Kumbe wanaume nao huingia katika Hedhi!

Kumbe wanaume nao huingia katika Hedhi!

TB nafikiri ni malaria tuu ilisumbua na hakuna uhusiano wowote na hiyo kitu
Hiyo kitu kwa wanaume hakuna bana

mkuu mi naunga mkono hoja... najitahidi kukumbuka lakini kwangukatina nature ya kawaida haijawahi kunitokea au huenda labda tunatofautiana
 
Leo sisemi ngoja nijifiche hapa nione jinsi watu wanavyo na kupandisha hasira.
 
We hedhi huijui. Hakuna damu hakuna hedhi. Hii mivurugiko ya kitabia na kiakili huwezi kuiita hedhi. Tafuta lugha muafaka na siyo kuunda vitu ingawa si wewe bali hao watafiti.
 
Huo utafiti inawezekana ulifanywa na watu ambao "tunawaita tech boyz" hawa hawakusoma Biology na kama hawajahangaika kwa bidii zao kujifunzi mambo yanawasumbua.
Khali ya mwili kubadilika badilika ni kitu cha kwaida kwa mwili.
Damu ya hedhi inatokana na yai linalokuwepo ili lirutubishe na sperm ili kuanza hatua za mwanzo za kutengeneza mto
to(Zygote).Inapotokea hakuna sperm za kuliutilizi linapasuka na kutoa hizo damu,sasa ukisema wanaume wanaingia hedhi inakuwa ngumu kueleweka.
Kuhusu mwanamume kuwa tayari kumpa mimba mwanamke hii ni at any time "t" anaweza kama sperm zake zinauwezo huo isipokuwa mwanamke kupata mimba ni lazima awe katika kipindi hicho(ovulation period).
Jifunze kutoka kwa wanyama,wanyama dume say ng'ombe hawayapandi majike ovyo mpaka yawe kwenye muda ambao yanaweza kupata mimba.Sisi wanadamu kwa sababu tunapenda sana starehe tukaona si vibaya hata muda ambao si wa ovulation tuendelee na kazi until further notice.
Hedhi si kukasirika au kubadilika kwa tabia ya mtu,jiulize mwanamke mjamzito haiingii hedhi na wengi wakiwa wajawazito tabia zao hubadilika.So inawezekana wakawa ktk hedhi?Huo utafiti unaweza ukawa right but wrong.
Pia biology iliyomuumba mwanamke si sawa na iliyomuumba mwanaume kuna tofauti kubwa e.g,ukichukua mwanamke na mwanamume ukawanyima chakula kwa say 6days mwanamume atawahi kusign out.Mwanamume na mwanamke kwa mfano wakipata maambukizi ya HIV siku moja vitu vingine viback constant no ARV ,mwanaume atawahi kufa so biology haiko sawa.Wanawake wanauwezo mkubwa wa kuvumilia stress kuliko wanaume.Hiyo report inawezekana "tech boyz" wameiandaa.
 
Kweli nahisi mtoa mada anaumwa,hiyo ya wapi hiyo..mnasoma history tu.. mtatuambia mwanaume anaweza beba mimba! Badilika
 
Mara nyingi nimekua nikiamini kwamba yale tunayoyafahamu kuhusu maisha ni machache sana ukilinganisha na yale tusioyafahamu. Kiasi cha miezi kadhaa iliyopita nilisoma utafiti fulani kuhusu hedhi. Awali nilipousoma niliona ni hadithi tupu. Lakini nilipoona ni vyema kuujaribu kwa kutenda miezi minne baadae nilishangaa. Hata wewe najua utashangaa utakaposoma makala haya. Lakini ombi langu kwako ni kukutaka ujaribu kufanya mazoezi ili uthibitishe ukweli huo.

Miaka ya hivi karibuni imegundulika kwamba hata
wanaume hupata hedhi-ingawa wanaume hawana alama za nje za kuwaonesha kwamba wako kwenye hedhi, kama walivyo wanawake ambao hutoka damu siku zao za hedhi zinapofika na kukamilika.

Kwa karne na karne hakuna mtu aliyekuwa akifikiria kwamba wanaume wangeweza kuwa wanapata nao hedhi kama wanawake. Kama mwanaume akiamua kuweka kumbukumbu zake kwenye dayari na kujiangalia kila siku hali yake inavyobadilikana kuwa ya kusikitika, ya kawaida, furaha na hasira……akiifuatilia hali yake namna hiyo kwa siku zote 28 za mwezi, halafu na mwezi unaofuata, akafanya hivyo hivyo, halafu mwezi wa tatu nao akatenda hivyo, na halafu ailinganishe miezi hiyo mitatu atashangaa.

