Kumbe Ubaguzi ni sera ya serikali ya Afrika Kusini!

MIDFIELD

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2013
Posts
1,944
Reaction score
703
Great thinkers habari zenu, wakubwa shikamooni.
Leo nimesikitika sana kuona kumbe suala la wa-Afrika kusini kuwabagua wa-Afrika wenzao lililokuwa likifanywa na hawa watu ilikuwa ni kutekeleza sera ya wakubwa wao (serikali yao) japokuwa sisi tulidhani walikuwa wahuni wachache kama serikali yao ilivyotaka kutuaminisha. Leo hii BBC wamenena ukweli ambao wameupata kutoka kwa wahamiaji nchini humo. Hili limedhihirishwa na mhamiaji mmoja toka DRC aitwaye Jean, ambapo watoto wake watatu walinyimwa kusoma shule za serikali bila sababu maalum. Ilimlazimu kuwapeleka shule ya binafsi ambayo nayo inaendeshwa na wageni. Na shule hii ilianzishwa mwaka 2008 baada ya machafuko kama haya ya kufukuza wageni weusi na kuua watu wapatao 62. Hata hii shule inatishiwa kufungiwa kwani wamekataa kuwapa usajili bila sababu maalum pia, kwa mujibu wa mmiliki. Na wametafuta wanasheria kuishitaki serikali kwa hilo.
Kwa hiyo jamani kumbe hili suala ni sera ya kina Zuma na serikali yake. Wanapojidai kuwakemea watekelezaji ile ni geresha tu.

My Take; Hivi huu ubaguzi hawa waafrika kusini wameambukizwa na wazungu waliowatawala???
 
Mkuu hata mimi nmeangalia hyo habari mpaka mwili ukasisimka.Eti wana sera ya kuwazuia watoto wasio raia wa Afrika Kusini wasisome Shule za Serikali.Yaani kwa mfano wa ndg zetu waliokimbia vita kuja kwetu watoto wao hawaruhusiwa kusoma Shule za Serikali.

Hii ni hatari
 
wJwCMyHDSOCXrW96ABhN
 
Wa-south Africa hawana Shukrani ( shukrani za punda ni Mateke) Ni wakati wa kuwafukuza na wao na makampuni yao na wachina wapewe nafasi zao
 
Robert malawa yule mtangazaji alikua sabc,South Africa Broadcasing Cooperation. Ni ya umma alipotuhumiwa kuwa inasemekana ni raia wa Zimbabwe alitimuliwa kazi on sport.Akaja kupata ajira multi choice kampuni binafsi. Watumishi wa serikali ndio wabaguz namba moja kuriko wale walioonekana wakiua,,uhamiaji,afya,elimu,police wana rugha za kejeli sana kwa wageni bt ssa wamejifunza maana kuona wasauzi weengi wakirudi na wao toka msumbiji,nigeria,zimbabwe na makampuni yao kufungwa biashara wamejifunza kitu ambacho walikua hawakijui kuwa kuna wasauzi wengi nje pia..
 
dawa yao ni serikali za africa kuwawekea vikwazo vya ki uchumi hawa punda wenye kurithi tabia za kikaburu.nimemkumbuka nyerere angekuwepo nadhani wangefukuzwa wote tanzania
 
Mimi sielewi kwa nini watu wanaenda kutafuta maisha huko bondeni.

Hivi huko watokako maisha ni mabaya na magumu kiasi hicho?
 
huku kwetu bado tuko kimya. raisi mtarajiwa alisema watz kule south wako 21 na wote wako salama. weka mbali na watoto
 
Mkuu hata mimi nmeangalia hyo habari mpaka mwili ukasisimka.Eti wana sera ya kuwazuia watoto wasio raia wa Afrika Kusini wasisome Shule za Serikali.Yaani kwa mfano wa ndg zetu waliokimbia vita kuja kwetu watoto wao hawaruhusiwa kusoma Shule za Serikali.

