Kumbe Hayati Magufuli ilibaki kidogo kumshtaki Karamagi mahakamani?

Kama JPM alimuona Karamagi kuwa si muadilifu ilikuwaje akamuachia aendelee na kampuni yake ya kushusha makontena bandarini? 🤔
 
Ila Kikwete alituharibia nchi sana, nashangaa sana watu wanaomshadadia
Si Kikwete Bali ccm maana walishaambiwa kuwa huyo Jamaa maadili ni zero . Ndo maana Mama anapoteza credit kwa kutaka Huyu Jamaa kujihusishahusisha na mambo ya nchi
 
HAKUWA NA HIYO NIA...

Chige's First Corruption Theory states that:-

To every grand corruption, there MUST BE two players to make it happen viz... high profile private sector executives in one hand and high profile politicians and/or top government executives in another hand.

Kwamba, hili Rushwa Kubwa ziweze kufanyika, ni LAZIMA pawe na pande mbili za kuwezesha rushwa hiyo kukamilika... kwa upande mmoja ni lazima pawepo na watendaji kutoka sekta na wanasiasa wakubwa na/au watendaji wakuu wa serikali!

Magu ALWAYS dealt with private sector executives na sio Wanasiasa wenye hadhi ya juu wala Watendaji wakuu wa serikali, na ndo maana katika miaka yake 5 YOTE, hakumgusa Mwanasiasa yeyote... alibaki tu kuishia "...gesi yote imeuzwa", imeuzwa na nani hakuwahi kutaja!

Mara kule kusini mtu ametafuna 20 Billion... Mtaje; HAKUWAHI KUTAJA!

Mara Mkataba wa Bandari ya Bagamoyo ni wa kifisadi... peleka basi mahakamani, hakuna hata mmoja aliyepelekwa!!

Akatangaza hadharani Kangi Lugola na Andengenye wamefanya yao... what happened?! Aliishia tu kuwatoa katika nafasi zao lakini cha ajabu akamrejesha tena Andengenye kwa madai eti ameomba msamaha!!!

Ni ZUZU tu ndie anaweza kudanganyika na Vita Dhidi ya Ufisadi wakati wa JPM!! Hata huyo Makonda ambae Magu mwenyewe alithibitisha kuagiza kontena lenye fenicha na kuzingizia ni vifaa vya walimu, bado alimwacha aendelee kuwa Mkuu wa Mkoa!!

Na hata huyo Kalamagi angeanzia wapi kwa mfano?! Kalamagi ni Swahibu Mkubwa wa Lowassa na Rostam Azizi!!

From nowhere, Rostam Azizi, hatua kwa hatua akaanza kuwa Swahibu wa JPM hadi kumtaka akagombee ubunge Morogoro!!!
Kaka adengenye sasa hivi ni mkuu wa mkoa wa Kigoma anakula tu mgebuka na ugali wa muhogo. Tatizo lilianzia pale kiongozi flani alianza kujenga image yake mwenyewe ya utakatifu na kama unavyojua tabia zetu watu weusi wale delegated kalibu wote wakabadilika wakageuka machawa. Rejea report ya CAG na upotevu wa 1.5tr mkulu alivyochimba mikwala lakini ma opportunist walioendelea kuimba nyimbo za sifa na kuabudu akina makonda mpaka kuweka plate number za serikalii kwenye magari yao binafsi. Ufisadi ni kitu kigumu sana vita yake sio ya maigizo unapaswa kuwa committed haswa
 
Magufuli alikuwa ni binadamu kama binadamu wengine kitu kilichomgharimu ni kutokuchukua hatua kwa mamlaka za juu za awamu iliyopita.

Hapa kuna kitu nimejifunza ukiwa moto kuwa moto kwelikweli maana hata maandiko yamesema ukiwa vuguvugu huna nafasi katika ufalme wa mbingu.

Na baada ya huyu bwana kutaka kujaribu kuanza kugusa baadhi ya watu na kuacha wengine hapo ndipo alipokosea wale aliowaacha ndio wakamuwahi yeye.
Nyie watu wa ajabu sana. Magufuli mwenyewe alikuwa mwizi kupindukia tatizo ni kwamba alitaka abakie anaiba peke yake.

