Kumblock ex wako kwenye mitandao, ni wazi kuwa hujakubali matokeo

Nyoka_mzee

JF-Expert Member
Nov 26, 2016
3,695
5,520
Imekuwa ni kawaida yetu wengi tunapoachana katika mazingira ambayo hatuko radhi kuachwa au kuacha huwa tunaamua maamuzi ambayo mimi binafsi nayaita si sahihi na sababu zangu nitaziweka hapa.

Wengi wamefeli katika hili. Hawakuweza kufanikiwa kusimama katika misimamo yao ya mwanzo walioiamini kama ni sahihi. Wengi wamejikuta wakiwa unblock ma-ex wao baada kipindi flani kupita.

Swali: Kwanini ublock mtu ambaye unajua wazi fika humuitaji na wala huna haja naye tena?.

Hii inaashiria wengi wanaowablock ma-ex wao ni kwamba bado wanawahitaji na hawawezi vumilia kuwaona wakiwa Huru na watu wengi na ndio maana huchukua maamuzi haya ili wasiumie..

Lakini kwa utafiti usio rasmi, wengi wanaofanya haya baada ya muda flani huishia kuwa unblock tu na maisha yakaendelea...

Wengi huwa bado hawako Radhi Kuwacha ma-ex wao waende, ndio maana huwawia vigumu kukubali matokeo kwamba mambo yamefika mwisho. Na ndio maana pia kwa hasira huamua kuwablock na zinapoisha hasira zao ndio mwanzo wa hasara zao....
 
Kila mtu ana mbinu yake ya kuhandle situation aliyonayo . .kama mtu anaona akiblock X wake ndio anafeel better sio mbaya kwasababu ndio njia yake ya kujisahaulisha nae

Ni kama vile tunavyoshauriwa kufuta namba,kutupa zawadi zao nk hayo ni mambo tu yanayowafanya wasahau haraka basi mi naona ni ruksa tu

Binafsi sijaona ubaya wa kublock mtu unayetaka kumsahau(kama inamsaidia kumove on)
 
mie wangu nilitoka na zawadi alizoninunulia kuzichoma nikazichome kufika nje nikapiga kiberiti kuziweka nikashindwa nikarudisha tu kabatini now naona kawaida sana. nkamblock then nikamuunblock sasa hvi tunawasiliana salam asbh mchna na jioni ila hatuongelei mapenzi yetu. namuona wa mawaida sana.KESHANITOKA MOYONI
 
Kwangu mimi naona blocking is for weak sitakublock wala ila kutakua na no calls & no texts show ile game ya ignoring each other ndo itabeba nafasi
Haina haja ya ku block, pia inasaidia mnoo kumuona wa kawaida. Sijui kutupa zawadi looh situpi kama kiatu nakivaa hadi kichakae
 
nimesoma hii thread nikajikuta nimekasirika ghafla imenikumbusha mengi asee. sipendi kuwa chanzo au sababu ya kubreak, tukibreak basi tusijuane tena maisha yangu yoote
 
Dhambi ya kufanya mapenzi kabla ya ndoa hiyo, ukiwa kama sisi wengine tunaosubiri mpaka siku ya ndoa huna haya matatizo, tunawekeza muda wetu kwenye mambo mengine na wala hakuna stress najua kitu changu kipo mahali kinanisubiri, baada ya ndoa tuanze kudinyana kihalali!!
 
Nina ku block, nafuta picha zako, napunguza mawasiliano na rafiki zako, kama nina kumbukumbu yako kwangu natupa, nachoma au nagawa kwingine.
Yaan naweka full sanctions kama za USA kwa Urusi.
Na sijioni weak kabsa, sasa kama tumeachana tuachane kweli.
 
Mkisha anachana,ya kale yamepita tazama yamekua mapya,ili uanze maisha mapya ya kuachana kitu cha kwanza ni kufanya juu chini kupoteza memories
 
Mtu unamblock kwa kuwa anakuwa kero mmeachana mara anatuma text za kutukana, mara anakutafuta usiku ukimkataza hasikii, ukibadilisha profile anaanza vi sms vya ajabu. Mara nimekumis mara wewe malaya tu from nowhere unablock mjinga kama huyo.
 
Back
Top Bottom