Hii ni hatari

Haswaaaa, yaani nikagundua kumbe hawa jamaa ni wabaguzi kutoka moyoni. Wakati wao walikuwa wanasoma, wanapewa mafunzo ya kijeshi wkt wanapigania kumwondoa kaburu nchini mwao na tuliwajengea hata camps pale morogoro kwa wanaojua. Na wengine walizaa hadi watoto na wameacha mbegu zao kwa dada na mama zetu hapa Tz
 
Mimi sielewi kwa nini watu wanaenda kutafuta maisha huko bondeni.

Hivi huko watokako maisha ni mabaya na magumu kiasi hicho?

Kwa kweli mkuu Nyani Ngabu hata mimi nashangaa sana kwani hawa watu walishaonesha kuwachukia toka 2007 kama sikosei
 
dawa yao ni serikali za africa kuwawekea vikwazo vya ki uchumi hawa punda wenye kurithi tabia za kikaburu.nimemkumbuka nyerere angekuwepo nadhani wangefukuzwa wote tanzania

Kusema kweli kama Afrika tungewatenga hawa watu wangejifunza kwa tabia zao mbaya kabisa. Wakae na nchi yao wanaojiona wameendelea sana, wakati hata Nigeria imeshawapiku kiuchumi
 
Robert malawa yule mtangazaji alikua sabc,South Africa Broadcasing Cooperation. Ni ya umma alipotuhumiwa kuwa inasemekana ni raia wa Zimbabwe alitimuliwa kazi on sport.Akaja kupata ajira multi choice kampuni binafsi. Watumishi wa serikali ndio wabaguz namba moja kuriko wale walioonekana wakiua,,uhamiaji,afya,elimu,police wana rugha za kejeli sana kwa wageni bt ssa wamejifunza maana kuona wasauzi weengi wakirudi na wao toka msumbiji,nigeria,zimbabwe na makampuni yao kufungwa biashara wamejifunza kitu ambacho walikua hawakijui kuwa kuna wasauzi wengi nje pia..

Kwa kweli suluhisho sahihi ndiyo hilo. Ni kuwafukuza na wao watu wao, wasidhani kuwa wao tu ndiyo wenyehaki ya kuishi nchi za wenzao. Dawa ni kuwarudisha tu kwao ili wakasimuliane huko
 
Nilipata kumsikia ndugu mmoja clouds fm-mtu yeyote mwenye passport ya Tanzania anachukiwa sana na wasimamia sera kwa sababu ya namna tulivou saidia wapinduzi ya SA huru ya leo"
 
Mimi sielewi kwa nini watu wanaenda kutafuta maisha huko bondeni.

Hivi huko watokako maisha ni mabaya na magumu kiasi hicho?

Kwa Tz bado maisha hayajawa mabaya kiasi hicho,labda hizo nchi zingine.
 
Haswaaaa, yaani nikagundua kumbe hawa jamaa ni wabaguzi kutoka moyoni. Wakati wao walikuwa wanasoma, wanapewa mafunzo ya kijeshi wkt wanapigania kumwondoa kaburu nchini mwao na tuliwajengea hata camps pale morogoro kwa wanaojua. Na wengine walizaa hadi watoto na wameacha mbegu zao kwa dada na mama zetu hapa Tz

Wapo kina John Dillinga (DJ JD) na pale Morogoro kuna watoto wengi tu wa kizazi chao ila Mungu yupo..
 
Ahaaa, kumbe John Dillinga ni Msouth! The Everlasting DJ or DJ of the Past, Present and Future! Big up kaka kutufahamisha
 
Mweusi anambagua mweusi mwenzake kisa mali, lakini si SOUTH TU HATA HAPA KWETU TUNABAGUANA SANA kujiona kabila na dini fulani ni wasomi na wenye mali sana TOFAUTI YAO NA SISI WAO WENZETU HAWAUWEZI UNAFIKI KAMA SISI TULIVYOWANAFIKI
 
Back
Top Bottom