Ila kwa umbumbumbu wenu mnamuona alikuwa anatetea wanyonge wa Tanzania.
 
Huenda niki ni cheti fake ama ndugu yake alikuwa cheti fake na ndiyo maana hiki cheti fake huwa kina hasira mbaya sana na Dk wa vyeti fake bwana JPM.

Vipi cheti fake umesharejeshwa kazini baada ya wenye roho nzuri kuingia madarakani?
Sawa cheti feki siyo huyo wa kwanza wako wengi tu. Hata yeye mwenyewe Magufuli PhD yake ilikuwa feki ndiyo maana alimuua Ben Saanane alipohoji. Na mwanaye Bashite naye alifoji jina la Makonda.

Leta hoja nyingine
 
Unaambiwa vyombo vya dola vilishaenda kumchukua kumpeleka kolokoloni kwa ajili ya kujibu tuhuma za kulisababishia Taifa hasara kupitia baadhi ya mikataba ya madini aliyoingia wakati akiwa Waziri akiiwakilisha Serikali.

Inasemwa mzee Mwinyi aliombwa na mmoja ya Viongozi mkuu mstaafu aende kumbembeleza JPM asifanye hivyo kwa sababu ya kumlindia heshima kwa sababu kwa vyovyote vile Karamagi angemtaja boss wake.

Inasemwa Karamagi alishajipanga kumtaja aliyekuwa kiongozi wake kama ndiye aliyemruhusu kuingia mikataba ile na yeye kama Waziri asingekuwa na uwezo wa kukataa maelekezo ya boss wake.

Ukweli ni kwamba JPM alipingana na mzee Mwinyi kuhusu kumlenga mkuu wa zamani wa mhusika bali lengo alitaka mhusika akajibu yeye kama yeye tuhuma zile baadae Jaji mkuu wa kipindi kile alimshauri JPM asitishe nia yake hiyo kwa sababu kwa vyovyote vile ilikuwa ni lazima mamlaka za uteuzi wa Karamagi zingeguswa na hiyo kesi jambo ambalo katiba ya Nchi inazuia.

Kumbukeni gesi iliyopo Mtwara Tanzania si ya Watanzania.

Nb: Huenda ndiyo JPM alikufa kifo chema!
Upuuzi tu mikataba ya hovyo ya madini na nishati imesainiwa tangu wakati wa mwinyi wakati huo magufuli BADO mshamba tu
 
Ila Kikwete alituharibia nchi sana, nashangaa sana watu wanaomshadadia
Sema ccm

unakumbuka mwinyi na mkwewe waliyo totosha dhahabu, mrema anajua

unaikumbuka kashfa ya Chavda??

Unajua mbuga ya loriondo iliiuzwa wakati gani?

Unajua kuwa loriondo iliuzwa wakati gani

Baada ya kuondoka Mwalimu awami zote zimefanya ufisadi wa kutisha
 
Nakumbuka dege liliungurumishwa usiku wa manane kwenda kufanya bargain na kiongozi wa juu wa china, kulikuwa na mawili kuingia mkataba wa kinyonyaji hasa huu wa gesi ama prince anyongwe hadharani.

Hii nchi ilichezewa mno wakati wa awamu ya tano.
Awami zote ccm haifai
 
Kwenye Richmond, Lowassa alimuuliza JK... "kuna kipi nilifanya ambacho ulikuwa hujui?"

Anyways, hakuna jambo kubwa serikali inafanya bila Cabinet kulipitia na kujadili. Karamagi asingeweza kusaini mikataba ya madini na makampuni huko nje bila Rais na Cabinet kuwa na taarifa.
 
Unaambiwa vyombo vya dola vilishaenda kumchukua kumpeleka kolokoloni kwa ajili ya kujibu tuhuma za kulisababishia Taifa hasara kupitia baadhi ya mikataba ya madini aliyoingia wakati akiwa Waziri akiiwakilisha Serikali.

