Kumbe tunaongoza kwa uvumi…!

Kumbe tunaongoza kwa uvumi…!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
KANUMBA%2BMAGAZINE.jpg


GAZETI++LA+LEO.bmp


Utafiti uliofanywa hivi karibuni umeitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi ambazo watu wake hupenda sana kuvumisha mambo na yakaonekana kama kweli. Pamoja na kuwa na vyombo vingi vya habari ambavyo vingasaidia kufafanua mambo, utafiti huo unasema, vyombo hivyo, navyo husaidia kuvumisha uongo na ukaonekana kuwa kweli.

Inaelezwa kwamba, wananchi wa Tanzania hawana kawaida ya kuchunguza au kujiuliza kuhusu mambo yanayowazunguka. Kila siku wanaamini wanakutana na jambo jipya hata kama liliwatokea jana na juzi. Ndio maana, matumizi ya wizi wa ulaghai (Utapeli) umekuwa ukifanikiwa sana.

Taarifa zinasema, nchini Tanzania mtu anaweza kuzusha jambo la kijinga na jambo hili likashika kasi na kufikia mahala ambapo hata mamlaka fulani zikaingilia kutaka kufanya utafiti au uchunguzi. Hata hivyo utafiti huo haukutoa mifano ya mambo ambayo yamekuwa yakizushwa hapa nchini na kuonekana kama kweli. Lakini huenda suala la mwanaume na mke wa mtu walionasiana guest wakati wakizini ni kati ya mambo hayo.

Lakini inaelezwa kwamba, huenda sababu ya watu kuwa wambea na wavumishaji ni kutokana na mfumo wa utoaji habari kwa umma kwa siku za nyuma. Magazeti na redio zilizokuwa zinaruhusiwa nchini zilikuwa ni za serikali peke yake. Wananchi walikosa nafasi ya kujua ukweli kuhusu mambo mengi yenye kuwazunguka, kwani mengine yangeweza kuikwaza serikali.

Kwa hiyo wananchi wakawa wanavumisha na kuzua pale jambo fulani dogo linapotokea mahali. Utamaduni huu umeendelea hadi sasa. Magazeti redio na televisheni zinadaiwa kwamba, nazo zimekuwa zikieneza umbea bila zenyewe kujua. Mwandishi anajua habar fulani ni uzushi, lakini kwa sababu anataka kuonekana amefuma habari nzuri, huupamba uvumi hadi unaonekana kama ni kweli.
 
Ingawa nakubaliana na hayo maoni ya kwamba Watanzania wengi hawana kawaida ya kuchunguza au kujiuliza kuhusu mambo yawazungukayo, ila habari hii haijaweka wazi huo utafiti uliofanywa hivi karibuni umefanywa na nani na umefanyikia wapi.
 
Mtambuzi tatizo tumezidi uvivu, si unajua maneno ya vijiweni yanavyoenea haraka.
na leo pia haukupita hapa kijiweni au ndo utakuja jtatu moja kwa moja.

Hiyo foleni iliyopo hapo mjini hapafai..........
Ngoja tu nisubiri J3

BACK TO THE TOPIC:

Uliyoyasema Mamndenyi ni kweli kabisa, haya mambo ya kushinda vijiweni yanazua mengi
 
Last edited by a moderator:
Ingawa nakubaliana na hayo maoni ya kwamba Watanzania wengi hawana kawaida ya kuchunguza au kujiuliza kuhusu mambo yawazungukayo, ila habari hii haijaweka wazi huo utafiti uliofanywa hivi karibuni umefanywa na nani na umefanyikia wapi.
Nyani Ngabu usingeuliza hili swali ningeshangaa sana................LOL
 
Last edited by a moderator:
Kuna ukweli mwingi sana katika hili. Watanzania ni watu wa ajabu sana wanaodanganyika kirahisi sana kwa mambo ambayo kiuhalisia hayapo. Watanzania wanaridhishwa sana na vitu vidogo vidogo visivyokuwa na maana. Kwa mfano habari za babu wa Loliondo, hadi serikali ikasaidia kuchimba ile mizizi, huku mawaziri nao wakiingia katika mkumbo wa watu wanaokwenda kunywa dawa kwa babu.

Hii ni ajabu, badala ya serikali kufanya utafiti ili kujiridhisha kwamba babu anatoa dawa ya ukweli, na yenyewe ikaingia katika mkumbo wa kumsaidia. Mwisho wa siku, waliokunywa ile dawa wanateketea kwa kasi ya kusikitisha. Katika hili, vyombo vya habari pamoja na serikali kwa ujumla vimechangia sana kupotosha ukweli na kuwasababishia wananchi usumbufu usio wa lazima.
 
Mtambuzi na hakuna pa kushinda kwa kuwa viwanda vilikuwa vinawafanya watu busy vimeuzwa, nafasi za kazi ni maalum kwa ajili yao na marafiki zao, mashambani ndo hivyo tena mvua za kusua sua, lazima watu wakae vijiweni na kuanza uzushi.

Hiyo foleni iliyopo hapo mjini hapafai..........
Ngoja tu nisubiri J3

BACK TO THE TOPIC:

Uliyoyasema Mamndenyi ni kweli kabisa, haya mambo ya kushinda vijiweni yanazua mengi
 
Last edited by a moderator:
Sio tu kwamba watu wa Tanzania wamekuwa ni wavivu wa kufikiri bali hata huko kufikiri hawawezi.
Maisha ya wengi yanaongozwa na MAWAZO, kabla ya jambo kuwa FIKRA hutangulia kuwa WAZO kwanza.
 
matambuzi huu uzi nao umekaa kiuvumi-uvumi tu!

embu vuka barabara basi.....................

Kwani hujui uvumi ndio unapendwa sana hapa JF...?

Umeona hali ya barabara ya kuelekea Isimani ilivyo? Naogopa kuvuka nitagongwa na magari....LOL
 
umenikumbusha hizi stori
  1. amina chifupa (RIP) kafufuka
  2. babu wa loliondo
  3. mtoto wa kanumba
  4. utata wa castor semenya
  5. freemason blah blah
  6. popobawa
  7. albino wanaleta utajiri
  8. etc
saa zingine nashangaa waTZ tunashindwaje kung'amua even the simplest of information kama ni ukweli au la.
omba Mungu akunyime kila kitu kasoro umaskini wa akili -_-
 
Back
Top Bottom