Mara nyingi nimekua nikiamini kwamba yale tunayoyafahamu kuhusu maisha ni machache sana ukilinganisha na yale tusioyafahamu. Kiasi cha miezi kadhaa iliyopita nilisoma utafiti fulani kuhusu hedhi. Awali nilipousoma niliona ni hadithi tupu. Lakini nilipoona ni vyema kuujaribu kwa kutenda miezi minne baadae nilishangaa. Hata wewe najua utashangaa utakaposoma makala haya. Lakini ombi langu kwako ni kukutaka ujaribu kufanya mazoezi ili uthibitishe ukweli huo.
Miaka ya hivi karibuni imegundulika kwamba hata wanaume hupata hedhi-ingawa wanaume hawana alama za nje za kuwaonesha kwamba wako kwenye hedhi, kama walivyo wanawake ambao hutoka damu siku zao za hedhi zinapofika na kukamilika.
Kwa karne na karne hakuna mtu aliyekuwa akifikiria kwamba wanaume wangeweza kuwa wanapata nao hedhi kama wanawake. Kama mwanaume akiamua kuweka kumbukumbu zake kwenye dayari na kujiangalia kila siku hali yake inavyobadilikana kuwa ya kusikitika, ya kawaida, furaha na hasira……akiifuatilia hali yake namna hiyo kwa siku zote 28 za mwezi, halafu na mwezi unaofuata, akafanya hivyo hivyo, halafu mwezi wa tatu nao akatenda hivyo, na halafu ailinganishe miezi hiyo mitatu atashangaa.
Kuna siku tatu, nne au tano ambazo zitafanana katika dayari zote tatu, lini ana hasira ana masikitiko, ni mharibifu, na tabia nyingine kama hizo. Hivyo ndivyo vipindi vya hedhi kwa wanaume kama ilivyo kwa wanawake. Zoezi hili anaweza kufanya mwanaume yeyote, akishindwa kupata matokeo anaweza kuwasiliana na mimi na kuuliza ni kwa nini nimeandika uongo.
Ni jambo ambalo lipo na limeshafanyiwa tafiti mbalimbali, hata mimi binafsi nimefanya zoezi hilo kwa miezi minne na limetoa majibu kama hayo. Kwa kawaida mwanaume hana dalili za kimwili za kutoka damu kama mwanamke – ndio maana, karne na karne hakuna mtu aliyejali – lakini ni jambo la uhakika kwamba wanaume wanapata hedhi.
Dalili za mwanaume aliye kwenye hedhi ziko akilini zaidi na sababu ziko wazi: mwanamke asili yake ni kimwili zaidi, kihisia zaidi, na mwanaume ana asili ya ubongo zaidi. Lakini mwanaume anapata usumbufu ule ule anaopata mwanamke anapokuwa kwenye hedhi. Tofauti ni moja tu, kwamba mwanaume hatoki damu. Lakini kila mwezi, baada ya siku 28, hali fulani ya kiakili na kihisia itakuwa inajirudia.
Hahaha endelea na utafiti mkuu usiishie hapo sasa au ngoja nisubiri tu naweza kurupuka hapa good one