Kumbe James Mbatia ni Civil Engineer?

Kumbe James Mbatia ni Civil Engineer?

Mkuu huruhusiwi kujiita Engineer kama hujasajiliwa na Engineers Registration Board (ERB) na ni ILLEGAL

Hiyo ya ERB ni kuweka tu utaratibu ili kuwa na watu ambao wame-practice na kusajiri kazi zao mbalimbali ili once atakapofanya kazi yoyote aweze kutambulika kwa kuwa tayari mamlaka zinazohusika zimeshamtambua lakini kwa akili ya kawaida kwa tafsiri tu ya Engineer ni mtu yoyote aliemaliza masomo ya uhandisi katika ngazi ya shahada na anafanya kazi ziendanazo na hiyo kozi aliyosomea.

An engineer is a professional practitioner of engineering, concerned with applying scientific knowledge, mathematics, and ingenuity to develop solutions for technical, societal and commercial problems. Engineers design materials, structures, and systems while considering the limitations imposed by practicality, regulation, safety, and cost

Mwenye Degree - Engineer / Mhandisi

Diploma au FTC - Technician / Fundi Mchundo

VETA - Fundi Sanifu
 
ndio maan nimesema, we have silly people who clame to know at their ignorance.

hapa tatizo nimegundua ni kiingereza ndio kinakusumbua maana hujaelewa chochote kwenye maandishi haya.

nilikuwa na haki kusema umejaa ujinga unaovuka kiwango cha mbwia unga aka teja.

hakuna mahali popote palipoandikwa kuwa hupaswi kujiita injia kabla hujasaliwa na hakuna kipengele hicho na Hakijawahi kuwepo katika taifa lolote duniani.

kwa nini nisikuite una kiwango cha kutosha cha ujinga.

eti nisimtukane mtu nisiyemjua, sihitaji kukujua maadamu nilishajua ujinga wako ndio tatizo.

haya maelezo yote yanaeleza mashariti ya kufanya kazi za kiinjinia kuwa ni sharti uwe imesajiliwa na board.

hili nilikuwa najua miaka yote na ukirejea majibu yangu nimetoa humuhumu nikawaambia injinia ni mtu yeyote aliyehitimu masomo ya uhandisi iwe kwa ngazi ya certificate,diploma ama degree na zaidi.

katafute ushahidi mwingine.

narudia tena hakuna sharti linalosema mtu hawezi kuitwa engineer mpaka asajiliwe.

na kama hutakuwa umeelewa majibu haya. nitatoa tafsiri ya sheria hii kwa lugha ya kiswahili ili uelewe na uzuri humu wapo watu wengi wenye uelewa maana tatizo kwako ni kimombo kilipita pembeni

Mkuu mpe za uso huyo, mbona hawahoji mkulu wao kupewa Uprofesee?
hahaaaaaa
 
Alienda kenya baada ya kufukuzwa kama sijasahau

Mbatia alikuwa mmoja wapo wa wanafunzi wengi wa Engineering waliofukuzwa pale UD wakati wa ule mgomo mwinyi aliosema "wamenitukana matusi ya nguoni". Alikuwa anasomea Civil Engineering hapa UD, alifukuzwa kuingia mwaka wa tatu.

Mbatia alikuwa ni mpiganaji wa kutetea maslahi ya watu kwa muda mrefu sana, japo alikulia katika familia iliyofaidika sana na dola. Baba yake nadhani alikuwa Balozi wa Tanzania katika nchi fulani za Ulaya wakati kina Mbatia wanakua.
 
una uhakika na ulichokiandika au unaropoka tu?

Hawa ndio regisrered engineers by ERB! Yaani nikiwa na degree yangu ya mech engineer toka majuu/Ujerumani inabidi hata wajerumani wasiniite engineer mpaka ERB ikubali kuwa niko registered! Hayo makubwa kwa nchi yetu!
 
Rasimu ya chenge mnayoipigia debe kuwa ikipita kwa kura za ndio itakuwa ni katiba nzuri kupita katiba zote duniani inasema mbunge anahitaji tu kujua kusoma na kuandika. Mbati anapita vigezo vyote hivyo kwa mbali sana
 
So what??
small minds Discuss people!
Ngoja nipite mie. Hakuna maarifa humu, nisije kudumua akili.
 
Hivi wakati anasoma civil ilikuwa ni miaka mingapi,coz kwenye part ya EDUCATION naona ameanza UDSM mwaka 1987 mpaka 1992,alafu NOT COMPLETED,pananichanganya sana hapa
 
Hivi wakati anasoma civil ilikuwa ni miaka mingapi,coz kwenye part ya EDUCATION naona ameanza UDSM mwaka 1987 mpaka 1992,alafu NOT COMPLETED,pananichanganya sana hapa

Ukiongeza na migomo maana those days Chuo Kikuu ilikuwa chuo kikuu kweli yaani kama kuna issue itatokea lazima itatingisha nchi na mijimaa ilikuwa inagoma hasa kiasi kwamba watu wanarudishwa mpaka kijijini kwao. (inawezekana walikaa nyumbani muda mwingi wakisubiri hatima yao)
 
Kwa sheria za Tanzania jina lako litaanza na Eng. kama utakuwa umesajiriwa na ERB. Kama kuna mtu yeyote humu amesajiiwa na ERB atakubaliana nami kwenye barua ya usajili unaambiwa kuanzia sasa jina lako litaanzia Eng.
 
