Kumbuka kuujali Muonekano wako uongeze kujiamini

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Jan 23, 2023
382
661
Muonekano wako ndo kila kitu. Ndio unaamua watu wengine tukuchukuliaje. Ndio unaamua watu wakuheshimu haraka au la. Muonekano wa nje upo juu yako kabisa. Unaweza kuubadili muda wowote na ukaufanyia kazi. Wala usisingizie kitu. Unaweza kujiweka utakavyo. Hivyo usipuuze hilo ukabaki kujisemea 'sina mvuto'. Hapana. Jitahidi upendeze na ujiweke msafi. Usipuuze muonekano wako kamwe.

Usipendeze ili umpate mwanamke fulani. Au ili fulani akuone. Hapana. Bali kwa ajili ya furaha yako mwenyewe.
Japo ni sawa kujiweka vizuri ili wengine wakuone (sote tunataka kuonwa) lakini sio ndo iwe kipaumbele chako sana, mpaka ukajibadilisha na kuwa usivyotaka.

Pia mwonekano wako unaamua utakaye mvutia. Sio wanaume wala wanawake. Wote. Ukiwa na mwonekano wa kitapeli. Utavutia matapeli na wanaotapeliwa. Ukiwa na mwonekano wa kiofisi. Utavutia mabosi na wafanyakazi aina hiyo.

Hata kama ni kwa sehemu ndogo usipuuze. Usije ukasema 'ah naenda hapo tu, haina haja'. Ujue umepunguza maksi zako mbele ya macho ya watu. Pendeza na Ufurahie Siku yako.

Siku Njema.
 
uzi wako ni batili
pesa ndiyo inayoleta kujiamini
pesa ndiyo kila kitu
mwonekano achia peahens
Ingekuwa muonekano ni issue wazungu wangezaraulika na Wacongo wasingeshikika.

Anyway tukubaliane tu umaridadi unaficha umaskini.

Kwahiyo ni muhimu sana kama umepigika jitahidi kujificha aibu yako kwenye pamba, mademu wanaweza kusema wewe ni bahiri kumbe mfukoni hauna kitu.
 
Uhangaikie muonekano na hela hauna ni sawa na gari bila mafuta! Ukiwa na hela mwili utaonekana wenyewe mkuu ujue ukiwa na hela hata vinywele vya kenywe mwili kunanamna vinakaa vizurivizuri hata usipovichana! Ukiwa huna hela Sasa vinasimama kama msumari ukimkumbatia mtu vimchome vimuue upelekwe jela ilimradi vimekuletea tabu tupu..!😂
 
Ahahaah shida ya JF comments za watu wa mwanzo ndio zinabadiri muelekeo wacomments zingine zote naona PESA PESA kila mtu, pesa sio kila kitu mazee , personally nikiuramba safi, nimenyoa kiaskari, pafyumu kwa mbali, nimekata kucha huwa kunanipa kujiamini hata kama Sina milungula.

Ukisema pesa pesa pesa kila sehemu, hebu chukulia uko kwenye presentation tu afu ukatokea umewaka hapo pesa zinakupaje kujiamini mbele za watu kama sio unadhifu wako.

Anyway tutafute pesa tunawiri ili nguo zitukae freshi
 
Ingekuwa muonekano ni issue wazungu wangezaraulika na Wacongo wasingeshikika.

Anyway tukubaliane tu umaridadi unaficha umaskini.

Kwahiyo ni muhimu sana kama umepigika jitahidi kujificha aibu yako kwenye pamba, mademu wanaweza kusema wewe ni bahiri kumbe mfukoni hauna kitu.
oh Gaddaf i06 ni bahili kumbe suti ni mkwala tu wallet ina vitambulisho!
 
download (4).jpeg
 
Back
Top Bottom