Kumbe Shamsi Nahodha Mwoga Eee! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe Shamsi Nahodha Mwoga Eee!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, Jul 15, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Na Jabir Idrissa

  WAZIRI Kiongozi wa Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha, ametoa kali. Anasema haoni faida yoyote katika utaratibu wa maswali ya papo kwa papo ndani ya Baraza la Wawakilishi (BLW).

  Kama vile hafahamu kuwa dunia sasa inapita katika zama mpya za teknolojia ya habari na mawasiliano, anathubutu hata kubeza utaratibu wa kila Alhamisi wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika bunge la Jamhuri.

  Nahodha amesema utaratibu huo si mzuri kwa sababu “unaweza kuniingiza katika matatizo makubwa kama ilivyomtokezea waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika suala la Zanzibar kama ni nchi au la.”

  Nahodha, mwanasiasa wa kwanza kijana zaidi kupata kuteuliwa kushika nafasi ya Waziri Kiongozi na ambaye sasa anatajwa kuutamani urais kupitia CCM katika uchaguzi mkuu mwakani, anasema:

  “Baraza la Wawakilishi ni chombo kikubwa na haiwezekani kwangu kukitumia kama chombo kisicho na maadili kwa kusema uongo. Mimi naogopa, (BLW) ni chombo kikubwa sana.”

  Anasema Zanzibar inaongozwa na rais na kwa hivyo haitapendeza kwake, waziri kiongozi, kuzungumza jambo barazani bila ya kushauriana na mkuu wake wa kazi, kwani anaweza kutoa majibu yasiyo sahihi na kwenda kinyume na kiongozi wake.

  Maelezo haya, aliyatoa alipokuwa anafanya majumuisho ya michango ya wajumbe waliojadili makadirio na matumizi ya ofisi yake kwa mwaka wa fedha wa 2009/10.

  Nahodha amekalia kiti cha msaidizi mkuu wa rais wa Zanzibar kwa miaka tisa sasa tangu alipoteuliwa mara ya kwanza Novemba mwaka 2000 baada ya kutangazwa mshindi wa uwakilishi jimbo la Mwera.

  Miaka tisa ni muda mkubwa kwa kiongozi kujifunza. Inapokuwa katika kipindi chote hicho kiongozi amekaa katika nafasi ileile, ndio kabisa anatarajiwa awe mjuzi wa kazi yake na mweledi kwa mfumo wa uongozi na utendaji.

  Ninamaanisha Nahodha si mgeni tena kiuongozi. Na hii ndio tofauti yake kubwa na Mizengo Pinda, ambaye ana chini ya miaka miwili tangu ateuliwe.

  Pinda aliteuliwa Februari mwaka jana pale Rais Jakaya Kikwete alipounda upya baraza la mawaziri baada ya mawaziri wa lile la kwanza la baada ya uchaguzi mkuu wa 2005, kukumbwa na kashfa ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond.

  Lakini pia lazima nieleze hapa, anaposema Pinda amepata matatizo katika utaratibu wa kujibu maswali ya papo kwa papo, Nahodha hasemi ukweli. Natoa sababu mbili.

  Katika suala la Zanzibar ni nchi au la, Pinda alijibu swali kwa kutumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.

  Hakutoa maelezo yale kichwani wala haikuwa hisia zake bali ukweli uliobainishwa katika katiba. Au tumesahau kwamba Pinda alisoma katiba siku ile?

  Sasa iwapo ukweli huo haukumfurahisha Nahodha na mawaziri wenzake katika SMZ; au na wananchi wengine wa Zanzibar, hilo si tatizo la Pinda. Na kama ni tatizo, basi tatizo ni katiba aliyoisoma.

  Sababu ya pili ni uimara wa Pinda katika kujibu anachoulizwa bungeni. Amekuwa akijitahidi na anapoona ameulizwa jambo zito kisera linalohitaji umakini zaidi, husema wazi.

  Mara kadhaa amesema angejua ataulizwa angeingia bungeni na maelezo ya maandishi. Wakati mwingine suala aliloulizwa, huwa linafuatiliwa na viongozi husika.

  Kwa mfano, alipokuwa anajibu kuhusu madai ya walimu nchini kote, wiki mbili zilizopita, Pinda alisema anafahamu kuwa hatua kubwa imepigwa katika kumaliza tatizo hilo na kuomba serikali iachiwe ikamilishe mchakato. Hayo ni maelezo ya kiungwana kwa walimu.

