Kama hujui uliza uambiwe.
Mahakama za kanisa zilikuwapo tokea katiba ya nchi hii inatungwa.
Na Polisi huandika R.B kumtaka muhusika aripoti kwenye mahakama za kanisa
Tena kwa kodi yetu sisi soote.
Unachoshindwa kuelewa ni kwamba HAKUNA SHEIKH ANAEWEZA KUTUMA R.B YA JESHI LA POLISI KUMWITA MUHUSIKA KSHERIA ILI AFIKE KWENYE MASHAURI YA KADHI KWA KUWA KISHERIA HAIPO.
LAKIN CARDINALI PENGO HUWEZA KUTUMIA R.B YA JESHI LA POLISI KUMWITA MUHUSIKA KWENYE MAHAKAMA ZA KANISA.KWA KUWA KIKATIBA NA KISHERIA ZINATAMBULIKA.
ELEWA HIYO HOJA..UELEWE HIYO HOJA.
Huu ni uwongo wa mchana kweupe kabisaa hakuna sehemu yoyote ambayo polisi wanaweza wakatoa rb ya kumuita muhusika kwenye mahakama ya kanisa.
Kinachoweza kufanyika polisi wanaweza wakatoa Rb namba kwa mtu yeyote aliyekwenda kutoa taarifa kituoni Kama namba ya kumbukumbu ya taarifa yake.
Lakini mambo ya kuhusiana na taarifa iliotolewa kituoni hushughulikiwa vituoni hukohuko Kama ni taarifa ya kupelekwa Mahakamani hupelekwa na polisi wenyewe kwenye mahakama hizihizi za kawaida.
Na siyo kweli kwamba kanisa wanaweza wakaenda kituoni wakachukua Rb namba ya kumuita mtuhumiwa Ili wakamshitaki kwenye mahakama za kanisa.
Isipokuwa mtu yeyote bila kujali dini yake ama taasisi yake anaweza akatoa taarifa kituoni akapewa rb namba yake.
Kitakachofuata polisi watafanya kazi yao ya kumuita/kumkamata mlalamikiwa kabla ya kupeleka kesi Mahakamani mlalamikaji ana weza akaomba polisi mambo yake ya ishie nje ya mahakama.
Hapo polisi wanaweza wakamruhusu bila kujali kuwa swala lake ana lipeleka kwa viongozi wa dini yake au ana peleka kwenye familia yake.
Baada ya suluhu,mlalamikaji ana rudisha mrejesho kituoni kwa hatua zaidi za kumaliza lalamiko lake kisheria.
Taratibu ambazo zinafanywa na polisi au mahakama hizihizi za kawaida kama malalamiko yake yalifikishwa mahakamani.