Kumbe hata TANROADS alianzisha Mkapa, sasa wengine walifanya nini miaka 10 Ikulu ?

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
6,410
8,911
Kuanzia TRA kumbe mpaka TANROADS ni Mzee Mkapa ( RIP) alianzisha, sasa wengine miaka 10 walikuwa wanafanya nini Ikulu ? Angalau Mzee Mwinyi miaka 10 alipiga kazi pia, alifanya mengi sana ukichukulia ukweli kwamba aliongoza nchi kipindi kigumu sana cha mageuzi ila 2005-2015 ni lost decade Tanzania, sioni kilichofanyika kama kuna anayejua ukiondoa substandard UDOM aseme, hata Bunge letu Dodoma ni Mzee Mkapa alijenga, Magufuli (RIP) alianza kujenga Mji wa kiserikali na kuhamia rasmi Dodoma.

Hata mchakato wenyewe wa Katiba ulianzishwa kipindi hicho ulikuwa fake, sasa nini kilifanyika cha maana kwa miaka 10 ?

Nilichojifunza ni kwamba ukiona mtu anatumia nguvu nyingi sana kutaka kuwa raisi ujue ni bogus, Mkapa wala hatukutegemea na wala hakuna aliyetegemea lkn alikuwa success story, ila nguvu iliyotumika kuingiza 2005-2015 ni kubwa mno tulichopata ni hasara tupu, 2015-2020 pia tulishtukizwa na ilikuwa ni success story depending on your IQ kama ni low unaweza usione, …
 
duh pole sana

kila awamu ina mengi iliyofanya.

tulia ujifunze, naamini umeleta hii mada kichokozi. ila tulia uelimishwe
 
Kikwete pamoja na mapungufu yake yote, hii nchi aliiunganisha kwa mtandao wa barabara kuliko wakati wowte ule akifuatiwa kwa karibu na uncle. Hata kwenye elimu mchango wake uko wazi. Tatizo alikuwa mpole sana.
 
duh pole sana

kila awamu ina mengi iliyofanya.

tulia ujifunze, naamini umeleta hii mada kichokozi. ila tulia uelimishwe
Sisi mwenyekiti wetu amefanya mageuzi makubwa ndani ya uongozi wake kama vile kuondoa ukomo wa mwenyekiti, kuajiri nyumbu wengi kwa ajili ya kumpigania yeye tu mitandaoni na chamani, Mwaka 2015 kakodisha chama kwa Lowasa na baada ya mkataba kuisha Lowasa katukimbia, kusajili wauza unga, wanywa gongo na mateja kuwa wanachama wetu. I mean mwenyekiti wetu kafanya mengi ndani ya chama chetu kuliko hao uliwataja hapa mtandaoni.
 
TRA iliasisiwa na mstaafu Mwinyi.

Akiwatumia zaidi Sanare na Kezilahabi.

1997 ilikuwa ni kuianzisha rasmi kwa kuunganisha Idara za Customs, Income Tax na Sales tax!
Mleta mada kahadisiwa na shemej yake, na yeye bila kuuliza watu tuliokuwepo enzi hizo, kaja mzima mzima kujiaibisha mwenyew hapa jukwaani.
 
Kuanzia TRA kumbe mpaka TANROADS ni Mzee Mkapa ( RIP) alianzisha, sasa wengine miaka 10 walikuwa wanafanya nini Ikulu ? Angalau Mzee Mwinyi miaka 10 alipiga kazi pia, alifanya mengi sana ukichukulia ukweli kwamba aliongoza nchi kipindi kigumu sana cha mageuzi ila 2005-2015 ni lost decade Tanzania, sioni kilichofanyika kama kuna anayejua ukiondoa substandard UDOM aseme, hata Bunge letu Dodoma ni Mzee Mkapa alijenga, Magufuli (RIP) alianza kujenga Mji wa kiserikali na kuhamia rasmi Dodoma.

Hata mchakato wenyewe wa Katiba ulianzishwa kipindi hicho ulikuwa fake, sasa nini kilifanyika cha maana kwa miaka 10 ?

Nilichojifunza ni kwamba ukiona mtu anatumia nguvu nyingi sana kutaka kuwa raisi ujue ni bogus, Mkapa wala hatukutegemea na wala hakuna aliyetegemea lkn alikuwa success story, ila nguvu iliyotumika kuingiza 2005-2015 ni kubwa mno tulichopata ni hasara tupu, 2015-2020 pia tulishtukizwa na ilikuwa ni success story depending on your IQ kama ni low unaweza usione, …
Uko sahihi kabisa Rais Mkapa alianzisha TANROADS na alitambua umuhimu wa kuwa na taasisi zinazodumu badala ya kutegemea mtu anayepita na kupenda kusema "Mimi nasema". Ila sina uhakika kama TANROADS aliyoianzisha Rais Mkapa ndiyo TANROADS ya leo! TANROADS ilianzishwa kwa mujibu wa makubaliano na wafadhili wa nje ambao walikuwa wanachangia ujenzi wa barabara lakini Serikali yetu ilikuwa haina utaratibu wa ukarabati mpaka barabara nyingine zilihitajika kujengwa upya. TANROADS ilianzishwa kwa makubaliano na uendeshaji wake ulitakiwa uwe katika kiwango cha kimataifa. Hilo ndilo jambo Tanzania hatuwezi kulifanya! Anayebisha atafiti!
 
Ni kweli lakini tusisahahu pia Mkapa alipata hiyo nafasi kwa sababu nchi ilikuwa katika mpito; alikuwa anajenga msingi wa uchumi wa kisasa. Kikwete angefanya nini? Aanzishe tu taasisi hata kama hazihitajiki?
 
Escrow, Richmond, Dowans, IPTL, EPA, Usafirishaji wa Twiga, Largest Hub of drugs distribution East and South of Africa...mnyonge mnyonge ila haki yake mpeni,kuna mwamba alianzisha yote haya, 10yrs hakukaa bure, he worked tirelessly to achive those institutions.
 
Kuanzia TRA kumbe mpaka TANROADS ni Mzee Mkapa ( RIP) alianzisha, sasa wengine miaka 10 walikuwa wanafanya nini Ikulu ? Angalau Mzee Mwinyi miaka 10 alipiga kazi pia, alifanya mengi sana ukichukulia ukweli kwamba aliongoza nchi kipindi kigumu sana cha mageuzi ila 2005-2015 ni lost decade Tanzania, sioni kilichofanyika kama kuna anayejua ukiondoa substandard UDOM aseme, hata Bunge letu Dodoma ni Mzee Mkapa alijenga, Magufuli (RIP) alianza kujenga Mji wa kiserikali na kuhamia rasmi Dodoma.

Hata mchakato wenyewe wa Katiba ulianzishwa kipindi hicho ulikuwa fake, sasa nini kilifanyika cha maana kwa miaka 10 ?

Nilichojifunza ni kwamba ukiona mtu anatumia nguvu nyingi sana kutaka kuwa raisi ujue ni bogus, Mkapa wala hatukutegemea na wala hakuna aliyetegemea lkn alikuwa success story, ila nguvu iliyotumika kuingiza 2005-2015 ni kubwa mno tulichopata ni hasara tupu, 2015-2020 pia tulishtukizwa na ilikuwa ni success story depending on your IQ kama ni low unaweza usione, …
Upofu wako kuona mambo ya kikwete hayawezi kufanya kuwa hajafanya kitu
 
Ni kikwete tena!!!!! Hakuna alichofanya?!!!!! Kuna jambo si bure, nahisi ni timu maalum imsundaa kwa ajili ya kumchafua huyu mzee,....sijui ni ile iliyoundwa kipindi kile cha 2016 kuja juu bado ipo?!
 
Kitu ulichosahau ni kwamba serikali inaendeshwa kwa mtindo wa kupokezana vijiti kama zile mbio za relay na timu ikimaliza huwa inashinda au inashindwa kama timu na siyo mtu mmoja mmoja. Ni kweli Mkapa alianzisha na kuendeleza yaliyoanzishwa na mtangulizi wake. Vivyo hivyo kwa Kikwete na Magufuli. Samia naye, kama watangulizi wake, anamaliza na kuanzisha yake. Ni fikira fikirishi kudhani kuna mtu kafanya na mwingine hakufanya wakati unaona kuna miradi mingi iliyomaliziwa na kiongozi ambaye wala hakuianzisha.
 
Back
Top Bottom