Imegeuka kuwa TV ya taifa. Nilikuwa mwanza kwa siku 10, nilikuwa nahama hotel na bar kila siku, kila ikifika saa 2 usiku wateja wote wanaomba wawekewe taarifa ya habari ya ITV sio tv nyingine yoyote ile.
Kuifahamu ni ngumu sababu haipatikani kwenye kila king'amuziNaona kama azam two nao habari zao za kina sana, kwa miaka ijayo itakuwa kidedea ila hivi sasa ni bado watu wengi hawajaifahamu
Ukitaka biashara yako idorore iwekee ushabiki wa vyama vya siasaKuna kitu kinaitwa ITV Syndrome kwa watanzania Karibu wote kwasababu TV ziliporuhusiwa kumilikiwa na watu binafsi ITV ni miongoni ya TV za mwanzo kabisa.
Hata huo mlio au melody ya taarifa ya habari haijawahi kubadilishwa toka wameanza na wamekuwa na habari nyingi nzuri toka mwanzo wakazoa watazamaji wengi dar na mikoani.
Na ilichukua watangazaji na waandishi wengi toka Redio Tanzania ya Serikali.
Ni kweliUkitaka biashara yako idorore iwekee ushabiki wa vyama vya siasa
Umenichekesha kwa kweliHuko Kolomije tukinunua tv tunasema tumenunua ITV

Kaka yangu hapanaaHawana uwezo wa kuifikia TBC kwenye habari na weledi..