan, Salehe Kibwana, Akida Boramimi bin Dai, Mmaka Omari na Sheikh Ali Kombora.

Lakini kwa kuwa hii historia ilifunikwa haijulikani matokeo yake ndiyo huu uadui ambao hata hapa barzani unajitokeza waziwazi.

Laiti watu wangejua tulikotoka historia hii ingezidisha mapenzi na mchango wa Waislam na Uislam kwake Julius Nyerere mwenyewe na kwa nchi hii ungeheshimiwa.

Leo inasikitisha kuwa walio madarakani hawataki kusikia lolote kuhusu Waislam na Uislam.

Matokeo yake ndiyo haya mnaweka vibonzo vya propaganda kuwatisha watu pasi na sababu.

Sisi dua yetu siku zote ni kuwa Allah adumishe amani na viongozi wetu watoe haki sawa kwa waumini wa dini hizi kuepusha vurugu kwa sababu dhulma ikiachiwa kuenea huangamiza.

Mifano iko mingi duniani.

1643343623531.png
 
Proved,
Nitageuza kidogo na sijui kama utanielewa.
Ikiwa imetokea hukunielewa sema.

Sheikh Ponda hakuwa upande wa CCM.
Sheikh Ponda alikuwa anamsaidia Kikwete.
Namkubali sana Sheikh Ponda, lakini hapa hapawezi kuwa na hoja yoyote ya msingi zaidi ya ndugu katika imaani.

Profesa Lipumba pia alishafanya hili kuokowa jahazi, alikiri kwa kinywa chake kwenye msikiti wa kwa Mtoro au msikiti wa Manyema kama sikosei.
 
Ina maana wote Lipumba na Ponda tukisema walimsaidia Kikwete na sio Ccm haileti maana, kwa kumsaidia huko Kikwete walijikuta wanaisaidia Ccm pia.

Jiulize Ponda alikuwa anamsaidia nani?

Mgombea alikuwa anachimbwa na yeye Ponda akitambua sababu yake.

Hapo ndipo lilipo jibu lako.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom