Kumbe Udhaifu wa Tulia ulionekana toka enzi anaomba kuwa Naibu Spika

Papushikashi

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
10,918
13,235

Hapa ni wakati anaomba kuwa naibu spika. Alijikanyaga sana alipoulizwa ni lini alihama kutoka kuwa mtumishi wa serikali hadi kuwa mwanasiasa?

Hata hivyo wabunge hawakukubaliana na majibu yake na kuanza kusema kuwa alibebwa, wapo wengine walimwambia kuwa aliingia kwa mlango wa nyuma.

Nahisi huyu dada ana hasira na wabunge hasa wa upinzani kutokana na mizaha waliyomfanyia siku hiyo akiomba nafasi ya kuwa naibu spika.
 
Ccm ipo mahututi hakika maana siku ya uchaguzi wa naibu spika bungeni mama tulia aliulizwa maswali akabaki kuhamaki asijue la kujibu.Yaani nilijiuliza hivi ilikuwaje akawa naibu mwanasheria mkuu wa serikali?Ccm hakishindikani kitu.
 
Watu walijua mapema kuwa huyu atakuwa tatizo ndiyo maana wabunge wanaimba amebebwa amebebwa amebebwa.................................
 
Hivi ni Mbunge gani huyo aliyeuliza swali hilo?
Jingine kweli Wapinzani wanastahili kuacha mihemko , hata kama kinachozungumzwa na mtu pumba muda mwingine kumsikiliza mtu ni busara na jambo la heri ili wasikizaji nao waweze kupata nafasi ya kupima mzani wa hoja.
 
Tatizo watu walishajua katumwa kwa Kazi maalum
 
Sidhan kama haya yanaumuhimu kwa sasaa, anahitaji kujirekebishaa.
Bado ni mgeni, anahitaji kujifunza zaidi.
 
Sasa kwa mwendo huu unategemea asifanye hayo anayoyafanya? Jambo la kushangaza kabisa ni kwamba baada ya kushindwa kabisa kujibu swali CCM walimpongeza alipokuwa anarudi kwenye kiti. Hii clip inaonesha hata spika alimbeba kuondoa aibu. Kaazi kweli kweli.
Ni aibu sana kwa wabunge wa CCM
 
Umechukua kadi lini? Jibu : wasio ruhusiwa kuwa wanachama wa. ....... Prof. Unatoa marks ngapi hapo?
 
Ccm ipo mahututi hakika maana siku ya uchaguzi wa naibu spika bungeni mama tulia aliulizwa maswali akabaki kuhamaki asijue la kujibu.Yaani nilijiuliza hivi ilikuwaje akawa naibu mwanasheria mkuu wa serikali?Ccm hakishindikani kitu.

Nilisikia huko siku aliyoondolewa watu walienda kukitwanga kwa furaha maana hata huko inasemekana alikuwa ni mzigo
 
Back
Top Bottom