Kumbe tunaongoza kwa uvumi…!

Kumbe tunaongoza kwa uvumi…!

katika vitu ambavyo sivipendi ni uvumi/udaku unapotezea sana watu muda, ukiwa na upeo mdogo na huna shughuli ya kufanya huo udaku, uvumi, majungu, masufuria ndio kazi yake. but time will tell
 
mid twenties, 23<my age<27

Oh okay, ndo maana basi.

Mumiani ni wanyonya damu. Kwenye miaka ya 80 walivuma sana jijini Darisalama. Kulikuwa na uvumi kwamba walikuwa wanalenga watoto wa shule za msingi.

Mimi nakumbuka siku moja tulikuwa darasani mara jamaa mmoja akatoka baruti huku akisema kawaona hao mumiani. Hapo kulikuwa hakuna cha kuuliza tena wala nini maana kila mtu alitoka nduki kuelekea maporini.

Ninachohisi kilichosababisha huo uvumi ni blood drives zilizokuwa zinaendeshwa na mashirika kama ya msalaba mwekundu.
 
yeah, you are right, ilikuwa ni mwaka 1988, ilisemekana jamaa alikuwa na nyumba ndogo, sasa mke akamwendea kwa mganga huko Kipalang'anda akapewa dawa aiweke kwenye maji yake ya kuoga ili jamaa akioga tu anamsahau nyumba ndogo na kumpenda mkewe.... sasa kwa mujibu wa uvumi huo, jamaa alipojimwagia yale maji si ndio akageuka nyoka aina ya chatu....

Nilikuwa naishai Buguruni wakati ule maeneo ya Kwa Makukula nyuma ya Kituo cha Polisi cha Buguruni na huo mkasa nilikuwepo mwanzo mwisho ni bahari mbaya tu nilivunjika mkono baada ya kuanguka wakati tukiwakimbia FFU waliokuja kutawanya watu...........

Labda kwa sababu ulikuwa mdogo ila nadhani hayo yalikuwa ni malipo halali ya kuwa shuhuda wa tukio..lol!!
 
MtambuziNakubaliana na utafiti huo kwa asilimia fulani, ebu angalia swala la fremason hata Tanzania jinsi linazungumziwa hakuna hata mtu mmoja mwenye kujua kuhusu hilo swala lakini ndio watoa habari wa kwanza, pia viongozi wetu wanatumia hiyo kama fursa ya kuweza kuwafanya watu wajinga ili waweze kuwatawala vizuri.
Na serekali inatakiwa ihakikishe inaweka sheria kuwabana vyombo vya habari vinavyoeneza habari za uzushi, ila yenyewe siri inaweka wazi na byana inafichwa kwa mfano walipolifungia gazeti la mwanahalisi je ni kweli walijiridhisha kuwa zile habari zilikuwa ni uzushi au ilikuwa siasa??
mbiona tunaona vijigazeti vingine vinaweza hata kutoa habari kuwa kuna mtu kafufuka mahali fula na wakawahoji watu hewa na kuweka picha za uzushi na wanauza ndio bishara inavyowenda.
nilikuwa naangalia kipindi cha Who want to be a millionaire cha BBC E nikajifunza kuwa wenzetu wana uelewa wa mambo mengi sana tofauti na sisi watanzania ambao vyanzo vyetu vya habari ni madalali, madereva teksi, wapiga viatu rangi, wauza kahawa, vinyozi na waudumu wa saloon, walinzi na wafanyakaziwa ndani. yaani habari za kizushi full
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana kabisa na hiyo assessment. Nataka tu kujua nani alifanya huo utafiti kwa sababu kusema ukweli, mtu wala huhitaji kufanya utafiti rasmi kugundua kuwa sisi Watanzania ni watu wa kuamini amini tu bila mpango.

Hata kwenye swala la kiimani za dini tuko hivyo hivyo ndio maana siku hizi unaona kunaibuka vijikanisa vingi maana watja tupo wengi??
 
Ila mtambuzi hilo la kunatana ni la kweli kama lilivyowasilishwa that time...source a friend of mine doctor Temeke and another Muhimbili kwani picha nzima iliishia Mhimbili. Na mwanaume alifariki kwa pressure..Sitaki maswali kwani sikuwepo.

uvumi cont........
 
Tatizo wengi wetu hatuna kazi na wagumu kupambana na ufukara

Kuondoa ili ni kuchakalika kwenye kilimo uvumi na biashara isitoshe kila shilingi tuipatayo kwenye izi kazi zetu iwe muhimu kwenye maisha yako ya baadae
​
 
Hebu ngoja kwanza...hiyo ya jamaa kugeuka nyoka ilisababishwa na jamaa kutoka na mke wa mtu ama ilisababishwa na dawa ya penzi ambayo mkewe na huyo nyoka mtu alimwekea mumewe kwenye maji ya kuoga ndiyo jamaa akageuka chatu?

Halafu kwa kumbukumbu zangu, hiyo ilitokea miaka ya '87 au '88. Hiyo si miaka michache iliyopita. Ni miaka 26 au 25 iliyopita...hiyo ni miaka mingi.

yote hii sababu ya uvumi sasa itajulikana kweli stori yenyewe ilikuwaje? maana kwenye uvumi husemwa mengi
 
Nakubaliana kabisa na hiyo assessment. Nataka tu kujua nani alifanya huo utafiti kwa sababu kusema ukweli, mtu wala huhitaji kufanya utafiti rasmi kugundua kuwa sisi Watanzania ni watu wa kuamini amini tu bila mpango.


Mike Tyson story ?lol
 
Mike Tyson story ?lol
halafu magazeti ya GP yakaandika front page bila aibu, nilichefuliwa kweli bcoz it took me 2min to prove the story is fake -_- wakati GP wanadai alitokea kidume wa kumtoa 'bikra' ptuuu. do you remember the 'giant snake in the dead sea' story iliyowekwa JF na ikatokea GP later that week?! i wish ningeweza ku-perform so poorly kazini kwetu kama wahariri wa GP
 
Kiukweli nchi yetu ni ya simple minded people..ndiyo maana hata Maximo alipata taabu kufanya kazi hapa Tz
Imagine mtu anatimuliwa timu ya taifa kwa utovu wa nidhamu uliokithiri, halafu anaenda kupokelewa kama kama shujaa kwenye klabu yake..wonders shall never cease in Tanzania...Halaf jambo lisilo na tija linaweza kuteka headlines za magazeti hadi ushangae...Fikiria tu babu wa Loliondo...Huwa wakati mwingine nasema tuko kama vile 'misukule' flani hivi..(sorry to say this).
 
Habari yenyewe imekaa kiuvumishaji

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ni kweli. Ule uvumi wa Mike Tyson kubadili jinsia ulisambaa Facebook. Ni wabongo tu walikuwa wanaiongelea. Lakini ukipiga search ya hiyo habari kwenye google kulikuwa hakuna habari yoyote kuhusu hiyo ishu zaidi ya gazeti moja tu la Zimbabwe. Hata ukijaribu kuwajulisha watu wanakataa kata kata, eti wanasubiri magazeti ya nyumbani yakanushe.

Ni uvumi, na kupenda umbea pia. Hiyo picha ya kunatana imechukuliwa toka kwenye video ile ya waKenya , si ndio?
 
1. kupenda udaku na kupuuzia mambo ya msingi
2. uwezo mdogo wa kufikiri au kutotaka kushirikisha ubongo
3. fitna
4. roho mbaya
5.......................

..............................###vinatufikisha hapo###
 
Back
Top Bottom