Kumbukizi ya miaka 20 ya Moses Nnauye imetegua vitendawili vingi

Kati ya vitu tunavyo weza kuja kuvijutia baadaye ni haya majina tunayo yaandika sana Sukuma gang ,Msoga gang na mengine yanayo fanana na hayo.

Nchi yetu ni ya watanzania wote bila kujari mkoa au Kijiji anacho tokea.
Magufuli ndiye kalihqribu taifa. Mwanzo hatukuwa na huu ujinga Magufuli ndiyo kauleta.

Watu wamebomolewa nyumba zao pale Kimara lkn Mwanza akasema ziaiguswe ni za wapiga kura wake

Dar wamachinga walipata kashkash Mwanza ilipoguswa akawa mkali na kusitisha nchi nzima

Teuzi zote zikawa zinaangalia Kanda ya ziwa

Kwahiyo alaumiwe mwanzilishi wa sukuma gang
 
Sukuma Gang tuna hazina ya potential candidates.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Tatizo lenu ndani ya chama chenu mshazoea kuwauzia Watanzania mbuzi kwenye gunia...
Yaani mnaamini mkimleta kilaza yeyote atachagulika hata kwa mitutu ya bunduki...!!
Hamuandai viongozi bali mnaandaa makundi hasimu ndani ya chama!
Mwisho wa siku nchi inakuwa kama gurudumu inazunguka ikiwa pale pale...!

NB: ccm na magenge yake yote - Sukuma Gang, Msoga, Visiwa, la saba, n.k ni hatari sana kwa maendeleo ya wananchi...
 
Magufuli ndiye kalihqribu taifa. Mwanzo hatukuwa na huu ujinga Magufuli ndiyo kauleta.

Watu wamebomolewa nyumba zao pale Kimara lkn Mwanza akasema ziaiguswe ni za wapiga kura wake

Dar wamachinga walipata kashkash Mwanza ilipoguswa akawa mkali na kusitisha nchi nzima

Teuzi zote zikawa zinaangalia Kanda ya ziwa

Kwahiyo alaumiwe mwanzilishi wa sukuma gang
Viongozi uandaliwa... Kuna madhara makubwa sana kuuziwa jina bila kufanya vetting ya kutosha na ya miaka mingi.
Yaliyotokea kwa Marekani ya Trump ndo kama yale yale yalotokea kwa nchini!
Kuwa na mfalme mwenye madaraka makubwa hasiyekuwa kiongozi!


NB: Nature inapotoa fundisho... Tujifunze!
 
Kati ya vitu tunavyo weza kuja kuvijutia baadaye ni haya majina tunayo yaandika sana Sukuma gang ,Msoga gang na mengine yanayo fanana na hayo.

Systems za binadamu haziko constant... zina kua... zinabadilika... Yote haya hayana budi kutoa kwanza kabla wananchi hawajajua thamani yao!

Nchi yetu ni ya watanzania wote bila kujari mkoa au Kijiji anacho tokea.

Hii conclusion inahitaji elimu kubwa sana kuitambua, kuielewa na kuiishi...
Nionavo mimi, ccm kwa makusudi imefanya mapinduzi kwa kuwapa watu elimu ya ovyo ya kuwafanya kuwa tegemezi!
Wengi wanaamini nchi hii ni ya viongozi na ccm; waamue wajuavyo na watakavyo... ilmradi wao wanaishi, wanakula, wanapigia makofi ya shangwe basi all is well!!
 
Uadui wa Nchimbi na Nape ulianzia wapi mkuu kama hutojari nifumbue macho wengine siasa imetupita pembeni.
Uadui ulianzia ufisadi wa Nchimbi ktk umiliki wa jengo la UVCCM hapo Dar. Nchimbi akiwa ni mwenyekiti wa UVCCM alifisadi mradi wa jengo hilo akishirikiana na Lowasa &co. Nape alikomalia jambo hilo, wakati huo Nchimbi akielekea kumaliza muda wake wa uongozi na akahakikisha kwamba Nape hapati nafasi ya M/kiti wa UVCCM. Kulikuwa na sarakasi za kishenzi tu hadi kuahirisha uchaguzi ili tu baadaye uchaguzi ukifanyika, Umri wa Nape uwe nje ya kanuni. Nape hakuipata nafasi hiyo.
 
Aliyemuombea Kikwete uwaziri kwa Mwinyi ni Wariobya sio Nnauye.
Warioba angemjua wapi Kikwete wakati Kikwete alikuwa wilayani mbali kabisa?
Nnauye alimjua Kikwete tangu jeshini na huko wilayani. Mwinyi aliwaingiza wawili kwa pamoja; Kikwete na Zakia Megji kwa kisinghizio cha damu mpya. Nyuma ya pazia nguvu ya udini ilisaidia sana.
 