  Kuthibitisha uimara wa Pinda katika kutumia vizuri fursa ya kujieleza kwa niaba ya serikali, tuone kauli ya Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alipokuwa anafunga muda wa nusu saa wa maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu siku hiyohiyo.

  Spika alimsifia kwa namna anavyozidi kudhihirisha umahiri wake katika kujibu kwa ufasaha maswali ya wabunge.

  Kwa kupima, Pinda ameonyesha uwajibikaji wa kiwango cha juu hata kuliko mawaziri wenye uzoefu bungeni kwa namna anavyojibu maswali. Kinyume nao, Pinda amethibitisha kujiamini na kila anaposimama anakuwa anajua hasa kile anachokieleza.

  Inapasa Nahodha afahamu kuwa utaratibu wa maswali ya papo kwa papo kwa kiongozi mkuu wa shughuli za serikali bungeni, unatumika kuuliza maswali ya kisera ambayo ni tofauti na maswali yanayoulizwa katika muda wa kawaida wa kipindi cha maswali na majibu.

  Waziri Kiongozi anapaswa kuwa anajua tofauti ya maswali hayo na kwamba yale ya kila siku asubuhi hujibiwa kwa maandishi baada ya wizara husika na kupewa muda wa kufanya utafiti na kuandaa majibu.

  Kwa kutumia utaratibu wa maswali ya papo kwa papo, serikali inajiweka wazi kwa umma. Inaonyesha ilivyo makini au dhaifu katika kutekeleza majukumu yake na kushughulikia matatizo ya wananchi. Serikali inaonyesha inavyowajibika au inavyozembea.

  Utaratibu huu ni muafaka kwa mazingira ya sasa ambapo serikali imekuwa ikikumbwa na mivutano na tuhuma nyingi za ufisadi, rushwa, uzembe na nidhamu mbovu miongoni mwa watumishi wake.

  Kuna tatizo kubwa SMZ. Serikali inaendeshwa kwa usiri mkubwa; bali inaendeshwa kivarange sana. Utumishi haufuati misingi ya utawala bora wala utawala wa sheria. Kila ofisa anafanya ajuavyo badala ya kufuata sheria, taratibu na kanuni.

  Haishangazi kuona serikali na taasisi zake zinapata huduma kinyume na utaratibu; haishangazi kuona taasisi binafsi zinatumika kama wakala wa serikali na bila ya kuwepo makubaliano yoyote rasmi.

  Inakumbukwa rais Amani Abeid Karume alisaini sheria ya kwanza ya manunuzi ya umma mwaka 2003. Leo anajua fika kuwa inapindwa na manufaa binafsi yanaishia kwa viongozi.

  Leo utakuta kiongozi anamiliki magari mengi nyumbani kwake kama vile ana yadi ya kuuzia magari. Taarifa zinasema baadhi ya magari ni yale yaliyobadilishwa kutoka namba za serikali. Matumizi ya mali za serikali kifisadi ni jambo la kawaida Zanzibar.

  Ndio maana hadi leo mkutano wa Baraza la Wawakilishi unafanyika bila ya kuwepo Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye ndiye mshauri mkuu wa masuala ya kisheria barazani.

  Ni Zanzibar ambako ofisa huendelea kuwa katibu mkuu wa wizara hata kwa miaka mitatu wakati akiwa masomoni nje ya nchi. Siamini Zanzibar haina mtu mwingine wa kushika nafasi hiyo.

  Haishangazi kuona mkuu wa wilaya au mkoa anahamisha ofisa kwa sababu amesema ukweli au amechukua hatua ifaayo kwa tatizo lililotokea.
  Pale hatua aliyochukua ofisa ikitofautiana na mawazo ya DC au RC, basi ni kosa na ofisa anashutumiwa na kuhamishwa.

  Wengi wa wananchi hawashangai kuona serikali inashindwa kugawa nyumba za maendeleo kwa wenye shida kwa sababu tu watakaonufaika zaidi ni wananchi wasiopendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Ndani ya SMZ, kuna tatizo kubwa la watumishi kulishwa na kuaminishwa siasa, huku wakikiuka misingi ya kazi zao.

