Wabunge wa CCM, mzaha wenu kwa Katiba juu ya muda wa Rais kukaa madarakani ni msiba kwetu sote

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
12,417
30,927
Kuna mtu aliwahi kusema humu Jamiiforums kwamba in politics everything happens for a reason. Akimaanisha kwamba lolote ulionalo kwenye siasa halitokei kwa ajali liko well calculated na linafanywa au kusemwa kwa sababu.

Nawaonya wabunge wa CCM mchezo wao na mzaha wao kwenye katiba yetu ni anguko letu sote. Mnaitoboa meli ambayo tumepanda wote, ikizama tutazama wote.

Mkapa RIP aliona mbali na kwenye kitabu chake alisema kuongeza muda wa kukaa madarakani kwa viongozi wa Afrika sio tu ni janga kwa nchi zao Bali pia regional instability ya Kanda nzima. Na akatolea mfano wa Burundi.

Pia alienda mbali akasema Salmin Amour commando alipotaka kujiongezea muda kule Zanzibar alimpinga na akamkemea.

Swali je wabunge wa CCM nyie mna exposure na ufahamu wa Mambo kuliko hayati Mkapa?

Mpaka Sasa kumbukumbu zangu zinaniambia wabunge wa CCM waliochagiza hoja hii ni Hawa wafuatao.

1. Yule wa Nkasi rtd
2.Juma Nkamia
3. Jah pipo wa njombe
4. Msukuma

Cha ajabu Rais mwenyewe kashasema yeye hataki kufanya huo ujinga nyie kwanini mnamlazimisha? Au ndio kujipendekeza kulikopitiliza?

Mtu wa karibu na Rais mh Polepole juzi tu hapa amerudia Tena dhamira ya Rais ya kutojiongezea muda Sasa nyie kimbelembele hiki mnakitoa wapi?

Chondechonde wabunge wa CCM msituharibie nchi yetu kwa upungufu wenu wa akili Kama mnajikomba kwa Rais basi fanyeni kwa Mambo yenu binafsi msilitingishe taifa letu.

Niwaombe wabunge mlioko humu Jamiiforums muwapigie simu hao wabunge wenzenu wasome andiko langu.

Pia naomba magazeti yacopi na kupest hizi hisia zangu juu ya mustakabali wa taifa letu.

Wabunge wa CCM mmetufanyia mengi ya kuudhi sisi watanzania tunawavumilia sasa msitutie vidole vya macho na mataco.
Ukimya wetu sio ujinga.

Nadhani mtatuelewa sisi watanzania wengine.
 
Hivi mtu mmoja aonekane anafaa kuliko watu 60 milioni ? Msione fahari kuiga ujinga wa China hata Kaka yako akiwa kubwa jinga huwezi kuwa na fahari naye. China ni kielelezo Cha ubaya wa binadamu katika kuonyesha ubinafsi wake uliopitiliza.
 
Ningewaona wa maana Kama mngempendekeza rais magufuli aendelee kubaki madarakani kwa kufwata mifumo ifuatayo.

1. UJERUMANI ANGELA MECKEL
HAwa watu mifumo Yao ni thabiti hata mtu akikaa miaka 20 taifa Halinung'uniki maana taasisi zao za kudhibiti "ubinadamu wa rais" Zina nguvu akizungua hawacheki na nyani wanakutoa in a flash of an eye.Mifumo iko wazi na mahakama Zina nguvu na demokrasia haina doa. Anjela mekel amekaa madarakani nadhani miaka 16 Sasa kabla ya hapo Helmut Kohl naye alikaa muda mrefu.

2. ISRAEL BENJAMIN NETANYAHU
Hawa pia mifumo Yao ina nguvu Sana waziri mkuu hayuko juu ya mahakama Benjamin NETANYAHU is the longest serving pm in Israel history lakini watu hawana tatizo na ndio maana wanaandamana kea Uhuru kumpinga na akizingua wanapiga chini siku hiyohiyo.
Mfano mzuri ni EHUD OLMERT huyu akiwa meya wa Jerusalem alikula hela ya uma baadae akawa waziri mkuu muda ulipoisha wakamfungulia kesi alifungwa jela miezi sita na uwaziri mkuu wake.