Nape ni mtoto wa Prof.Mwandosa
Hebu angalia lisiti hiyo ya watoto wa mzee Nnauye kutoka kipande cha gazeti, miaka 10 baada ya kifo chake. Je, Nape yupo hayupo? Yaani hata ktk kundi la wajukuu hayumo!

nnauye.jpg
 
Sisi Sukuma Gang hatutakubali kabisa lazima turudi ulingoni tena, afe beki afe kipa,ujinga wakati wa kwenda tu,tumeshajua kila kitu walichofanya hawa Msoga Gang.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
Sukuma Gang wameshaondolewa kwenye reli tayari. Imebaki kuangukia kwenye korongo...... Poleni sana. Mlikuja kwa kasi kubwa bila ya kuchukua tahadhari. Mkaendelea kukanyaga mafuta na kusahau breki.
 
ABUU KAUTHAR

Tukio la kawaida la mkusanyiko wa watu kumkumbuka mpendwa wao limenifumbua akili na kuyajua mambo mengi kuhusu siasa za nchi hii na asili ya uhusiano wa karibu wa baadhi ya watu.

Nazungumzia kumbukizi ya miaka 20 tangu kufariki kwa mmoja wa viongozi mahiri wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Brigedia Jenerali Moses Nnauye, ambaye, kama cheo kinavyojieleza, pia aliwahi kuhudumu serikalini, jeshini huku akikumbukwa zaidi kwa kipawa chake cha muziki.

Ukiacha familia ya Nnauye mwenyewe (mjane na watoto), walikuwepo pia Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, na Makatibu wakuu wa CCM wastaafu Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba.

Orodha hii ikanikumbusha tukio lile enzi ya awamu ya tano ziliponaswa sauti zikimsema vibaya marehemu Rais wa Awamu ya Tano, John Pombe Magufuli. Ni wazee hawa, (ukimuondoa Kikwete) ndio waliosikika wakimsema vibaya marehemu. Pia alikuwemo Nape, ambaye katika mazungumzo na Mzee Makamba alisikika akimuita ‘baba’ kwa heshima zote.

Hawa jamaa pamoja na marehemu ambaye walijikusanya kumkumbuka, wametoka mbali na sio ajabu kwamba wanazeeka wakiwa na ukaribu mkubwa, sio wao tu bali hata familia zao! Naamini wapo sahihi watu waliosema kuwa kuna ‘family coalition’ (muungano wa familia) unaosaidiana kuhakikisha wanatawala nchi hii.


Wote watatu niliowataja licha ya kulelewa ndani ya chama, pia walikuwa wanajeshi mahiri, enzi hizo wakati chama kimeshika utamu na hatamu zikiitangulia sio tu serikali bali hata jeshi. Kikwete, hadi anatoka jeshini alikuwa Luteni., Kinana alikuwa Kanali na Makamba alikuwa Luteni huku marehemu waliyekuwa wakimuadhimisha akiwa Brigedia Jenerali. Hii inaelezea hisia za kujiona wanastahili zaidi kukamata uongozi wa nchi wanayoona kuwa wameipigania chamani, jeshini na serikalini.

Ukiangalia historia zao, walianza kwenye chama pamoja,wakahudumua tena pamoja jeshini na kisha serikalini. Nnauye na Makamba walikuwa na mengine ya kuwaunganisha: sanaa. Wote walikuwa waimbaji enzi hizo. Kwa kweli, sikuwa najua kuwa Nnauye alikuwa ndio John Komba wa kwanza!

Hotuba ya Makamba ilifichua siri nyingi, ambapo alielezea ukaribu wake mkubwa na Nnauye kiasi kwamba bosi wake huyo wa zamani alimfia mkononi, akimsaidia kumtamkisha neno muhimu kwa Muislamu kulitamka kabla ya kifo: Laa Ilaaha Illa llah (Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu).

Kinana alisema katika hotuba yake kuwa Nnauye aliacha mafunzo mawili makubwa: Kwanza kiongozi huandaliwa na pilli, mafanikio huja kwa kuwa na ‘organization’ nzuri katika taasisi. Kwangu, kauli hizi ni dongo kwa marehemu JPM ambaye anajulikana kama kiongozi aliyekosa malezi ya chama na ambaye hakuna na weledi katika organization ya chama na badala yake alikuwa mtu wa ‘matamko’.

Wapo watu waliotafsiri kusanyiko lile kuwa sio tu ni maadhimisho ya kumbumbuka Mzee Nnauye bali pia shukrani kwa kundi lile kwa Mwenyezi Mungu wao kwa kuwatoa kifungoni baada ya kuwekewa alama ya X na JPM. Sio siri kuondoka kwa JPM kumewapa ahueni Mzee Makamba na Kinana ya walau kufurahia uhuru na kutoishi kwa wasiwasi tena! Sio siri pia kuwa kuondoka kwa JPM kumefufua matumaini ya kupanda kisiasa kwa wakina Nape, Ridhwani na Januari.


