Kumbukizi ya satellite ya kwanza kurushwa duniani tarehe na mwezi kama leo mwaka 1957

Thabit Karim

JF-Expert Member
Sep 3, 2012
364
645
SPUTNIK-1 SATELLITE YA KWANZA DUNIANI

Na Thabit Karim Muqbell

Sputnik-1, Rus: Спутник-1, Eng: Satellite-1.

Mwaka 1957 Historia ya teknolojia ilibadilika na dunia ilisimama pale USSR walipofanikiwa kurusha satellite ya kwanza na ya aina yake katika anga za kati za juu. Sputnik-1 ilikua ni satellite ya majaribio ktk teknolojia ya satellite ulimwenguni lakini lengo kubwa lilikua ni USSR kuionesha USA namna USSR ilivyokua haishikiki ktk mambo kadhaa ya teknolijia duniani.

Mnamo 4/10/1957 Katika kituo cha kurushia Marocket ya masafa marefu Baikonour Cosmodrome, USSR wanasayansi kadhaa akiwemo Mkuu wa kitengo cha Anga na Chief designer wa Makombora ya masafa marefu Sergei Korolev walifanikiwa kurusha Satellite hii na kuishtua dunia. Sputnik-1 ilikua satellite ya mviringo ikiwa na redio moja yenye betri tatu ndani iliyokua ikitoa signal duniani.

Malengo ya Sputnik-1 yalikua ni kuionesha USA na Dunia kwa ujumla namna ambavyo USSR walivyo na uwezo wa Kiteknolojia, Pia kuanza kufanya tafiti juu ya umuhimu wa satellite hasa katika maswala ya upepelezi na mawasiliano. Sputnik 1 ilipokua angani kila mtu katika ardhi ya Dunia alikua na uwezo wa kuiona kwa Telescope na kusikia ikitoa mlio wa 'beep beep' kwa kifaa cha short wave receiver. January 1958 Sputnik-1 iliungua na kuisha kutokana na joto lilikua juu ya uso wa Dunia na kuwa ndio mwisho wa Sputnik-1.

Sputnik-1 ina mchango mkubwa sana katika teknolojia ya satellite ambayo bila teknolojia hii pengine Dunia isingekua hapa ilipo. Bila satellite, kusingekua na Internet, Live coverage, Weathering, Upelelezi, Communications na mengineyo. Hakika Sputnik 1 haitokuja kusahaulika na Wanadamu ulimwenguni kote.

FB_IMG_1601815891590.jpeg
 
duh!! wenzetu wametoka mbali. kipindi hicho nchi nyingi za Afrika bado zina tawaliwa.
 
Mwaka 1982 kijijini kulikua ukiwa mtupu sasahao mwaka 1957 wanafanya mambo hayo....Africa kweli masikini
 
Sputnik 1 (Kirusi Спутник kwa maana msindikizaji) ilikuwa satelaiti ya kwanza iliyotengenezwa na binadamu na kuzunguka Dunia katika anga-nje. Ilitengenezwa katika Umoja wa Kisovieti na kurushwa angani tarehe 4 Oktoba 1957 kutoka kituo cha Baikonur (leo nchini Kazakhstan).

Sputnik 1 ilikuwa na umbo la tufe lenye kipenyo cha sentimita 58 na masi ya kilogramu 83.6. Ilikuwa na antena mbili zenye urefu wa mita 2.4 na 2.9. Ilibeba vifaa vya kupima jotoridi ndani yake pamoja na shinikizo la gesi iliyo mwilini mwake transmita ya redio iliyorusha vipimo hivi kupitia antena.

Sputnik 1 ilizungukua Dunia mara 1,440 katika muda wa miezi 3 hadi kushuka na kuungua katika angahewa ya Dunia tarehe 4 January 1958.

Kurushwa kwa Sputnik 1 kulitokea wakati wa mashindano makali baina ya Umoja wa Kisovieti na Marekani. Marekani ilishtuka kabisa kwa sababu waliwahi kuamini ya kwamba walikuwa mbele. Mshtuko wa Sputnik ulisababisha mabadiliko katika siasa ya Marekani iliyoongeza juhudi zake katika teknolojia na elimu. [1] Hapo yalianza mashindano ya anga (en:Space Race baina ya Marekani na Umoja wa Kisovieti ambapo pande zote ziliendelea kupeleka satelaiti nyingi kwenye anga zilizofuatwa na vyomboanga vya kubeba watu hadi Marekani ilifauli kufikisha watu mwezini mwaka 1969.

Chanzo: Sputnik 1 - Wikipedia, kamusi elezo huru
 
How the mighty have fallen.
USSR a country with an envied industrial prowess.
Modern day Russia is not even close to being a shadow of former-self.
 
How the mighty have fallen.
USSR a country with an envied industrial prowess.
Modern day Russia is not even close to being a shadow of former-self.
Nani alishangaa uwezo wa kitasnia ya Umoja wa Kisovyeti? Tangu 1960 hivi (wakati kiongozi wao alipoahidi kupita Marekani kwenye ubora wa maisha) ilionekana hawawezi. Viwanda vyao na mpangilo wa uchumi vyote nyuma. Watu wa pekee waliowaona kama wakubwa walikuwa hao katika nchi za kilimo sehemu za Asia na Afrika, ambao wakati ule hawakuelewa bado jinsi ya kujenga tasnia ya viwanda. Wasovyieti waliwekeza uwezo wao, pesa na wabingwa na muhandisi bora kwenye tasnia ya silaha pia kwenye mashindano ya anga-nje dhidi ya Marekani na sehemu chache nyingine. Pale waliweza kufikia matokeo mazuri. Kwa jumla walikuwa nyuma kabisa na hii iikuwa sababu ya kuonekana nyuma mara ukomunisti uliokwisha na watu waliweza kutoka nje kusafiri na kuona mambo mengine. Walishindwa kutengeneza bidhaa zilizotafutwa penginepo duniani. Siku hizi wanasogea mbele polepole.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom