Haya ndio mambo ninayotaka kusikia kwa sasa.Thanks mleta ujumbe
Nimeduazwa na kampeni za Obama na Romney kwenye mbio za kuelekea IKULU ya Marekani hivi juzi kwenye mdahalo wao wa pili. Obama na Romney yeyote atakaepita sera yake ya kwanza ni kurudisha viwanda Marekani ili wamarekani wapate ajira. Viwanda vingi vya Marekani vilihamishishiwa bara la Asia kwasababu thamani ya USDollar ni kubwa mno inayofanya gharama za uzalishaji ziwe kubwa mno Marekani, hivyo wenye viwanda walikimbilia China, India, Singapore, Japan, Africa kutafuta faida. Baada ya Marekani kushindwa kuishawishi China iongeze thamani ya fedha yake sasa wana mkakati wa kuishusha thamani ya dollar yao ili kuvutia uwekezaji na wamarekani walioikimbia nchi kibiashara kurudisha mitaji yao ya viwanda nchini mwao. Kwasasa Marekani haina viwanda kabisa, ukifika pale Detroit mji ambao ulikuwa chimbuko la viwanda duniani sasa hivi yamebaki magofu tu watu pia wameukimbia mji na majumba yao kwa kukosa ajira. Nikiwanda cha kutengeneza magari ya FORD tu ndicho bado kikubwa kilichobakia pale. Mkakati mwingine wa kukuza uchumi wao ni kuanza kuchimba mafuta na gesi yao wenyewe badala ya kuagiza bidhaa hizo ng'ambo. Hivyo, bei ya mafuta duniani nayo itashuka miserably kwakua mnunuzi mkubwa atabakia China na India tu. Kama Obama atapita atapunguza matumizi ya kijeshi kwa kupunguza ukubwa wa jeshi na kuacha vita Afghanstan. Hivyo nawapa tahadhali watu wanaoiabudu sarafu ya US$ kuwa kuweni chonjo msije mkapata hasara ghafla punde dola inaposhuka kufuatia mabadiliko ya kiuchumi yanayotarajiwa kufanywa marekani baada ya uchaguzi wa NOvemba.
Soon itakuwa 1$ = 1Tsh.
Kwa hiyo itachukua muda gani kufikia 1Tsh = 1$?Unaota ndoto? Kwa nini Japana pamoja na export ya bidhaa za dhamani kubwa duniani lakini pesa yake ingali inatambaa chini? Kwa nini wanafanya hivyo? Mashirika ya fesha duninia yako wapo na yanahodhiwa na nani?
Sababu kubwa inayopelekea wafanyibiashara wa Kimarekani kuhamishia viwanda vyao nchi za Asia ni gharama ya uzalishaji. Hapa Marekani miminum wage nadhani ni dola $7.50 wakati nchi za Asia unaweza kuwalipa wafanyikazi dola moja kwa saa na hizo zikaonekana kuwa hela nyingi za mshahara. Uzuri wa kushushwa kwa thamani ya dola ni kwamba bidhaa ambazo bado zinazalishwa Marekani, zitakuwa na bei rahisi katika masoko ya nje, hasa masoko ya Ulaya, na itawavutia watalii wa kigeni, hasa kutoka nchi tajiri, kama vile Ulaya na Japan, kutembelea Marekani. Unakuta viwanda vikubwa kama Nike vinawalipa wafanyikazi wake chini ya dola moja kwa saa halafu wanauza viatu vya Nike katika maduka ya Marekani kuanzia dola $60 kwenda juu. Lakini all in all, hata kama dola itashuka thamani, tusitegemee kwamba shilingi ya Tanzania automatically itapanda thamani. Hiyo ni dynamic nyingine kabisa.
Tatizo la kutokusoma uchumi.Hujui hata maana ya kushusha thamani dolla.Pili fuatilia kila uchaguzi unaposogea dolla huwa inakuwaje,Swala la ajila lipo kote China hali ni mbaya sana hata uchumi wao umeshuka sasa kwa miezi kama minne.Elewa uchumi siku zote sio Static
siku dunia ikifika mwisho atakaporudi masihaKwa hiyo itachukua muda gani kufikia 1Tsh = 1$?
Ninachopenda viongozi wa hizi nchi zilizoendelea wako very strategically na ni rahisi mno wao kujitathmini na kuona mapungufu yao.......sio huku kwetu