Ninachokiona ni kuwa hizi familia ziko ‘connected’ mno na kuna makubaliano mengi ya kifamilia. Nani alijua kuwa kumbe wakina Nape walikabidhiwa kwa Makamba awalee baada ya kufariki kwa mzee wao? Nani hajui kuwa Kikwete kambeba sana Januari na kumlea kisiasa? Kinana naye akawa karibu na Nape enzi zao chamani akimpa madini ya ‘organization’ ambayo naye alijifunza kwa Mzee Nnauye? Yapi mengine hatuyajui katika mikataba hii ya kifamilia?

Nikiangalia mustakbali wa nchi, nikirejea sauti zile zilizovuja za kumponda JPM hasira zao sitashangaa hawa wababe wakiichukua nchi baada ya Rais Samia kustaafu. Tayari kuna tetesi kuwa Rais Samia anapokea ushauri kutoka Mzee wa Chalinze, ambaye ndiye mzee wa hawa vijana.

Halafu vijana wako vizuri na wamejipanga hasa Januari ambaye anajulikana kama kipenzi cha watu wa mitandaoni hasa Twitter (Twitter darling), ingawa kwa upande mwingine sio siri rekodi yake ya utendaji haivutii, haishtui.


Bila vikwazo vingine njiani, naiona serikali huko mbele ya Rais Januari, Waziri Mkuu Nape huku wakina Ridhwan, Bashe wakipewa majukumu kubwa katika Baraza la Mawaziri.

Tusubiri na tuone

Ngoja tusubiri
 
Magufuli ndiye kalihqribu taifa. Mwanzo hatukuwa na huu ujinga Magufuli ndiyo kauleta.

Watu wamebomolewa nyumba zao pale Kimara lkn Mwanza akasema ziaiguswe ni za wapiga kura wake

Dar wamachinga walipata kashkash Mwanza ilipoguswa akawa mkali na kusitisha nchi nzima

Teuzi zote zikawa zinaangalia Kanda ya ziwa

Kwahiyo alaumiwe mwanzilishi wa sukuma gang
Mi husema ukweli kwa ujinga ndani ya nchi. Kubomolewa kwa Mwanza ilikuwa ni kama ubomoe ubungo Kibangu, ni squatters ambazo watu wa uwanja wa ndege walitaka ziondolewe kwa shida kwamba watu wasipite karibu na uwanja wa ndege. Which was nonsense! Kwani ndege ni nunda mula watu?

Machinga wa Mwanza mtaa maarufu uitwao Makoroboi ni jambo la kulielewa vizuri sana. Mtaa unaitwa makoroboi kwa sababu tangu miaka ya 60 ni mtaa wa machinga watengeneza makoroboi. Baadaye wahindi wakafungua msikiti, geti likitokea mtaa huo. Kwa ubaguzi wa wahindi wasiotaka hata mswahili aswali msikitini kwao, wakaona kama weusi hawa wanaharibu sura ya msikiti. wakaanza kuhonga maafisa wa jiji ili waondolewe. Je, hiyo inafaa kwa Afrika?

Kuhusu Kimara, hapo ni uzembe tu! Hakuna aliyeonewa. imesemwa mara nyingi kwamba Morogoro road tangu enzi ya mkoloni ina sheria yake, ikitambulika kama barabara kuu ya kutoka Dar. Sheria haijawahi badilika miaka yote. Kwa uzembe wetu tukaivamia tangu ubungo mataa ya zamani kulikuwa na bucha za nyama kibao hata transformer zikiwa ndani ya nyumba za watu. Kimara hadi vent za bomba kuu la maji zilikuwa nyumbani kwa watu. watu walijenga hadi juu ya bomba. Nani wa kulaumiwa? Tusipende kudeka deka!
 
Gujiwe la watu lilikuwa linajiendea tu!! km jongoo! halioni mbele!...lilikuwa na akili fupi sana! Dunia ina wenyewe hii! ukiji make! make! wana kume kisha Dunia bana kamwe usikurupukege! utaumia sana!! hata ufanyeyje! ndo ilivo! .......

ni km Mbinguni tu! kule bana tukifika usijitie kihere here!! cha kumjua saaana Mungu, km kile eee cha yaliyo mkuta Shetani! ..huyu jamaa mpaka leomitaa ya mbinguni ameisahau! na hatakiwi huko! shetani alijifanya kumjua Mungu sana! akaingiza na utani bila kujua!!!

yaliyo mkuta Jiwe kila mtu najua.......jiwe bana ni km alikuwa na tabia za Babab yake shetani kabisaaa!! kiburi kilimfanya ashindwe kujus namna ya uongozi!
 
Back
Top Bottom