TANZANNIA
JF-Expert Member
- Sep 29, 2015
- 1,047
- 384
Ni juzi tu baada ya kutoka kwenye mihangaiko ya kutafuta riziki,muda wa sita kasoro hivi usiku naelekea nyumbani,nyumba kama ya nne hivi kabla sijafika kwangu nikaona watu wamelala nje kuanzia kibarazani hadi karibu na barabara,na maturubai yamefungwa,kama vile pana msiba,wengine wamewasha moto wanapika.
Nami nikahisi pana msiba,nikaendelea na safari yangu hadi nyumbani na kumuuliza wife kama hapo jirani pana nini,akasema hajasikia na wala hajui chochote.basi tukalala hadi asubuhi,kulipokucha nikakatiza mitaa ile ili kujua kuwa jana kulikuwa na nini,maajabu nikakuta pako shwari kabisa,hakuna dalili ya turubai wala moto,nikajaribu kuuliza watu wawili watatu wakasema hawajui chochote,nikabaki hoi....kweli usiku ni usiku.