Kuna siku tatu, nne au tano ambazo zitafanana katika dayari zote tatu, lini ana hasira ana masikitiko, ni mharibifu, na tabia nyingine kama hizo. Hivyo ndivyo vipindi vya hedhi kwa wanaume kama ilivyo kwa wanawake. Zoezi hili anaweza kufanya mwanaume yeyote, akishindwa kupata matokeo anaweza kuwasiliana na mimi na kuuliza ni kwa nini nimeandika uongo.

Ni jambo ambalo lipo na limeshafanyiwa tafiti mbalimbali, hata mimi binafsi nimefanya zoezi hilo kwa miezi minne na limetoa majibu kama hayo. Kwa kawaida mwanaume hana dalili za kimwili za kutoka damu kama mwanamke – ndio maana, karne na karne hakuna mtu aliyejali – lakini ni jambo la uhakika kwamba wanaume wanapata hedhi.

Dalili za mwanaume aliye kwenye hedhi ziko akilini zaidi na sababu ziko wazi: mwanamke asili yake ni kimwili zaidi, kihisia zaidi, na mwanaume ana asili ya ubongo zaidi. Lakini mwanaume anapata usumbufu ule ule anaopata mwanamke anapokuwa kwenye hedhi. Tofauti ni moja tu, kwamba mwanaume hatoki damu. Lakini kila mwezi, baada ya siku 28, hali fulani ya kiakili na kihisia itakuwa inajirudia.

Na kama umejaribu kujichunguza kwa mwaka mzima, utashangaa kwamba, ulikuwa na hasira mgomvi, mwenye huzuni na vingine vya aina hiyo, si hivihivi tu bali ni kwa sababu ulikuwa kwenye hedhi. Kama ukishafanya zoezi nililokwambia la dayari, jiulize, kama ulipokuwa kwenye hali hizo ulikuwa umekerwa na yeyote au chochote. Utagundua kwamba hukuwa umekerwa bali ulikuwa unasumbuliwa na hedhi yako.

Mwanaume na mwanamke wameumbwa kwa ‘matofali’ yaleyale, kwa maumbile yaleyale na baiolojia ileile. Tofauti yao ni kwamba
mwanaume ni chanya na mwanamke ni hasi kama tungekuwa tunazungumzia umeme. Huwezi kupata umeme kwa kuwa na chanya mbili; wala ukitumia hasi mbili bali ukichanganya chanya na hisi. Hivyo, kama mwanamke anapata hedhi kama hatua muhimu kuelekea mwito wa kimaumbile, haiwezekani mwanaume asipitie hatua hiyo, ingawa kwa uchanya wake.

Kupata hedhi kwa mwanamke inaeleweka kwamba, ni kutokana na wito wa kimwili. Maana yake ni kwamba, alikuwa amefikia hatua ambapo kimaumbile alitakiwa kujamiiana ili apate ujauzito. Je, kama hakuna mabadiliko kwa mwanaume, itawezekana vipi mwanaume kujamiiana na mkewe ambaye yuko kwenye hitaji hili la kimaumbile?

Ina maana basi kwamba mwanaume naye ni lazima kila mwezi awe na mabadiliko ambayo yatamfanya aingie mahali ambapo atavutana na mwanamke kimapenzi. Hili ni suala la maumbile ili kufanya kuzaliana kuwepo. Utajuaje kuwa mwanaume ameingia kwenye hali hiyo? Ndiyo pale ambapo wataalamu wamegundua hizo siku nne au tano za mabadiliko ya kiakili kwa mwanaume!

Mkuu tunashukuru kwa post nzuri... Lakini taratibu babu hizo highlight zinahusu, wanawake ndo chanya na waume hasi babu. Pia am curious to know, vip upo kwenye hedhi leo? mi ntamfanyia uchunguzi Ba msapu niprove hii hypothesis
 
Mtambuzi
Huo utafiti wamefanya Taasisi ya Cameroon?

Kama ni wenyewe, ndio sababu wanasema tukubali ndoa za jinsia moja, waume kwa waume.

Au sikuelewa somo la leo,?" Mwanamme anapata hedhi"

Kama anapata hedhi basi aolewe kama mwanamke, au?

Nina mashaka na utafiti huo wa taasisi hiyo ya Cameroon. Hawa wamekusudia kulazimisha ushoga tu.Watatumia kila mbinu.
 
huu ni upuuzi. kama ni
kweli basi mke na mume kuzaa lazima wote wakutane wakiwa katika hedhi
na
ingekuwa hivyo famile chache zingepata kuzaa. Ongea na daktari wako kwa
ufafanuzi zaidi. Huyu ana hiden agenda ambayo ni mbaya.

umeona eeeh...
 
Back
Top Bottom