Mkanda wa surual nilio uokota na kuutumia, kumbe haukua Mkanda

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,746
Nj story ndefu kidogo ila nitaifupisha,

Nakumbuka nikiwa kigoma naishi huko kwenye migazi na kusaga mafuta ya mawese, mazingira ya kazi yalikuwa hivi pembeni ya MTO ndo kuna kiwanda cha kusaga mafuta ya mawese na kutoka mtoni kama mita 500 ndo pana maturubai tumefunika kwa juu kwa ajili ya kuishi.

Sasa siku moja asubuhi naamka naenda mtoni kuchota maji ninawe uso nikakuta mkanda njia ya kuingilia mtoni, basi bhana nikachukua ule mkanda nika utundika pale juu kiwandani nikiamini kama kuna aliyeusahau atakuja kuuchukua.

Ule mkanda ulikaa kama siku tank hivi nikaamua kuuchukua na kuanza kuuvaa, ndani ya wiki moja nikaanza kuumwa nikaenda kupima nikaambiwa Nina taifod na UTI nikapewa dawa nikaanza kutumia lakini hazikunisaidia kitu zaidi ya ugonjwa kuwa afadhali ya Jana

Nikarudi tena kupima baada ya kumaliza dawa na halina kuwa vile vile, nikaambiwa Nina amwiba, nikapewa vidonge vya kutafuna lakini wapi, hapo sasa ndo nikahamia kwa mitishamba lakini halina ikazidi tu kuwa mbaya kwani nlianza kupiga hata 10 tu nakaa kupumzika, nilikonda vibaya mno.

Basi bhana nilipata nafuu kidogo nikamuomba boss nirudi nyumbani singida akakubali, nikakata tiketi ya treni mpaka morogoro maana niliamua kwenda Arusha kwa kaka, lakini hapo nyuma kuna wamama walikuwa wanaongea eti Mimi nimetoka singida na kupata kazi wakati watoto wao hawana kazi.

Basi bhana halafu kipindi hicho nilikuwa najisaidia choo kama ya mbuzi, baada ya kufika morogoro nilipanda gari hadi Arusha mererani kwa kaka, nilipofika tu halina ikarudi upya mpaka kaka akanichukua na kuamua kwnda kunipima UKIMWI japo mm nilikuwa sijui na hakuniambia, ila nilijua baada ya dokta kuuliza Mara ya mwisho kupima ilikuwa ni lini na majibu yalikuwaje nikamwambia basi akaniambia Niko poa.

Tukarudi nyumbani na kuendelea kuhangaika na kunywa dawa yofauti maana tukienda maabara wanatuambia ni malaria lakini wakitupa dawa hazifanyi chochote, ilikuwa usiku nikilala shuka linaloana kwa jasho ukikamua maji yanatoka, na nilikuwa natetemeka mno basi bhana nilipata nafuu kidogo kuna tajiri akawa anatafuta mfanya kazi sasa kaka akaniambia niende tu nikajisikilizie huko huko.

Nikakubali nikaja mpaka Arusha mjini nikaja nikaanza kazi ya kufuga kuku na u houseboy nikawa napata shida kwani nilikuaa natetemeka mikono yaani nikishika kikombe cha chain chain inamwagika, hivo nilikuwa nakunywa chain kwa kuinamisha kikombe kikiwa mezani.

Baada ya hiyo halina kuisha nikaanza kuvimba korodani, moja ya kulia na baadae ikafuatia ya kushoto, hapo ujanja ukawa hakuna kwani hiyo halina niliamua kuificha kwa bosi wangu lakini ikawa ngumu kwani nilishindaa hata kuvaa surual nikawa natembea nimepanua miguu.

Muda huo kaka alikuwa ananitumia dawa za kienyeji na bosi nilishamwambia ile halina ikawa inaisha na kabla sijapona inarudi tena yaana.

Lakini sijui nini kilitokea nikamwita Dada wa kazi na kumwambia njoo na mafuta ya taa, nikachukua ule mkanda na kuutoa kiunoni na kuuloaanisha na mafuta ya taa na kuuwasha moto na kuungua kabisaa, tokea siku hiyo kila kitu kikawa shwari kabisa,

Sijui ni kitu gani kilinijia kichwani ila naamini ni Mungu ndo alinionyesha.
 
Ni nyoka ulikuwa unatembea nae. Hapo Kuna mtu aliambiwa akatupe ili aokoke na matatizo yalio mpata sasa wewe hukujua na si mkanda tu hata pesa njia panda usiokote ni mikosi imetupwa.
 
Ni kweli watu hutupa majini mikosi yao njia panda majalani kwenye miti mikubwa makaburini baharini ukiwa mwenzangu na mie mwepesi au tamaaa umeona pesa basi unayavagaa japo wengine wanatambuka bila kujua unabeba majini mikosi uchawi wa mtu.
 
Ndo maana wakaweka wakajua rahisi kushawishika kuwa na roho ya kukinai,potozea Je mfano ungekuwa mkanda wa mtu alouliwa ukakutwa nao wewe si balaa Hilo, jiepushe sana na vitu unavyo weza kuepuka nishaokota kanga mtu katupa nikaachana nayo maana sijui mtu katupa kweli au katupa mambo yake.

Mimi nilkuta njiani bulungutu la noti za 10,000, na nikaliacha. 🤣🤣
 
Back
Top Bottom