Kumbe Sumbawanga pakishamba sana!

Kumbe Sumbawanga pakishamba sana!

bush crazy

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
773
Reaction score
1,087
Nimekuwepo siku mbili, nimepamaliza pote kupafahamu kwa kutumia baiskeli tu!

Ila barabara kutokea tunduma ya ukweli balaa(international)

=======

In late 2000's nilipata kuishi Sumbawanga. Napafahamu kwa kiasi chake. Sijaelewa mtoa mada anapopa-term SBA kuwa ni " pa kishamba", amepafananisha na mahali gani au ametumia vigezo gani.
Binafsi kwa kipindi nilichoishi kule, nilipaona ni mahali pazuri ambako Mji umepangiliwa vizuri, hali ya hewa nzuri, upatikanaji wa vyakula "natural" ni rahisi na wa bei nafuu sana. Halikadhalika maisha ya kule si magumu kulinganisha na Miji mingine.

Sent using Jamii Forums mobile app


Nawapongeza Watumishi wa Ardhi waliofanya kazi Sumbawanga kati ya mwaka 1980 mpaka 2006 kwa kuupanga Mji walipima viwanja maeneo mbalimbali ya Mji kama vile Kristo Mfalme, Kisiwani, Malangali, Hali ya Hewa , Makutano Kizwite, Regional block Jangwani Bangwe na Majengo na Katandala Hongereni sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app

1549951224611.png
1549951739544.png
 
Subiria mapovu mkuu kutoka kwa wenye mkoa wao
 
TANZANIA hii hakuna sehemu ya kijanja wala yakifala kote kunafanana tu..
Ni mjinga peke yake anayedhani kuwa Dar ndio kila kitu maeneo kama msasani bonde la mpunga,mwananyamala kisiwani,kinondoni shamba,tandale kwa tumbo,vingunguti spencon,jangwani n.k huwezi kuyaona mikoani
 
Nimekuwepo siku mbili nimepamaliza pote kupafahamu kwa kutumia baiskeli tu! ila barabara kutokea tunduma ya ukweli balaa(international)

Hata Pinda amehama huko. Yupo Dodoma analima zabibu!!!
 
Miji yote ya Tanzania inafanana isipokuwa Dar Es Salaam pekee. Kuna wazungu walisema, Dar is the richest city in Tz, na kweli nimeamini. Hata hizi piki piki za Boxer zipo huku Dar, Mikoani bado wanatumia mchina. Majumba mazuri yamerundikana Dar. Typical modern houses za mikoani ni ndogo ndogo sana. Dar kuna mansions hatare. Magari ya mikoani ni yale tulikuwaga tunaendesha Dar miaka ya tisini. Dar ni ya kipekee sana ukilinganisha na mikoa mingine iliyobaki.
 
Back
Top Bottom