Mihimiri ya CCM imenyauka
Hizi ni Siku za mwisho za utawala wao Haramu
Ubabe umeshindwa
Wizi umeshindwa
Uongo umeshindwa
Hongo ya Fedha imeshindwa mbaya kabisa
Akili na Roho zao pia zimeshindwa
Wamebaki na magari ya fahari,mashati ya kijani na matusi midomoni.
POLICE FFU na UWT ninyi mnatumiwa kama vijiko vya chipsi, nasema ole wenu hasa ninyi wakuu wenye madoa mabegani.
Ushindi wa CDM Arumeru si ushindi wa wana Arumeru tu bali ni ushindi wa Wanyonge wote nchini Tanzania
Ushindi wa CDM Arumeru ni ukurasa mpya katika mapambano ya kuiondoa CCM madarakani.
Ushindi wa CDM Arumeru ni Tunu ya UTU kwa wazalendo wote Tanzania
Ushindi wa CDM Arumeru ni Nguvu mpya ya kuchochea mapambano ya kuondoa unyonge na aibu Tanzania
Ushindi wa CDM Arumeru ni pigo kwa CCM na vibaraka wake wa nje na ndani wafanyao Tanzania shamba la BIBI
Ushindi wa CDM Arumeru ni Pigo la moyo kwa Edward Lowassa na wapambe wake
Ushindi wa CDM Arumeru ni Jibu sahihi la majibu ya dharau na matusi yote ya nguoni toka kwa Makomredi wa CCM
Ushindi wa CDM Arumeru ni sababu tosha ya kila mpigania Haki,heshima,Usawa na Maendelea Tanzania kujaa Ari na nguvu mpya
Ushindi wa CDM Arumeru ni ni fundisho kwa CCM kwamba Ubaya haulipi na wema ni Tuzo ya dhahabu.
ALUTYE PE NDI NYWAA UWULASI :first: mapambano bado yanaendelea
Vox Populi Vox Dei Regnat Populus - SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU ACHA WENGI WATAWALE.