Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,494
- 37,786
1. Mwaka 1985-1995 Tanzania iliongozwa na Rais Alli Hassan Mwinyi. Alilirithi nchi iliyotoka kupigana Vita miaka 5 nyuma na kuacha uchumi uliodhoofika kiasi cha Rais wa nchi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwataka Wananchi kufunga mikanda. Katika kipindi chake ndipo tulipoona Sera ya Soko huria (Yeye akiita Ruksa), Kurejeshwa Kwa mfumo wa kidemokrasia wa vyama vingi, Uhuru wa kukosoa, kufunguliwa Kwa wanasiasa waliokuwa kizuizini nk. Lakini mpaka Leo hakuna MAKUMBUSHO ya Mwinyi.
2. Mwaka 1995-2005 Tanzania ilikuwa chini ya Benjamin William Mkapa. Huyu ni Rais wa Kwanza Tanzania kuongoza nchi yenye upinzani rasmi wa Kisiasa baada ya ushindi wake katika sanduku la Kura dhidi ya Mgombea machachari Augustine Lyatonga Mrema (RIP). Huyu ndiye muasisi wa misingi ya uchumi unaotegemea pato la ndani Kwa kuanzisha mamlaka imara ya Mapato (TRA), Msamaha mkubwa wa madeni Kwa nchi, Ubinafsishaji wa mashirika ya Umma yaliyokufa au kudorora, akifungua uchumi wa kusini mwa Tanzania ulioathiriwa na Sera ya ukombozi wa Afrika, ujenzi wa miundombinu Kwa kauli yake ya "kusafiri Kwa Tax toka Mtwara hadi Bukoba, nk. Still hata huyu sijawahi kusikia MAKUMBUSHO ya Mkapa.
3. Mwaka 2005-2015 nchi iliongozwa na Jakaya Mrisho Kikwete akishirikiana Kwa karibu na Swaiba wake Waziri Mkuu Edward Ngoyai Lowassa. Huyu katika kipindi chake alijitahidi kuimarisha elimu Kwa kuhakikisha Kila Kata inakuwa na shule ya sekondari, Elimu Kwa walioikosa (MEMKWA), kuongeza miundombinu ya barabara, Uimarishaji wa demokrasia, Mchakato wa Katiba mpya japo haikufika mwisho nk. Mpaka Leo hakuna MAKUMBUSHO ya Kikwete.
4. Mwaka 2015-2020+ akaja jembe, tingatinga John Pombe Magufuli. Kwa miaka yake 5 na miezi 3 madarakani alijitanabaisha kama adui wa ufisadi, wizi, uzembe na udanganyifu. Muumini wa ujenzi wa miundombinu kama Msingi wa uchumi nk. Mwaka mmoja baada ya kifo chake tayari ana Makumbusho yake. Hivi ni serikali hii hii iliyoona aliyeongoza miaka 10 Hana cha kukumbukwa Bali aliyeongoza miaka 5? Au kuna mfadhili kajitolea kujenga na atatuwekea vitu vya kutukumbusha ukuu wa Mwendazale ndani ya miaka 5? Kama ni serikali basi kuna mahali hapako Sawa au Kwa makusudi mmeamua kuwadharau wengi na kumtukuza mmoja. Vinginevyo mtueleze vigezo mlivyotumia kufanya upendeleo huu.