Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 13,061
- 11,668
Rais sio mtumishi wa umma ( Civil servant). Makamu wa Rais nae sio mtumishi wa umma. Mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya sio watumishi wa umma vilevile. Hawa ni viongozi wa kisiasa na wanawakilisha vyama vyao au chama kilichomweka pale. Katibu Mkuu na watendaji wengine serikalini ni watumishi wa umma na wanaongozwa na Waraka wa Watumishi wa Umma ambao unawataka wasifungamane na chama chochote. Ndio maana Waziri anaweza kushabikia chama chake bila tatizo lolote lakini Katibu Mkuu haruhusiwi kufanya hivyo. Ndio maana huwezi kumuona Kijazi kwenye vikao vya CCM hata kama ana kadi. Kama Msemaji wa Ikulu ni mtumishi wa umma nae hatakiwi kuonyesha waziwazi mapenzi yake kwa chama cha Rais wake. Lakini kama sio, basi kuvaa kijani ruksa.Kwani rais nae si analipwa mshahara na kodi za wananchi? mbona ana Chama?
Amandla....