Kumbe udini ndio ulitumika kumdhuru Lowassa kisiasa?

Kumbe udini ndio ulitumika kumdhuru Lowassa kisiasa?

Acha Matusi, angalia huo waraka kwanini ni Udini ndio Mantiki ya Chama Cha Mapinduzi?

Hayo ndio Maoni yangu weka Maoni yako na sio kutukanana? WOW AND YOU HAVE JUST JOINED JF MAY 25 2011
NAONA UMETUMWA!!!

When the sun rises, it rises for everyone

akili yako inakwambia anayejiunga humu ndani na kuamua kukosoa papo hapo basi ametumwa eeh?? kweli zero brain wamejaa humu na wewe kiongozi wao
 
How about you? a New Person Just Join May 25th 2011? Hauna Chuki?

sasa kuna kosa gani kujiunga sasa hivi na kuanza kukosoa papo hapo??
sijaelewa hii mantiki ya kusema kwamba mtu kujiandikisha leo na kukosoa hapo hapo eti kwamba ametumwa..
chuki iko wapi ??
 
Ncheme Nchicheme?
Nakala chapishi
Mtumie mwenzio
Jiandikishe utaarifiwe



Masikini Mzee Ali Hassan Mwinyi!

Ncheme Nchicheme? Oktoba 31, 2007




TUNGEKUWA tumejaaliwa uungwana na Mwenyezi Mungu, nasi tukawa ni watu wa kukiri makosa yetu na kisha tukawa na moyo wa kutaka radhi wale tuliowakosea, basi Watanzania wengi tungekuwa tumekwisha kuunga ujumbe wa watu wasiopungua 500 kwenda kuanguka chini ya miguu ya Mzee Ali Hassan Mwinyi huku tukimwomba atusamehe kwa makosa makubwa tuliyomtendea.

Ujumbe huo ungepaswa uongozwe na wahariri na wasanifu wakuu wa tahariri katika magazeti ya miaka ya mwanzo ya 1990, kwa sababu sisi ndio hasa tulikuwa msitari wa mbele katika kutenda makosa hayo dhidi ya mzee huyo ambaye tulimbatiza jina la "Mzee Ruksa".

Kosa kubwa tulilotenda dhidi ya Rais huyo wa Awamu ya Pili ilikuwa ni kumhusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi, hata kuwafanya wasomaji wa magazeti yaliyochapishwa wakati huo, waamini kwamba kilichokuwa kikifanyika Ikulu ulikuwa ni uharamia wa hali ya juu.

Sasa tunajua kwamba yote haya hayakuwa kweli. Haiwezekani kusema kwamba Mzee Mwinyi hakuwa na dosari, kwani kusema hivyo ni kumwondoa kwenye kundi la binadamu.




Alikuwa na dosari zake na udhaifu wake, na hayo bado anayo hadi leo, kwa ilivyokuwa wakati akiwa Ikulu. Lakini pia ni kweli kwamba sehemu ya udhaifu wake ilitokana na wema na upole wake katika mazingira ya "manyang'au" aliowaamini na ambao hawakusita kuutumia upole wake na jina lake kufanya walivyotaka kwa kumsingizia yeye.

Leo hii sote tunajua kwamba tulimwonea sana Mzee Mwinyi kwa kumbebesha mambo yasiyokuwa yake. Na wala si yeye peke yake aliyekumbwa na uonevu huo bali pia mkewe, Bi Sitti Mwinyi, ambaye naye alihusishwa na kila aina ya maovu kutokana na uvumi ulioenezwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Baadhi tutakumbuka pia kwamba Mzee Mwinyi aliwahi kulalamika hadharani kwamba uvumi ulikuwa umeenezwa kuhusu yeye kumwoa kigori mdogo kwa kumfanya aache shule… kila aina ya uvumu na uzushi. Mzee huyu muungwana alivumilia, akavuta subira, akasamehe. Haishangazi kwamba amebaki kuwa kipenzi cha Watanzania kutokana na upole, unyenyekevu na uadilifu wake.

Tunajua sasa kwamba, ingawaje vitendo vya ufisadi vilitendeka chini ya uongozi wake, yeye mwenyewe binafsi hakuhusika moja kwa moja.

Baada ya Mzee Mwinyi kuondoka madarakani ndipo nchi hii imepata bahati mbaya si tu ya kuendelea kuelemewa na vitendo vya ufisadi katika safu za uongozi, bali pia mkosi wa kuwa na ‘kiongozi' mkuu anayesimamia ufisadi huo kwa kushiriki yeye mwenyewe binafsi kuunda kampuni ya biashara na kuisajili rasmi kwa anwani ya ofisi ya umma, na hata kujihaulishia umiliki wa kampuni ya serikali na kuiandikisha kwa jina lake na familia yake na maswahiba zake.

