Kama kawaida yako unaandika makala mwenyewe halafu unazuga eeeh! Jibadilishe utakavyo jibadilisha lakini utajulikana tu. Mdini mkubwa we!
Hii makala imeenda mbali sana na kutoa madai mengi sana mazito; ni madai mazito ambayo hayapaswi kuachwa bila kujibiwa. Ni madai ambayo yametolewa kuhusu watu mbalimbali yakidai ukweli. Sijui kama mwandishi ana majibu yenye kuweza kutosheleza na kutetea madai yake. Ila kuna kitu hapa nadhani kinafikiicha kwa chini. Tunapozungumzia udini hauko kwa wanancdhi wa kawaida - at least not the majority of our people. Ni udini wa baadhi ya viongozi na watawala ambao wanautumia ili aidha kubakia madarakani au kuja kuingia madarakani.