Hivi wakati anasoma civil ilikuwa ni miaka mingapi,coz kwenye part ya EDUCATION naona ameanza UDSM mwaka 1987 mpaka 1992,alafu NOT COMPLETED,pananichanganya sana hapa

engineering course ni miaka minne.
1987/1988=first year.
1988/1989=second year.
1989/1990=third year.
1990/1991=fourth year.

kutakuwa na jambo lilitokea na mwenye taarifa anaweza kutoa.

japo najua mwaka 1990 kama sikosei kuna mgomo uliosababisha mpa wanafunzi mwaka wa kwanza wasiende kabisa chuo na ilibidi wasubiri mwaka uliofuata.

sijafahamu kama mgomo huu uliathiri mpaka continuing students. na ninashawishika kuamini huu mgomo ndio ulikuwa sababu maana haiwezekani ulisababisha mpaka waliomaliza form six wasianze chuo mwaka ule alafu wahusika wa mgomo kwa maana waliokuwa chuo tayari wabaki salama na kuendelea na masomo kama kawaida.
 
Mbatia alikuwa mmoja wapo wa wanafunzi wengi wa Engineering waliofukuzwa pale UD wakati wa ule mgomo mwinyi aliosema "wamenitukana matusi ya nguoni". Alikuwa anasomea Civil Engineering hapa UD, alifukuzwa kuingia mwaka wa tatu.

Mbatia alikuwa ni mpiganaji wa kutetea maslahi ya watu kwa muda mrefu sana, japo alikulia katika familia iliyofaidika sana na dola. Baba yake nadhani alikuwa Balozi wa Tanzania katika nchi fulani za Ulaya wakati kina Mbatia wanakua.
Uongo! Hakuwahi kuwa balozi katika nchi yoyote.
 
Kwa sheria za Tanzania jina lako litaanza na Eng. kama utakuwa umesajiriwa na ERB. Kama kuna mtu yeyote humu amesajiiwa na ERB atakubaliana nami kwenye barua ya usajili unaambiwa kuanzia sasa jina lako litaanzia Eng.

hebu iweke hapa hiyo sheria titoe tafsiri yake.

maana navyojua mimi ni kwamba hiyo sheria inakulazimisha kutumia initial ya Eng hata kama hutaki lakini haimaanishi kuwa kwa kufanya hivyo ndio umepewa iinjia. hii ni kama condition ama terms katika mainjinia waliosajiliwa. ni sawa na sheria inayotaka madereva na makondakta kuvaa sare. haimaanishi kuwa hizo sare ndio udereva ama ukondakta. ama mainjinia kuvaa uniform za kiinjinia ,its just a principle. na ukitaka kujua. HAKUNA PEROMOTION WALA AWARD AMA CHETI KINACHOTOLEWA KUWA SASA WEWE NI INJINIA. mathalani ukiangalia wakili ni tofauti na uwakili si tu kusoma sheria. na hata ujaji si tu kusoma sheria na ndio watu wanakuwa awarded ujaji ama uwakili. lakini unasheria mtu akimaliza law tu tayari ni mwanasheria iwe amejisajili TLS ama laa.
 
Ndugu yangu kuna cheti kinatolewa kwanza kuna Graduate Engineer baada ya hapo unatakiwa uproduce engineering report ambayo umepractice engineering work under supervision ya Professional engineer. Bodi inakaa inapitia then wanakupa Cheti kikiwa na picha yako wanatoa na leseni ambayo ina dumu kwa miaka mitatu unatakiwa urenew
 
Udakitari wa tiba ya binaadamu ni profession ya zamani duniani na Tanzania. Unapotunukiwa degree yako e.g. MD unatambuliwa kama dakitari lakini kwa nchi nyingi duniani huruhusiwi ku-practice kama dakitari, inabidi ufanye na kutimiza mahitaji ya internship. Baada ya hapo Baraza la Madakitari la Tanganyika ndio wanaweza kuku register na hiyo inakupata uwezo kisheria ku-practice independently kazi ya udakitari. Kwa hiyo ukipata degree yako unaweza kujiita Dr. XYZ but ili upactice lazima uwe na registration. Ukiboronga wanaweza kukufutia usajili na ukapoteza haki ya kupractice lakini bado ni dakitari labda chuo ulichohitimu wakunyang'anye degree yako.