Tumshukuru Mungu tunayo Katiba inayoweka mipaka ya mihula ya uongozi, la sivyo baada ya mihula mitano tungeikuta nchi imehamia bara jingine kwa jinsi tamaa za wakuu zilivyozidi na jinsi matumbo yao yalivyo na nafasi za kujaza.

Kisha tumshukuru Mzee Mwinyi kwa uungwana wake, na mwisho tumwombe radhi kwa jinsi tulivyomdhalilisha.

Raia Mwema Toleo Na 1.
 
nimesoma habari hii vizuri sana. kama ni kweli hiyo ni mipango ya muheshimiwa basi mipango hiyo .ISHINDWE KWA JINA YESU AMENI.
 
Amefanya kazi wapi na ukaona uimara wake? Unajua kama mtu hajafanya kazi ya kumuonyesha kwenye public anakuwa na mwamvuli mzuri. Lakini mimi simjui vizuri.

Asha Rose ni lawyer, wakati nafanya kazi in one of the trusted NGO (jina kapuni) tulikua tunamtumia sana kwenye ushauri wa mambo mbalimbali. Nimefanya naye kazi kwa ukaribu nikiwa kwenye NGO hiyo, lakini wakati huo alikua hasikiki sana; watu walimjua kama senior lecturer of UNIV of Dar-es-salaam. Ni kutokana na reputation yake aliyokua nayo wakati huo ndio alipitishwa kutusaidia katika kutupa ushauri kwenye issues za human rights etc. Infact wakati huo sikujua kama ni mwanachama wa CCM damu kiasi hicho. However siwezi kusema sana labda there is another side of her I did not see. Wakati mwingine watu wanafanya kazi au wana-respond kutokana na mazingira yaliyowazunguka.
 
Waliyemzuia Lowasa asiwe Rais mwaka 2015 ni wale waliomzuia Mzee Malecela mwaka 1995.

Ni nani hao?

Ni wakatoliki

Waislam hawajawahi kuwa na uaduia na walutheri!

Chukua maneno yangu uyarekodi mahala. Raisi 2015 ni ama Magufuli au Membe vinginevyo atakuwa Padri Slaa. Halafu fuatilia ni dhehebu gani wote hao!

Asiyeamini amuulize Philemon Michael.
 
Watanabe nani kakwambia rais ajae anatoka CCM?! Naomba kila penye neno 'Mrithi wake' weka 'Mgombea wa CCM' alafu rekebisha Tamati/Hitimisho ya taarifa ongezea na fafanua ni kwa jinsi gani Lowasa alionewa katika sakata la Richmond na Dowans? lasivyo toa neno Lowasa alitolewa kwa sababu za Udini! Lasivyo nitafikiria kuwa lengo lako kuu ni tumia huo mwanya kumsafisha Lowasa!

Nyie tumieni njia yoyote ile kuchakachua mambo yenu lakini 2015 msiote ndoto kama hamta badilika kuanzia kwenye unyayo hadi utosini.

Mtaisikia Ikulu kwenye magazeti na kama Mkileta mambo ya Laurent Gbagbo atakiona cha moto kwa taarifa yako huyo Rais wako yupo katika Black list na uhusiano wake mchafu na Qadhaffi unaeleweka ila kawekwa kiporo!
 
Kama ni kweli Migiro na Mwinyi ndiyo tarajio la Kikwete/CCM kwa urais wa 2015,basi CCM wajiandae kuwa chama cha upinzani.Likipigwa hili zengwe,lazima baadhi ya vigogo wa CCM watajiondoa na kuanzisha chama chao au watakwenda CHADEMA.Vyovyote vile Mwinyi na Migiro hawana ubavu wa kushinda Urais wakisimama against Lowasa,Dr.Slaa,Sitta au Magufuli
 
Waliyemzuia Lowasa asiwe Rais mwaka 2015 ni wale waliomzuia Mzee Malecela mwaka 1995.

Ni nani hao?

Ni wakatoliki

Waislam hawajawahi kuwa na uaduia na walutheri!

Chukua maneno yangu uyarekodi mahala. Raisi 2015 ni ama Magufuli au Membe vinginevyo atakuwa Padri Slaa. Halafu fuatilia ni dhehebu gani wote hao!

Asiyeamini amuulize Philemon Michael.

