The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,911
- 2,891
Kuna msemo wa kiha ambao tafsiri yake ya kiswahili inasema fimbo iliyompiga mke mwenzio wewe itupe mbali.
Niutumie usemi huu kumkumbusha kaka yangu Slaa kuwa mfumo alioupigania kama si kuuasisi ndani ya CHADEMA ndo huohuo uliomwondoa kwani tuliishuhudia CHADEMA chini ya ukatibu mkuu wake ikifukuza watu bila kuja na maelezo ya maana sana sana tunaambiwa ni msaliti.
Waathirika wa hiyo fukuzafukuza ni kama kina Juliana Shonza,Mtela Mwampamba,Zitto Kabwe,Samson Mwigamba,Kitila Mkumbo na wengine walioamua kuondoka baada ya kuona demokrasia iliyoko CHADEMA imejengwa juu ya kusujudia watu.
Haya yote Dr. Slaa alikuwa anayajua vizuri kwa hiyo leo namshangaa kwanini anapata tabu ya kuishangaa CHADEMA kumfanyia ilichomfanyia.
Mimi nadhani aache kulalama awapongeze kwa kazi nzuri waliyofanya, ajue kuwa hiyo ndio CHADEMA na wengine walioko huko pia niwakumbushe yaliyompata ndugu Slaa yanawahusu pia kwani CHADEMA haitabiriki hata kidogo.

Last edited by a moderator: