sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Pamoja na utawala wa mwendazake kutamatika, bado mbinu chafu zinazoongeza hofu dhidi ya wnanchi na mali zao zinaendelea kwa kasi.
Takribani wiki moja sasa imepita,siku ya Ijumaa iliyopita watu wasiojulikana wakiwa na gari nyeusi tinted, walimteka kijana mmoja mwendesha Toyo, maeneo ya kwa Mathias Kibaha na kumtupia kwenye buti ya gari na kuondoka naye. Kijana huyo kwa jina anaitwa Shahibu Saidi, mkazi wa mtaa wa Bungo, mwenye imani ya dini ya kiislamu dhehebu la Sunni.
Ndugu wa mhanga huyo wamejaribu kufuatilia vituo vyote vya polisi Kibaha bila mafanikio kwa kuambiwa kuwa,Jeshi la Polisi Wilayani Kibaha halina taarifa hizo. Hili ni tukio la kumi ndani ya wiki mbili sasa,likiwalenga vijana hao wa Kisunni.
Matokeo kama haya yanaongeza hofu kwa wananchi na familia zao, lakini yamezua taharuki kubwa kwanini walengwa wanekuwa ni vijana wenye imani ya kiislamu dhehebu la Sunni tu.
Nachukua fursa hii kuhisihi serikali ya JMT kulitazama kwa umakini mkubwa jambo hili,kwani licha ya kuongeza hofu kwa wananchi linaongeza chuki ya wananchi dhidi ya serikali yao. Pia niwakumbushe kuwa madaraka na mamlaka ya serikali yatatoka kwa wananchi na msingi mkuu wa serikali ni ustawi kwa wananchi wake,kama nchi haikaliki ni mbadala wa kuwahakikishia amani wananchi.
#bringbackShahibunawenzake
#peaceandharmony