Sidhani kama mfumo wa ERB ni tofauti. Cheti chako kinakufanya uwe engineer lakini huwezi kupractice TZ bila kuwa registered. Hiyo ya kuitwa Eng. XYZ inaelekea ni utashi ERB lakini haimuondolei ambaye hana ERB registration hadhi ya kuwa engineer.
 
Hata fundi vibatari ni Engineer.Tatizo la hawa wanaojiona ma engineer huku jf ni kuulewa kiingereza,ndo walewale wa my daily bread is engineering.
 
Ila uprofesa na udaktari wa kichina wa kikwete na mary nagu ndo halali?
 
Ndugu yangu kuna cheti kinatolewa kwanza kuna Graduate Engineer baada ya hapo unatakiwa uproduce engineering report ambayo umepractice engineering work under supervision ya Professional engineer. Bodi inakaa inapitia then wanakupa Cheti kikiwa na picha yako wanatoa na leseni ambayo ina dumu kwa miaka mitatu unatakiwa urenew
mbona umejibu kitu ambacho sijataka? usifikirie mimi ni ignorant kwenye engineering field ndio maana kuna watu nimewaambia kitu walichosema hakipo , wakaleta ushahidi mwisho wakaabika na hawarudi tena humu maana waliongea wasiyoyaelewa.

kifupi natambua kuna cheti kinatolewa na ERB lakini yale maelezo niliyokuwa najibu ni hoja ya jina kuanza na Eng. kitu ambacho si tatizo kwangu ila hoja yangu ni kwamba neno Eng siyo kigezo cha wewe kuitwa engineer wala hicho cheti siyo kigezo cha wewe kuitwa engineer ndio maana nikataka niwekewe hapa hiyo sheria. ENGINEER NI YULE ALIYESOMA NA KUFAULU MASOMO YA ENGINEERING

LABDA HATA KABLA HUJAILETA HIYO SHERIA NATAKA NIKWAMBIE.

HAKUNA SEHEMU YOYOTE DUNIANI AMBAPO KUNA SHERIA INAYOSEMA ENGINEER NI YULE TU MWENYE CHETI KUTOKA TAASISI YA USIMAMIZI WA WAHANDISI KINACHOMRUHUSU KUFANYA KAZI ZA KI-ENGINEER AMA YULE TU AMBAYE JINA LAKE LINAANZA NA ENG.

labda hapa utanielewa.

kama unabishaleta hapa hiyo sheria.

vinginevyo tukubaliane kuwa TAASISI ZOTE ZA USAJILI WA WAHANDISI KOTE DUNIANI HAZINA LENGO LA KUFANYA MTU AITWE INJINIA BALI LENGO LAKE NIKUSIMAMIA KAZI ZA MAINJIA WALIOSAJILIWA NA KUTAMBULIKA.

na hawa ndio wanaruhusiwa kusaini nyaraka,kupewa kandarasi nk lakini katika field kwa maana ya kazi wanafanya wote hata wasio na usajili wa ERB ila wakiharibu yule aliyesaini ambaye kasajiliwa ndio atakuwa answerable.
 
Udakitari wa tiba ya binaadamu ni profession ya zamani duniani na Tanzania. Unapotunukiwa degree yako e.g. MD unatambuliwa kama dakitari lakini kwa nchi nyingi duniani huruhusiwi ku-practice kama dakitari, inabidi ufanye na kutimiza mahitaji ya internship. Baada ya hapo Baraza la Madakitari la Tanganyika ndio wanaweza kuku register na hiyo inakupata uwezo kisheria ku-practice independently kazi ya udakitari. Kwa hiyo ukipata degree yako unaweza kujiita Dr. XYZ but ili upactice lazima uwe na registration. Ukiboronga wanaweza kukufutia usajili na ukapoteza haki ya kupractice lakini bado ni dakitari labda chuo ulichohitimu wakunyang'anye degree yako.

Sidhani kama mfumo wa ERB ni tofauti. Cheti chako kinakufanya uwe engineer lakini huwezi kupractice TZ bila kuwa registered. Hiyo ya kuitwa Eng. XYZ inaelekea ni utashi ERB lakini haimuondolei ambaye hana ERB registration hadhi ya kuwa engineer.
kwenye uhandisi kuna tofauti kidogo.

si lazima uwe na usajili ERB kufanya kazi za uhandisi.

lakini huwezi kumiliki/kuongoza kampuni ya uhandisi kama huna usajili.

huwezi kupewa kandarasi na hurusiwi kuomba kandarasi kama huna usajili.

huwezi kusaini mikataba ya uhandisi kama huna usajili.

huwezi kusimamia kandarasi kama huna usajili ERB.

haya ndio matakwa ya kisheria.

LAKINI KAZI YA UHANDISI UNARUHUSIWA KUFANYA LAKINI CHINI YA KAMPUNI YENYE USAJILI ERB, AMBAPO WASIMAMIZI WAKUU LAZIMA WAWE NA USAJILI ERB NA LIKIHARIBIKA JAMBO WAO NDO WA KUULIZWA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom