Intelligent businessman
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 26,772
- 54,044
Andres Iniesta Kondoo fulani katikati ya msitu wa mbwa mwitu wakali
Ile picha ya kibabe sana, aliipiga 'Felipe Mondrovera' wa 'Getty images'. Ilikuwa Juni 10 2012 mechi ya kwanza ya EURO. Hispania waliianza kampeni yao ya kutetea taji la mataifa Ulaya. Kumbuka hapo walitoka kuchukua EURO 2008 pale German na Kombe la Dunia 2010 pale kwa Madiba.
Rekodi ilikuwa inasema, hakuna taifa lililowahi kutetea taji la mataifa Ulaya (EURO). Zaidi ya yote, hakuna taifa lililowahi kuchukua mataji matatu makubwa mfululizo. Hata Brazil ya 1958 haikuweza. Ila Hispania walikuja EURO 2012 wakiamini inawezekana.
Kwanini wasiamini hivo? Walikuwa na kila kitu, walikuwa na kila mtu. Xavi Hernandez, Sergio Busquets, Andres Iniesta, David Silva, Cesc Fabregas, Xabi Alonso. Utawaambia nini watoto wa Vicente Del Bosque? Wanapika tu sambusa uwanjani. Hawaelewi kitu zaidi ya kupiga mpira. Miguu yao ina sumu hatari, kila wanaloamua uwanjani linakubali
Hapo nimekutajia tu viungo, sijaugusa ukuta wa Sergio Ramos, Gerald Pique, Alvaro Arbeloa na Jordi Alba. Utawaambia nini? Enzi hizo wanacheza bila namba tisa. David Villa na Fernando Torres hawakumbukwi kabisa kuwa wapo benchi. Hiyo Hispania, acha kabisa! 🙌.
Najua unajua walibeba lile kombe. Hiyo siyo hoja yangu ya msingi. Hoja yangu ni zile njia alizokuwa anapita Andres Iniesta. Kila mechi aliyokuwepo uwaniani, aliondoka na picha za kutisha. Mara nyingi utamuona katikati ya msitu wa wachezaji wa timu pinzani. Lakini ghafla tu utamuona ameondoka. Atatoa pasi yenye macho, Atapiga chenga au atachezewa rafu. Kitu kimoja tu cha hakika ni kuwa hawezi kupoteza mpira.
Moja ni ile niliyoizungumzia pale mwanzo, mechi dhidi ya Italia. Akiwa katikati ya Christian Maggio, Claudio Marchisio, Thiago Motta, Leonardo Bonucci na Giorgio Chiellini. Alipita kati yao na kuwaacha watu mdomo wazi. Mpaka leo, ile picha inatumika na 'getty' kama cover ya picha zao zote za michezo.
Ila kwa Iniesta picha kama zile zipo nyingi sana. Matukio kama yale ameyafanya sana. Yapo zaidi ya 100. Tukisema tuyajadili leo hatutayamaliza. Pale EURO 2012 aliyapiga zaidi ya 30. Ukipata muda uzitazame. Maestro huyu Andres Lujan Iniesta.