Kwahiyo wanaojikomba kwa magufuli angalau wangeanza na kuchagiza katiba yenye nguvu na sio hii ya Sasa ambayo rais akikosea mihimili yote inafyata mkia. Yani tuwe na bunge la kijinga Kama la ndugai halafu magufuli atawale 10 yrs more acheni ujinga nyie CCM mtageukana wenyewe kwa wenyewe mkose pa kutokea .

You short sighted people.
 
Wanapanga kufanya uhalifu kwenye katiba ya nchi february hii , Sanga hakuropoka kwa bahati mbaya
Kama ni hivi basi anaewatuma ni Magufuli mwenyewe na hili litakuwa doa kubwa Sana kwenye historia ya taifa letu.

Nyerere resigned peacefully
So was mwinyi mkapa and jakaya magufuli plz never try this do not sabotage our constitution.
 
Tunaonya kwa uwazi juu ya kuchezea katiba ili hata historia ikiandikwa kwa damu sisi tutakuwa tumenawa mikono hatutakuwa na hatia mbele za Mungu na watanzania wenzetu.
 
Haya mawazo ya hawa wabunge wanaotaka rais kuongezewa muda ni in direct kick, yuko mtu nyuma hili hawezi jitokeza hadharani kudai hili kwa sababu ataambiwa amevunja miiko na itikadi/katiba ya nchi., ukweli ni kwamba inataka kutumika mwamvuli wa hawa wabunge wasiojielewa sasa ambao akili zao na maarifa yao yametekwa nyara ili isomeke kwenye vyombo vya kimataifa na dunia kwamba bunge la Tanzania limemuongezea rais wao muda kuendelea kusalia madarakani ingawa rasi mara kadhaa amekuwa akikataa kuongezewa muda tafsiri hasa inatakiwa isomeke hivyo.

Wadanganyika amkeniii., akina Tundu Lissu washaliona hili kitambo ndio mana hupiga kelele akiwa kule uhamishoni belgium lakini hakuna anayemsikiliza mana ni mpaka uweke bando udownload Youtube, Watanzania wengi bado wanaona ni utani bado, time will tell.
 
Tunaonya kwa uwazi juu ya kuchezea katiba ili hata historia ikiandikwa kwa damu sisi tutakuwa tumenawa mikono hatutakuwa na hatia mbele za Mungu na watanzania wenzetu.
Katiba ni ya wananchi wakiamua Rais aongezewe muhula mwingine hakuna wa kuzuia hilo. Rais wa 32 wa Marekani Franklin Roosvert muhula wake wa kipindi cha miaka minane uliisha mwaka 1941 kwa mujibu wa katiba, lakini wananchi wakasema sisi ndio wenye katiba tunamwongezea muhula mwingine, na ikawa hivyo mpaka mwaka 1945,na hao ndio mababa wa demokrasia duniani sembuse sisi.
Tuachane na matashi binafsi,tuwaachie wananchi wakiamua aongezewe muda hakuna mwenye moral strength ya kuzuia.
 
Kuna mtu aliwahi kusema humu jamiiforums kwamba in politics everything happens for a reason. Akimaanisha kwamba lolote ulionalo kwenye siasa halitokei kwa ajali liko well calculated na linafanywa au kusemwa kwa sababu...
Hiyo kataa ya Magufuli ni changa la macho. Kama Magu alitishia kumfuta uanachama mbunge yeyote ambaye angeendelea kupinga uamuzi wa serikali wa kukwapua ile fedha ya mfuko wa korosho, na alikuwa tayari hata kumtimua Waziri mkuu, kisa tu naye anatoka kusini, unataka kunambia kama kweli Magu hataki hizo saundi za kuondoa ukomo wa urais, zingeendelea?
 
Hivi mtu mmoja aonekane anafaa kuliko watu 60 milioni ? Msione fahari kuiga ujinga wa China hata Kaka yako akiwa kubwa jinga huwezi kuwa na fahari naye. China ni kielelezo Cha ubaya wa binadamu katika kuonyesha ubinafsi wake uliopitiliza.
Nadhani wanataka kuiga ujinga wa chadema, mwenyekiti amekaa madarakani kwa miaka 16 sasa. Kama kitendo hicho ni sawa kwa chadema, kwa nini isiwe sawa kwa tanzania?
 
