Kumbe Hawa Ngulume bado Mbabe?

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,976
10,466

Niwe wazi kuwa sina ubaya na huyu mkuu wa wilaya mtukuka, ila nitasimulia ubabe wake kwa ufupi tu. Akiwa mkuu wa wilaya ya Konondoni, mnamo mwaka 2002, aligoma kabisa kusaini fomu zetu za kuombea mikopo kwa ajili ya masomo ya chuo kikuu. Nakumbuka wanafunzi wengi wa vyuo vikuu tuliokuwa wakazi wa wilaya hii tulipata shida sana kupata huuma hii, na kuna wengine walilambwa vibao walipomlazimisha awasainie fomu zao. Ikabidi sisi waoga tuene mikoani kwenda kusainiwa fomu hizi.
Sasa niliposikia kituko hiki cha kumpiga mkulima wa Mbarali nikakumbuka yale aliyoyafanya alipokuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni, nikajisemea kimoyomoyo kuwa, alaaas! Kumbe Mama bado mbabe sio? Hajaacha tu?
 
Hivi unamjua Hawa Ngulume wewe au umemsikia tu? Vituko vyake alipokuwa DC pale Bagamoyo je? alikuwa maarufu kwa kuita watu ofisini kwake (awe mfanyakazi katika ofisi yake, mfanyabiashara pale mjini Bagamoyo au yeyote aliyetokea kufanya jambo kinyume na anavyotaka yeye (hata kama kafanya jambo sahihi kabisa!). Basi ni kukunjwa shati (au gauni!) na kutwangwa makonde tu! Huyu mama ana tatizo la kiakili jamani. Ila sijui kwanini analindwa na kuhifadhiwa tu, anafanya yote haya bila wasiwasi wa kukaripiwa kutoka juu wala pembeni! Labda tuulize kama wenzetu mnajua chimbiko la huu wazimu wake na jeuri kali kama hiyo! Ningekuwa mkuu wake wa kazi ningeshamsimamisha kazi na kutaka akapimwe akili siku nyingi!
 
inabidi mh Ngulume ajirudi na kuomba msamaha wana Mbarali kama ni kweli au sifa nyingi ulizopewa za kufanikisha kutuondoa sisi wafugaji bonde la Ihefu zimekulevya ukajikuta unafanya mambo yasiyo na staha
 
inabidi mh Ngulume ajirudi na kuomba msamaha wana Mbarali kama ni kweli au sifa nyingi ulizopewa za kufanikisha kutuondoa sisi wafugaji bonde la Ihefu zimekulevya ukajikuta unafanya mambo yasiyo na staha

Mbona mi sielewi ina maana ni baunsa kiasi gani hadi awakunje wanaume wazima na ndevu zao? si wamrudi tu??
 
Hawa ngulume zamani alikuwa afande wa JKT. Na huko ilikuwa ni ubabe tu. Niliwahi kusimuliwa na kaka yangu kuwa wakati hawa ni afande pale makutopora JKT Hawa alikuwa ana tabia kila saa kumi na moja asubuhi anaingia kwenye mahema na dorms za kuruta wa kiume kuwaamsha waende kukimbia mchaka mchaka. Siku moja waliamua kumfundisha aadabu. Alipokuja saa zile za alfajiri kuwaamsha akawakuta wote wamelala uchi mtupu juu ya vitanda vyao. Alitoka mbio na kunza kuwabembeleza watoke. Hawa ni DC mbabe ndiyo maana anamuona Lowasa kuwa ananyanyasa madc wakati si kweli. Tatizo ni lake.
 
Si aligombea ubunge singida akatoka patupu- harafu nasikia ni mgonjwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…