Acha kuwalaumu wakatoliki.Aliyemnyima Urais Malecela 1995 ni Nyerere,na again 2005 ni Mkapa ndiye aliyemuengua.Ingawa hao wawili wote ni wakatoliki,haina maana kuwa wanawakilisha wakatoliki wote Tanzania
 
Kama ni kweli Migiro na Mwinyi ndiyo tarajio la Kikwete/CCM kwa urais wa 2015,basi CCM wajiandae kuwa chama cha upinzani.Likipigwa hili zengwe,lazima baadhi ya vigogo wa CCM watajiondoa na kuanzisha chama chao au watakwenda CHADEMA.Vyovyote vile Mwinyi na Migiro hawana ubavu wa kushinda Urais wakisimama against Lowasa,Dr.Slaa,Sitta au Magufuli

Kwa CCM kila kitu kinawezekana kwa sasa. Mbona wamekua kimya hivi kwenye maswala muhimu ya nchi e.g. mikataba mibovu, mfumuko wa bei, uvunjwaji wa haki za binadamu, bunge linaendeshwa kihuni tu nobody says anything that make sense etc. Even kenye issues walizo-introduce wao kama kujivua gamba nalo linawafanya bubu. What else is not possible?
 
Sio haki kuhamisha thread ya mtu na kuipeleka sehemu asiyokuwa na access nayo. Nimeonelea nichukue kifungu hiki cha maneno tujikumbushe na tutafari kuwa kama hii lililozungumzwa ni sahihi bali kuna fact yake iliyosababisha hilo. Fact yenyewe ni udini wa EL kwa kuwekeana mkataba wa siri na makanisa ingawa JK kashindwa na kaachia. sasa endelea....
Kuna tetesi Zimeenea mtaani kuwa baada ya JK kuingia madarakani aligomea ruzuku iliyokuwa ikitolewa na Serikali kuendesha makanisa pamoja na taasisi zinazoendeshwa na makanisa katoliki nchini kama shule, hospitali na vyuo. "The Government shall provide financial assistance to Church institutions and shall seek financial assistance to Church run social services in its bilateral negotiations with foreign governments"

source
:The Memorandum of Understanding between the Government of the United Republic of Tanzania and the Tanzania Episcopal Council (TEC) and the Christian Council of Tanzania-page 3 (attached herewith)

Nasikia JK aliwaambia kuwa nchi hii haina dini na itakuwa ubaguzi kuwapa ruzuku watu wa dini moja na kuwaacha wa dini nyinginezo akatolea mfano kuna waislam, wabudda, masingasinga, wahindu na wasiokuwa na dini je hao hawana haki ya kupewa ruzuku? na serikali ikitoa ruzuku kwa hawa wote itawezaje kujiendesha? Basi bora mkose wote. Hapo naona JK aliona mbali sana ila hakujua kama anajiharibia yeye na chama chake.


NA NDIO MAANA KWA KUTUMIA MLANGO WA NYUMA KUNA CHAMA KIKASIMAMISHA WATUMISHI WA MUNGU KWA WINGI NA KUFANIKIWA KUPENYA KILA PEMBE YA TANZANIA.
 
Nikikumbuka fitna chafu za m-kwere dhidi ya Salim wakati ule wa mchakato ndani ya ccm. Nashindwa kutoiamini habari hii. Haiwezekani awe malaika sasa hivi... Wanasema 'hasidi haachi asili'
 
Kwa CCM kila kitu kinawezekana kwa sasa. Mbona wamekua kimya hivi kwenye maswala muhimu ya nchi e.g. mikataba mibovu, mfumuko wa bei, uvunjwaji wa haki za binadamu, bunge linaendeshwa kihuni tu nobody says anything that make sense etc. Even kenye issues walizo-introduce wao kama kujivua gamba nalo linawafanya bubu. What else is not possible?

Mkuu;kifupi ni haiwezekani.Hata kama wanategemea dola au kuiba kura,hili litawashinda.Ukipata 20% na mpinzani wako akapata 80%,utaibaje hizo kura sasa???
 
Watanzania bado imara na wanajua nini wanataka manake kama kuwashiwishi kupitia chuki za kidini bado kuleta matunda yanayokusudiwa na waroho wa madaraka. Raisi anayo haki ya kuchagua watu anaotaka kufanya nao kazi na kikwete sio wa kwanza mbona baba wa taifa katika hili atolewi reference?

Hoja nzuri lakini haina maslahi kwa mtanzania wa kawaida.
 
Samahani,

Mwenzenu siku hizi Nina allergy na magazeti yetu. Eti huu upupu umepulizwa RAIA MWEMA?

Omarilyas
 
Hoja hii inauma hasa kwetu wakristo. In God we Trust and always JESUS is power.
 
Back
Top Bottom