Kumbe Kweli Mapenzi Yanaumiza

Kumbe Kweli Mapenzi Yanaumiza

Darmian

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2017
Posts
17,311
Reaction score
46,810
Aisee nilikuwa nawashangaa wale ambao wanalia kuhusu mapenzi,wale ambao wameachwa,au wametendwa in one way or another..Nikawa najisemea ni ujinga kuumia au kulia lia kisa kuachwa au kutendwa,au kupoteza uhusiano na mtu umpendaye kwa sababu mbalimbali..

Kumbe bhana haya mambo yanatokea tu automatically unajikuta upo kwenye hali hiyo..

Kuna mtoto mmoja mzuri ambaye kimsingi alinivutia,so nikamtokea na kwa kiasi fulani nikamwin..mazingira niliyompata na tuliyoendelea kuwa nayo hayakunipa nafasi ya kuwajua ndugu au rafiki zake kiundani..

Sasa bhana from nowhere mtoto akawa hapatikani kwenye simu,miezi ikapita,mwaka n.k

Jana from nowhere nikakutana na mtu ambaye ambaye alinitambulisha kuwa ni rafiki yake,so ikabidi nimgusie kuhusu huyu mtoto,akanipa no zake ambazo anapatikana

Usiku nikamcheki nini,na ikabidi nimuulize what went wrong??,akawa kama tu anajiuma uma hivi..mwishoni akaniambia yupo kwenye serious relationship for the meantime kwahiyo hatuwezi kurenew uhusiano wetu..Daah niliumia kinoma

Nahisi pia nimeumia kwa sababu kwanza huyu mtoto alikuwa na vigezo vyote vya mtu nimtakaye..wanawake wako wengi lakini ni kazi kumpata yule unaye-mpicture kwenye akili yako japo hata kwa asilimia 65 tu..

Anyway ndo maisha..siku nzima akili haipo sawa,hadi saivi 00:57 nipo macho,I can't believe that..Kwa swala hili ambalo kwa wengine linaweza kuwa la kawaida ila kwangu mimi limenipa wakati mgumu..

Lets call it LOVE
 
Pole mkuu, jitahidi ulale sasa.
Ila wewe umeumiaje na wakati mliachana mwaka mzima bila mawasiliano??Au ni wivu , hahahahah[Nimekutania]
 
Pole mwaya, kwanza uzi huu utakupa nafuu ya kumsahau.

Kama usingizi hauji weka aviation fuel kwenye kilauri upunguze tafakuri kesho nayo ni siku.

Laah kama waishi mwenyewee nenda sebleni washa mziki unaoupenda cheza walau masaa 2 au 1 bila kupumzika kisha kaoge utalala usingizi mzitoo ukiamka asubuhi machungu yote ya Mahaba kwishney.

Shukuru Mungu amekwambia ukweli maana angekudanganya akuchote hisia ale viepe na pizza zako kisha akusapraisi naolewa jumamosi hii, hapo ndo ungekufa kihoro.

K’ Matata.
 
Mimi mwenyewe ndo najiuliza hapa ni wivu naona kuna mwamba anamu-hold down huyo mtoto au nini??
 
Pole mwaya, kwanza uzi huu utakupa nafuu ya kumsahau.

Kama usingizi hauji weka aviation fuel kwenye kilauri upunguze tafakuri kesho nayo ni siku.

Laah kama waishi mwenyewee nenda sebleni washa mziki unaoupenda cheza walau masaa 2 au 1 bila kupumzika kisha kaoge utalala usingizi mzitoo ukiamka asubuhi machungu yote ya Mahaba kwishney.

Shukuru Mungu amekwambia ukweli maana angekudanganya akuchote hisia ale viepe na pizza zako kisha akusapraisi naolewa jumamosi hii, hapo ndo ungekufa kihoro.

K’ Matata.
Nice advice..
 
Mapenzi hayana baunsa ukiona mwanaume anajitutumua humu kuwa hawezi kubembeleza mwanamke au hawezi kulilia papuchi moja kisa zipo nyingi basi ujue huyo hajawahi kupenda halafu kinachonishangaza wanaume wa siku hizi hawana mapenzi kwa wanawake zao ila wanataka wanawake zao wawe na utii kwao hata maandiko yanasema mwanaume ampende mkewe na mwanamke amtii mumewe

Sasa unakuta mwanaume hampendi mkewe au mpenzi wake ila anataka huyo mkewe au mpenzi wake amtii yaani dunia imebadilika sana siku hizi wanaume wengi wamekuwa wakatili kwa jina la tamaduni za kiafrika na ndo hawa tunaowasikia na kauli zao hizi za "tunapiga na kusepa" au "tunazalisha na kuacha" yaani imefikia hatua badala ya kutafuta suluhisho la kupunguza maovu tunatafuta mshindi nani kati ya mwanaume au mwanamke ajabu sana
 
Ni kweli usemayo lakini ukumbuke nyinyi ndiyo mnasababisha tuwe hivi. Wanaume tunapenda mara moja na tukishaumizwa kwenye hiyo mara mmoja ni mwendo wa kula na kusepa.
Na tukipenda huwa tunakuwa kama ndege aliyemwagiwa maji na nyinyi ndiyo mnaona kama fursa ya kutupanda vichwani.
 
Pole mwaya, kwanza uzi huu utakupa nafuu ya kumsahau.

Kama usingizi hauji weka aviation fuel kwenye kilauri upunguze tafakuri kesho nayo ni siku.

Laah kama waishi mwenyewee nenda sebleni washa mziki unaoupenda cheza walau masaa 2 au 1 bila kupumzika kisha kaoge utalala usingizi mzitoo ukiamka asubuhi machungu yote ya Mahaba kwishney.

Shukuru Mungu amekwambia ukweli maana angekudanganya akuchote hisia ale viepe na pizza zako kisha akusapraisi naolewa jumamosi hii, hapo ndo ungekufa kihoro.

K’ Matata.
Aweke ngoma ya Big Sean - I dont *** with you 😂😂😂 kwa replay.

Nzuri sana kwa kuondolea machungu.
 
Back
Top Bottom