PostGE2025 Kumbukizi - PM Mstaafu Majaliwa: Madaraka hayalazimishwi, ukilazimisha hautadumu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,268
Reaction score
13,895

===
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alisema Tanzania iko mikononi mwa Mungu na ndiyo maana imeendelea kuwa nchi yenye amani na utulivu na kimbilio la mataifa yaliyopoteza tumaini.

“Nchi hii imeshikwa na Mwenyezi Mungu na ni kwa sababu viongozi wa dini wanaendelea kuliombea Taifa hili, kwa hiyo na sisi tunalo jukumu la kuhakikisha kwamba nchi hii inabaki kwa salama,” amesema.

Alitoa kauli hiyo (Ijumaa, Desemba 31, 2021) wakati akizungumza na waumini baada ya kushiriki ibada ya Ijumaa na kuzindua msikiti wa Nkowe, ulioko kata ya Nkowe, wilayani Ruangwa, mkoani Lindi.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu alisema madaraka yote yanatoka kwa Mwenyezi Mungu na yeye ndiye hupanga nani awe nani na kwa wakati gani. “Tuache tabia ya kuwafanya viongozi washindwe kufanya kazi zao kwa kuwatengenezea migogoro ya kila siku, tena mengine ya kusingizia tu.”
 
1765300624989.jpeg
 
View attachment 3513583

Ya lini hii?
 
Yaan wakitaja mambo ya Dini nachukia na dini kabisa
 
Back
Top Bottom