  Haishangazi siasa kuingizwa katika kila jambo hata lile lisilo la kisiasa; bali suala dogo tu linalostahili kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma.

  Nahodha aseme tu kwamba labda pamoja na kukalia uwaziri kiongozi kwa miaka tisa, hajafanikiwa kujenga ujasiri kikazi. Anaogopa.

  Labda aseme kwamba anayoyashuhudia serikalini, na hususan katika ngazi ya juu ya uongozi kama yake, yanakinzana na matarajio yake na yale ya wananchi.

  Ukweli ni kwamba wananchi wa Zanzibar wanahitaji sana utaratibu wa maswali ya papo kwa papo barazani. Yapo maswali mengi yanakosa majibu hata kupitia maswali yanayoandaliwa majibu kwa muda mrefu.

  Mawaziri wa SMZ wameonyesha uwezo mdogo kujibu maswali, isipokuwa ni mabingwa wa kubabaisha kwa kutoa majibu ya kisiasa zaidi kuliko kuzingatia hali halisi ya jambo.

  Utasikia mawaziri wanasema, “naomba hili nitamjibu kwa maandishi.” Haya ni majibu ya kizembe yanayoonyesha mawaziri hawafuatilii shughuli zinazofikishwa maofisini mwao, iwe kutoka ndani au nje ya wizara.

  Ajabu, waziri hutumia dakika tano kuzungumza, lakini ukitafakari alichokisema, unabaini ameshindwa kujibu swali aliloulizwa.

  Kwa hakika, Baraza la Wawakilishi linahitaji sana leo utaratibu wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Kiongozi, kuliko wakato wowote huko nyuma. Yapo matatizo mengi yanayotaka hatua makini na kwa wakati.

  Hivi kwa nini Nahodha ametoa majibu yasiyo na mwelekeo kuhusu msimamo wa serikali katika suala la utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia wakati anajua baraza limetoa maazimio ya kutekelezwa katika mkutano uliopita?

  Hivi kwa nini serikali imeshindwa kueleza kwa ufasaha, itafanya nini katika suala la kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi, kuwa sharti la mtu kuandikishwa kuwa mpiga kura wakati sharti hilo linalohimizwa na sheria halitambuliki katika katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984?

  Huu ni umangimeza tu wa viongozi wa SMZ na CCM wa kuamini kuwa ni lazima kukwamisha wananchi kuingia kwenye daftari la kudumu la wapiga kura (DKWK) kwani wana uhakika wameshindwa uchaguzi hata kabla ya kupiga kura.

  Na bado wanataka watu waamini serikali ina nia njema ya kuendesha uchaguzi huru na wa haki mwakani (!) Uongo mtupu.

  Nampenda Nahodha, kama kijana mwenzangu, bali tu pale anapojali maslahi ya nchi yake. Lazima awe muwazi na muungwana. Kama anaona mambo ni magumu, aachie ngazi ili kuepuka lawama mwishoni.

  Iwapo kila akipima tangu alipoteuliwa anaona hajafanya la maana na hajapata ujasiri, basi ni uungwana kusema, “Ndugu zangu, nimeshindwa.”

  Na ni vizuri Nahodha akasema hivyo sasa kuliko kusubiri lala salama. Lakini wa kufanya hivyo ni kiongozi muadilifu anayejali nafasi aliyopewa kuwa ni ya umma na si yake binafsi.

  Mbinafsi, licha ya kushindwa kazi, ataendelea kujigamba mbele ya watu na kuwadadisi, “Jamani, kwani mie ndo sifai kuwa rais?” Inataka moyo.

  SOURCE: MWANAHALISI.
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  wenyewe hawataki muungano

  get over it
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Na sasa hawataki kabisa mafuta na gas viwe vya muungano, walitaka bendera yao, wanataka mahakama ya kadhi, wataka tujiunge na OIC nchi yote na si waislam tu... Kwa kifupi wanataka mapinduzi ya Pili ""Second Zanzibar Revolution"" na ikiwezekana Revolution without Pemba!!! So tuwe na serikali nne ya Tanganyika, Ya mungano, Ya Zanzibar, ya Pemba!!!! Lakini mkulu yuko kimya sana na mambo mengi, eti ni kweli kimya means ndiyo???
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Nahodha 'eshi kunichekesha...
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Shida sio madini,wanataka kujitenga!!Bendera wamepewa sisi tanganyika hatuna,wimbo wanao sisi tanganyika hatuna,wanataka kujiunga EAC kivyao sisi tanganyika hatujadai,wanataka chama cha cha mpira wajitegemee sisi hatujadai,wanataka serikali kibao zisizo na msingi wowote.Wanataka kutulazimisha watanganyika tujiunge OIC na mihakama ya kadhi na ndio lengo kuu hatutaki labda kwa kuwa rais ni muislamu.
  Ngoja tusubili tuone..........
   