Katiba ni ya wananchi wakiamua Rais aongezewe muhula mwingine hakuna wa kuzuia hilo. Rais wa 32 wa Marekani Franklin Roosvert muhula wake wa kipindi cha miaka minane uliisha mwaka 1941 kwa mujibu wa katiba, lakini wananchi wakasema sisi ndio wenye katiba tunamwongezea muhula mwingine, na ikawa hivyo mpaka mwaka 1945,na hao ndio mababa wa demokrasia duniani sembuse sisi.
Tuachane na matashi binafsi,tuwaachie wananchi wakiamua aongezewe muda hakuna mwenye moral strength ya kuzuia.
Unalinganisha Tanzania na Marekani? Acheni utani mnataka tuanze kuharibu taifa hili, tumuongezee muda kwa lipi jema amelifanya kwa watanzania zaidi ya viongozi wengine waliopita?
 
Kuna mtu aliwahi kusema humu jamiiforums kwamba in politics everything happens for a reason. Akimaanisha kwamba lolote ulionalo kwenye siasa halitokei kwa ajali liko well calculated na linafanywa au kusemwa kwa sababu...
You are talking to CCM zombies in the Parliament, it is just like pounding water in a mortor.
 
Katiba ni ya wananchi wakiamua Rais aongezewe muhula mwingine hakuna wa kuzuia hilo. Rais wa 32 wa Marekani Franklin Roosvert muhula wake wa kipindi cha miaka minane uliisha mwaka 1941 kwa mujibu wa katiba, lakini wananchi wakasema sisi ndio wenye katiba tunamwongezea muhula mwingine, na ikawa hivyo mpaka mwaka 1945,na hao ndio mababa wa demokrasia duniani sembuse sisi.
Tuachane na matashi binafsi,tuwaachie wananchi wakiamua aongezewe muda hakuna mwenye moral strength ya kuzuia.
Kuna natural forces katika hilo hasa hali ya uchumi wa nchi husika. Kama raisi analeta positive impact kwenye maisha ya raia na kila mtu ananufaika na uwepo wake madarakani basi hakuna kipingamizi yani!

Hao wote mnaotolea mifano hawakuwa katika situation ambayo sie tupo. Sina hakika kama wali suggest hayo nyakati ambazo raisi aliwafanya wale mlo mmoja badala ya mitatu, walifungiwa biashara na mianya ya ajira kwa kodi kandamizi, huduma za kijamii kusua sua hasa afya, uhuru wa kujieleza ukikandamizwa, kudhulumu pensheni za wastaafu na wanachama ambao wameacha kazi kabla ya umri wa kustaafu, inshort mambo mengi yakiwa kinyume na matarajio.

Hatuwezi kulazimishana raisi abaki madarakani kwa falsafa za kikasuku au kuiga mataifa mengine ambayo wao walipendekeza hilo baada ya hali ya wananchi wote kuwa nafuu kimaisha na raha kuzidi. Tusikubali kuburuzwa na wapumbavu wachache ambao wao ndio wananufaika na uongozi uliopo sasa ila wengi tunaumia kweli kweli. Sio sawa kabisa!
 
Hata akimua kuongeza mpk akafika miaka 200 hatuna cha kumfanya wanyonge sisi.
Uzuri haya mambo yana mwisho, kuna mahali atakanyaga waya ndo atajua hajui. Watu mnaoona wanyonge wakiamua kukichafua hamna mtu atabaki salama.

Kuna ukomo wa uvumilivu siku zote mtu akiwa abused kwa muda mrefu huwa anadevelop roho ya ukatili automatically.
 
Hivi mtu mmoja aonekane anafaa kuliko watu 60 milioni ? Msione fahari kuiga ujinga wa China hata Kaka yako akiwa kubwa jinga huwezi kuwa na fahari naye. China ni kielelezo Cha ubaya wa binadamu katika kuonyesha ubinafsi wake uliopitiliza.
Kwanza tumemvumilia sana,na amezeeka.Atupishe hata leo.
 
Maamuzi ya kubadili vipengele vya katiba lazima yafanye na wananchi sasa kupitia referendum kama ilivyo kwa katiba nzima. Wakifanya hao wawakilishi, itakuwa ni kwa maslahi binafsi na wananchi mbele ya safari wataona hiyo katiba si yao.
 
Back
Top Bottom