1. Ina katiba yake ila Tanganyika haina katiba tunatumia ya jamuhuri ambayo hailindi maslahi ya watanganyika.
2. Ina Bendera yake sisi ya Tanganyika tumeweka kabatini.
3. Rais na makamo wake, sisi hatuna raisi wala serikali ya tanganyika wala mawaziri wala wabunge.
4. Wana mamlaka zao kamili kama mamlaka ya mapato ZRA sisi tanganyika ukitoa TLS hakuna kitu tunamiliki.
5. Wanazo ofisi za BOT sisi tanganyika hatuna.
6. Wana vitambulisha vya taifa la zanzibar sisi tanganyika hatuna vitambulisho vya taifa letu.
ila wanataka kutumia mapato na rasilimali za tanganyika kwaajiri ya maendeleo yao binafsi katika kivuli cha jamuhuri ya muungano. Huu upuuzi tuukatae kuanzia sasa. Kama kusomesha wazanzibar kwa gharama za kodi za huku.
Kodi tunazolipa huku wakati wa kuingiza vitu kama magari na mizigo kule hawana hicho kitu, gharama zao kule ni nusu ya za huku. wewe una nunua IST milioni 17 nenda kaulize Zanzibar ni bei gani. Umeme kaulize ni kiasi ganiwanalipia? Kaulizie bundles za internet wanalipia kiasi gani kule?
Tudai tanganyika yetu, ipate katiba yake na bendera yake ipepee upya na tuanze na maisha yetu mapya bila CCM.
hii video ni dedication kwa watanganyika wenzangu wote. Simba kaamka anataka territory yake.