Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau amani iwe kwenu.
Nimefuatilia kwa karibu hali ya wanasiasa wanaojivua uanachama wa CCM na kujiunga na vyama vingine. Nimefuatilia pia wale wanaotoka vyama vya upinzani na kujiunga na CCM ama kwenda vyama vingine vya upinzani. Nimefuatilia ili kujua sababu za wao kujiengua uanachama na vile vile nimeangalia nini kimewapeleka huko walikoenda ( push and pull factors). Nimeangalia pia hali ya wanasiasa hao wakiwa kwenye vyama vipya na hatma yao kisiasa.
Baada ya kutafakari sana, nimebaini kuwa wengi wa wanasiasa wanaohama CCM na kwenda vyama vingine, wamekuwa wakifanya hivyo kwa chuki hasa baada ya kukosa nafasi ya uteuzi katika ngazi mbalimbali. Kwa wale wafuasi wa kawaida, wamekuwa wakifanya hivyo baada ya mgombea wanayempenda kutoteuliwa kugombea nafasi fulani. Hapo ndipo wanapoamua kwenda upande mwingine ambako ama huteuliwa moja kwa moja kugombea nafasi walizokosa ama kupewa hadhi zaidi ya kiuongozi.
Hata hivyo, pamoja na kupewa hadhi hiyo huko walikoenda, asilimia kubwa ya makada hao wamejikuta wakiikumbuka zaidi CCM na wengi wao wamekuwa wakiendelea kumiliki kadi za CCM hata kama wapo upinzani. Huko wanakoenda hakika wamejikuta wakikosa ushirikiano na mahaba kutoka kwa wafuasi wao na hivyo wanajikuta wanaishi maisha ya ukimbizi wa kisiasa.
Nimebaini pia kuwa mambo yakienda kombo huko walikoenda wengi wao wanatamani kurejea CCM ambako kwa hakika ndiko kwenye raha ya maisha yao kisiasa. Dr Slaa anamiliki kadi ya CCM na siku zote pamoja na kuwa alishika nafasi ya juu sana CHADEMA hakika amekuwa mwanachama mwaminifu na mtiifu wa CCM na amekuwa akilipa michango yake ya mwaka kwa wakati.
Juma Duni Haji alikuwa mgombea Mwenza wa CHADEMA akitokea CUF. Baada ya kubaini kuwa CHADEMA hakuna siasa bali ni mkusanyiko wa wapiga deal, alijikuta anakosa hamasa ya kuendelea kuwepo kwenye chama hicho na kuamua kurejea kwao CUF. Edward Lowasa alikuwa na matumaini kibao ya kuteuliwa kuwa Mgombea wa CCM, Baada ya kukosa nafasi hiyo, alijikuta anakimbilia CHADEMA ambako kwa sasa anaishi kama mkimbizi. Kuna taarifa kuwa Lowasa amemwandikia Katibu Mkuu wa CCM barua ya kuomba radhi na kutaka kurejea CCM.
Kingunge Ngombale Mwiru licha ya kuondoka kwa hasira ndani ya CCM, ameshamwomba radhi Mwenyekiti wa CCM na anatamani kurejea chamani. Frederick Sumaye alitishia kurejea CCM baada ya kuona kuwa CHADEMA wamempa kisogo. Baada ya kugundua hilo, Freeman Mbowe akabadili gia angani na kuamua kumteua kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu hata kama hajawa mwanachama wa chama hicho. Ipo mifano mingi ila kwa leo naishia hapa.
Kwa hali hii, nashauri itungwe sheria ambayo itaruhusu wanachama kwenda kufanya siasa kwa mkopo kwenye chama kingine na wawe huru kurejea kwenye chama chao wakati wowote watakaoona kuna haja ya kufanya hivyo. Kwa kufanya hivyo, itawasaidia sana vyama vya upinzani ambavyo mara zote wamejikuta wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa wanasiasa makini hasa inapokuja wakati wa uteuzi na uchaguzi.