Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,673
- 11,342
Mkuu huruhusiwi kujiita Engineer kama hujasajiliwa na Engineers Registration Board (ERB) na ni ILLEGAL
ndio maan nimesema, we have silly people who clame to know at their ignorance.
hapa tatizo nimegundua ni kiingereza ndio kinakusumbua maana hujaelewa chochote kwenye maandishi haya.
nilikuwa na haki kusema umejaa ujinga unaovuka kiwango cha mbwia unga aka teja.
hakuna mahali popote palipoandikwa kuwa hupaswi kujiita injia kabla hujasaliwa na hakuna kipengele hicho na Hakijawahi kuwepo katika taifa lolote duniani.
kwa nini nisikuite una kiwango cha kutosha cha ujinga.
eti nisimtukane mtu nisiyemjua, sihitaji kukujua maadamu nilishajua ujinga wako ndio tatizo.
haya maelezo yote yanaeleza mashariti ya kufanya kazi za kiinjinia kuwa ni sharti uwe imesajiliwa na board.
hili nilikuwa najua miaka yote na ukirejea majibu yangu nimetoa humuhumu nikawaambia injinia ni mtu yeyote aliyehitimu masomo ya uhandisi iwe kwa ngazi ya certificate,diploma ama degree na zaidi.
katafute ushahidi mwingine.
narudia tena hakuna sharti linalosema mtu hawezi kuitwa engineer mpaka asajiliwe.
na kama hutakuwa umeelewa majibu haya. nitatoa tafsiri ya sheria hii kwa lugha ya kiswahili ili uelewe na uzuri humu wapo watu wengi wenye uelewa maana tatizo kwako ni kimombo kilipita pembeni
Mkuu huruhusiwi kujiita Engineer kama hujasajiliwa na Engineers Registration Board (ERB) na ni ILLEGAL
Alienda kenya baada ya kufukuzwa kama sijasahau
una uhakika na ulichokiandika au unaropoka tu?
Hivi wakati anasoma civil ilikuwa ni miaka mingapi,coz kwenye part ya EDUCATION naona ameanza UDSM mwaka 1987 mpaka 1992,alafu NOT COMPLETED,pananichanganya sana hapa
Hivi wakati anasoma civil ilikuwa ni miaka mingapi,coz kwenye part ya EDUCATION naona ameanza UDSM mwaka 1987 mpaka 1992,alafu NOT COMPLETED,pananichanganya sana hapa
Uongo! Hakuwahi kuwa balozi katika nchi yoyote.Mbatia alikuwa mmoja wapo wa wanafunzi wengi wa Engineering waliofukuzwa pale UD wakati wa ule mgomo mwinyi aliosema "wamenitukana matusi ya nguoni". Alikuwa anasomea Civil Engineering hapa UD, alifukuzwa kuingia mwaka wa tatu.
Mbatia alikuwa ni mpiganaji wa kutetea maslahi ya watu kwa muda mrefu sana, japo alikulia katika familia iliyofaidika sana na dola. Baba yake nadhani alikuwa Balozi wa Tanzania katika nchi fulani za Ulaya wakati kina Mbatia wanakua.
Kwa sheria za Tanzania jina lako litaanza na Eng. kama utakuwa umesajiriwa na ERB. Kama kuna mtu yeyote humu amesajiiwa na ERB atakubaliana nami kwenye barua ya usajili unaambiwa kuanzia sasa jina lako litaanzia Eng.
hebu iweke hapa hiyo sheria titoe tafsiri yake.
maana navyojua mimi ni kwamba hiyo sheria inakulazimisha kutumia initial ya Eng hata kama hutaki lakini haimaanishi kuwa kwa kufanya hivyo ndio umepewa iinjia. hii ni kama condition ama terms katika mainjinia waliosajiliwa. ni sawa na sheria inayotaka madereva na makondakta kuvaa sare. haimaanishi kuwa hizo sare ndio udereva ama ukondakta. ama mainjinia kuvaa uniform za kiinjinia ,its just a principle. na ukitaka kujua. HAKUNA PEROMOTION WALA AWARD AMA CHETI KINACHOTOLEWA KUWA SASA WEWE NI INJINIA. mathalani ukiangalia wakili ni tofauti na uwakili si tu kusoma sheria. na hata ujaji si tu kusoma sheria na ndio watu wanakuwa awarded ujaji ama uwakili. lakini unasheria mtu akimaliza law tu tayari ni mwanasheria iwe amejisajili TLS ama laa.
mbona umejibu kitu ambacho sijataka? usifikirie mimi ni ignorant kwenye engineering field ndio maana kuna watu nimewaambia kitu walichosema hakipo , wakaleta ushahidi mwisho wakaabika na hawarudi tena humu maana waliongea wasiyoyaelewa.Ndugu yangu kuna cheti kinatolewa kwanza kuna Graduate Engineer baada ya hapo unatakiwa uproduce engineering report ambayo umepractice engineering work under supervision ya Professional engineer. Bodi inakaa inapitia then wanakupa Cheti kikiwa na picha yako wanatoa na leseni ambayo ina dumu kwa miaka mitatu unatakiwa urenew
kwenye uhandisi kuna tofauti kidogo.Udakitari wa tiba ya binaadamu ni profession ya zamani duniani na Tanzania. Unapotunukiwa degree yako e.g. MD unatambuliwa kama dakitari lakini kwa nchi nyingi duniani huruhusiwi ku-practice kama dakitari, inabidi ufanye na kutimiza mahitaji ya internship. Baada ya hapo Baraza la Madakitari la Tanganyika ndio wanaweza kuku register na hiyo inakupata uwezo kisheria ku-practice independently kazi ya udakitari. Kwa hiyo ukipata degree yako unaweza kujiita Dr. XYZ but ili upactice lazima uwe na registration. Ukiboronga wanaweza kukufutia usajili na ukapoteza haki ya kupractice lakini bado ni dakitari labda chuo ulichohitimu wakunyang'anye degree yako.
Sidhani kama mfumo wa ERB ni tofauti. Cheti chako kinakufanya uwe engineer lakini huwezi kupractice TZ bila kuwa registered. Hiyo ya kuitwa Eng. XYZ inaelekea ni utashi ERB lakini haimuondolei ambaye hana ERB registration hadhi ya kuwa engineer.