Inasemwa mzee Mwinyi aliombwa na mmoja ya Viongozi mkuu mstaafu aende kumbembeleza JPM asifanye hivyo kwa sababu ya kumlindia heshima kwa sababu kwa vyovyote vile Karamagi angemtaja boss wake.

Inasemwa Karamagi alishajipanga kumtaja aliyekuwa kiongozi wake kama ndiye aliyemruhusu kuingia mikataba ile na yeye kama Waziri asingekuwa na uwezo wa kukataa maelekezo ya boss wake.

Ukweli ni kwamba JPM alipingana na mzee Mwinyi kuhusu kumlenga mkuu wa zamani wa mhusika bali lengo alitaka mhusika akajibu yeye kama yeye tuhuma zile baadae Jaji mkuu wa kipindi kile alimshauri JPM asitishe nia yake hiyo kwa sababu kwa vyovyote vile ilikuwa ni lazima mamlaka za uteuzi wa Karamagi zingeguswa na hiyo kesi jambo ambalo katiba ya Nchi inazuia.

Kumbukeni gesi iliyopo Mtwara Tanzania si ya Watanzania.

Nb: Huenda ndiyo JPM alikufa kifo chema!
Huwa nafikiri nchi hii iingie vitani Kwanza halafu tuanze upya ustaarabu
 
Kumuhukumu Kikwete nikumuonea tu kwani kila kiongozi ana mema na mazuri yake. Kila zama na kitabu chake hivyo Kikwete na Jpm hawakuwa malaika wana mapungufu yao pia wana mazuri sio lazima kuyaorozesha hapa. Sio vizuri kuwaza mambo kwa chuki Sasa hivi kuna mikanganyiko na misigano ya makundi vijana tukae neatral tusiwe mashabiki wa upande wowote tutalibomoa Taifa letu
Tukibadili katiba tutaanza na yule kikongwe, kaburi la mkapa, kaburi la chato na mkwere pia wote tutawanyonga na vibaraka wao,
 
Sema ccm

unakumbuka mwinyi na mkwewe waliyo totosha dhahabu, mrema anajua

unaikumbuka kashfa ya Chavda??

Unajua mbuga ya loriondo iliiuzwa wakati gani?

Unajua kuwa loriondo iliuzwa wakati gani

Baada ya kuondoka Mwalimu awami zote zimefanya ufisadi wa kutisha
CCM ni ukoo wa panya wote majizi
 
Mkuu hujaielewa vizuri hoja ya mleta mada! Ukisoma mistari ya chini hapo kuna statement inasema, aliitwa hadi aliyekuwa jaji mkuu wa wakati huo ili kutoa ushauri naye akashauri kesi isifunguliwe! Hapo ni kwamba jaji mwenyewe alijiridhisha kuwa kama kesi hiyo ingefunguliwa basi mkono wa sheria usingeiacha salama mamlaka ya uteuzi wa Karamagi!
Mfano hata wewe kama uliua mtu mwaka 2010, ukaja kukamatwa leo na katika utetezi ukaja kumtaja alokutuma au mliyeshirikiana nae kufanya hivyo, sheria haitamuacha salama!
Hivyo kama hayo ni ya kweli basi kesi hii ilizimwa kuepusha shari kwani ni lazma wangeguswa watu nyeti!

..Magu angemshtaki vipi Karamagi wakati alishaanza kula na Rostam Aziz?
 
Magufuli kama aliamua kupambana na hao jamaa angepambana nao mwanzo mwisho, kuliko kuwa na nia, uwezo, na sababu lakini akaacha kwa lengo la kuwalinda wastaafu.
Nilimkubali Magufuli kwa baadhi ya mambo aliyosimamia na kuyafanya; lakini kulialia kila siku kuwa nchi imechezewa sana huku akishindwa kuwachukulia hatua hao waliochezea nchi naye alionekana mbabaishaji na mpigaji kama waliomtangulia.

Hii nchi haiwezi kunyooka bila kuongozwa kijeshi japo kwa miaka miwili.
 
Back
Top Bottom