Kumbe dawa ya magazeti ya udaku ni Ukuda. Kwa mara ya kwanza hawakuweka udaku juu ya msiba wa Mkapa. Pongezi Mwakyembe

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,297
21,439
Kwa mara ya kwanza msiba mzito umeisha salama bila kuwepo na habari za udaku. Tulizoea huko nyuma magazeti mengi yalizoea kufanya udaku kwa kukuza story ili yauze nakala nyingi hususani kwenye misiba ya watu mashuhuri!

Ingekuwa zamani msiba wa mkapa usingeisha salama bila habari za magazeti udaku kuweka habari mifano mwa hizi!!
  1. Msiba wa mkapa Vuta Ni kuvute😋😋
  2. Mazishi ya mkapa wingu zito😋😋
  3. Mauza uza yatawala msibani
  4. Kuku afunga njia msibani
  5. Joka kubwa laonekana lupaso
  6. mabomu yazua tafrani msibani
  7. Mganga atinga msibani na ungo
  8. mwewe washiliki mazishi masasi
"Tuliliona Hilo kwa baba wa taifa, Tuliona Hilo kwenye msiba wa Juma Alli Juma, Tuliona Hivyo kwenye msiba wa kanumba na wengine kibao!"

HAKIKA DAWA YA UDAKU NI UKUDA!

Heshima imerudi mahala pake
Ustaarabu umerejea!!
 
Mkuu, upo sahihi!
Naongezea: -

-Mkapa ameuwawa na ugonjwa usiokuwepo Tanzania

-Alichoelezwa JK dakika ya mwisho.....

-Siri ya JPM kugawa fedha wakati akitoka msibani hii hapa…..

-Mazungumzo ya mwisho ya Ben na Kinana, hadharani…… .
 
Back
Top Bottom