 6. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Nawashangaa ndugu zangu wa zanzibar kumchukua Shamsi Nahodha akajadili kero za Muungano na Mizengo Pinda katika meza moja, wakati anasema wazi kuwa hana uwezo na umakini wa kujenga na kutetea hoja za papo kwa papo. Atawezaje huyu kusimama na Pinda aliyejubiri wazi wazi kukubali maswali ya papo kwa papo?
  Huu ndo uwezo wa kufikiri wa Waziri kiongozi wa SMZ ambaye malaki ya wananchi wa zanzibar wanamtegemea kusimama kutetea maslahi ya wananchi. Dunia ya sasa kukosa kiongozi asiyejiamini kufanya maamuzi magumu na kuyatetea ni khasara kubwa kwa taifa ni afadhali Bw. Nahodha amalizie muda wake atupishe. Na tusimsikia kutaka kugombea urais maana uwaziri hauwezi ataweza urais!!!
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Iwapo CCM -Zenj watamsimamisha Nahodha 2010, basi watakuwa wamechemka big time...
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Jul 15, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Nilikuwa sijawahi kufikiri kwamba Zenj kuna ufisadi. Kumbe nao wanatafuna kimya kimya!
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Jul 15, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Siasa wanasema SI-HASA. Unaweza ukaingia kwenye si-hasa ukadhani utafanya vizuri ukajikuta umechemsha hata kuliko Nahodha. Kumbuka kwenye si-hasa unaserve interest za waliokuweka, kumbuka mlamgo uliingilia na huohuo unaweza kutoka. So, Nahodha knows exactly what he is doing!
   
 10. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Vipi wewe umevuta nini- naona hueleweki? (kumradhi)
   
 11. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tutakuona ukiingia wewe- Inshalla. Lakini kuwa na heshima na insaafu kwa huyo Nahodha. Ni Kiongozi wetu na ni Waziri Kiongozi.
   
 12. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #12
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nyinyi Wazanzibari mna uwezo -sasa msishushane hadhi-uwezo mnao
   
 13. BUSARA6

  BUSARA6 JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2009
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 340
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Na nia mnayo!
   
 14. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nafikiri ipo kwa wengi wa Wa-Zanzibari hawapingi Muungano huu tulionao.
   
 15. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #15
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Are you still on medication?kama wengi wa-zanzibar hawapingi Mungano huu tulionao ,sasa hivyo vilio vya nini vya mafuta ,mapato ya kodi etc ,Viongozi wa Tanganyika nawaunga mkono kwa kauli zao ,wamekuwa wakiiendesha serekali ya zanzibar kwa hali na mali na kulitaka kulijuwa hilo mfano mdogo mwezi huu wamepeleka ndugu zao (POLISI na MAJESHI wanafatia) kule pemba kuhakikisha SMZ wanaendelea kuwa madarakini halafu leo mumekuwa mnatowa madai haya na yele, nafikiri ni wakati muafaka kwa chama kuanza kuzikushanya hizo kadi za kijani kama walivyofanya B4
   
 16. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #16
  Jul 16, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Nilikuwa nishaanza kupona ule ugonjwa wa kutoweza kushangaa...!

  Nahisi kama unanirudia tena...! Mwe!
   
 17. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #17
  Jul 16, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mwenzako nakula "tizi" kweli kweli, nikiingia hapo 2015 (wakati huo BLW litakuwa Chukwani kule na vichwa vitupu vinavyo think zanzibar and zanzibaris only and nothing else, vitakuwa humo).Pakacha, namheshimu Maalim Shamsi Nahodha hasa alipokuwa akitupa "matirio" pale Idara ya Habari Maelezo(stz), lakini suala la uongozi ni ishu nyengine kabisa.

  Hayo kayasema mwenyewe Nahodha au hukumsikia?

  Na uwezo upo
   
Loading...